Yahya Jammeh aongezewa miezi mitatu na bunge

Farudume

JF-Expert Member
Jan 10, 2013
3,946
3,687
Bunge la Gambia limemuongezea Profesa,Dr.Yahya Jameer kwa miezi Mitatu zaidi.Hii ni baada ya kutangaza hali ya hatari na kusema kwamba uchaguzi uliingiliwa na Mataifa ya Nje.
Kesho Rais Mteule anategemewa kuapishwa.

My Note.

Huyu jamaa ni aibu kwa afrika.Viongozi wa Afrika wajitahidi kutawala kwa kufuata katiba ili muda wa kuondoka Madarakani ukifika waondoke kwa Amani.
 
Huyu jamaa ni aibu nyingine kwa mtu mweusi!
Na kwa sababu wananchi wake wameshamkataa, ili AU isionekane ni muungano uchwara waingilie kati kama nchi za ukanda huo zilivyokwisha amua na kumfurumusha kwa nguvu liwe fundisho kwa madikteta wengine barani. Wanaoikataa ICC hapo ndipo wataona umuhimu wake.
Anajihami na jeshi lakini ukifuatilia habari za Gambia kwa karibu ni wazi na mgawanyiko wa jeshi utadhihirika muda sio mrefu. Idadi ya mawaziri na mabalozi waliomkana hadi sasa inatosha kuhalalisha zoezi la kumuadabisha.
 
Wale wanajifanya ni madikteta watazame saga la Gambia na ni lazima atoke madarakani tu maana hata wanajeshi wa Gambia hawawezi kumtetea mpuuzi huyo.
 
Nchi nyingi za Kiafrika hasa Kusini mwa Jangwa la Sahara Demokrasia yao ni Kama Gambia.
Hii ndio sababu zinzng'ang'ania kujitoa ICC.
 
Yahya-Jammeh.jpg

Bunge la Gambia limeongeza muhula wa Rais wa Gambia Yahya Jammeh ambao unakamilika siku ya Alhamisi kufuatia kushindwa kwake kwenye uchaguzi kwa siku 90.

Bunge pia limeidhinisha uamuzi wa Jammeh wa kutangaza hali ya tahadhari ya siku 90, katika taifa hilo dogo la Afrika Magharibi.

Viongozi wa kanda wametishia kutumia nguvu za kijeshi kumlazimisha bwana Jammeh kuondoka madarakani, ikiwa atakataa kusalimisha mamlaka kwa rais mteule Adama Barrow.

Maelfu ya watalii raia Uingereza na Uholanzi wanaondolewa kutoka Gambia.

Nchi hiyo ni maarufu kwa watalii kutokana na fukwe zake.

Jammeh atangaza hali ya tahadhari ya siku 90Nigeria kumpa hifadhi rais Yahya Jammeh iwapo atajiuzuluBuhari kuongoza mazungumzo kuhusu GambiaWaziri wa habari Gambia akimbilia SenegalWatalii waondolewa Gambia

Gambia ilitumbukia kwenye mzozo baada ya bwana Jammeh kukataa ushindi wa bwana Barrow kwenye uchaguzi wa tarehe mosi mwezi Disemba.

Viongozi wa kanda wameshindwa kumshawishi Bwana Jammeh kuwacha madaraka.

Nigeria imetuma meli ya kivita kumshinikiza bwana Jammeh kuondoka madarakani.

Muungano wa nchi za magharibi mwa Afrika Ecowas, umeandaa kikosi kinachoongozwa na Senegal lakini bado unasema kwa hatua za kijeshi ndizo zitakuwa za mwisho.

Source: Freedomnewspaper online
 
Africa for Africans! Ni ulafi wa madaraka kwa viongozi wa kiafrika
 
Wabunge wa chama cha Jammeh wapo 64, wa upinzani 4, Jammeh alitaka hali ya hatari itangazwe alijua lazima bunge litapitisha.
Kinagaubaga hii siyo hali ya hatari ila ni kujitafutia muda zaidi kipindi anatafuta njia ya kumfanya aendelee kubaki madarakani.

ECOWAS hawataingilia, kwakua wataonekana wameenda kinyume na sheria ambayo inamfanya Jammeh aendelee kubaki kutokaña na kutangazwa hali ya hatari.
 
Whats the difference between gambia and zanzibar?its the same situation...the only mistake which jammeh made was to accept election results...

But also adama barow is a fool...how comes outgoing president has conceded defeat then you are threatening to send him to jail or icc?
 
Kuna kipindi unatamani kusema maneno fulani lakini unamkumbuka Mungu kwamba utamkufuru. Lakini kiukweli Afrika inatia kinyaa kwa waliobahataika na kustrugle kupata maono ila kwa mzwazwa na mambumbu yanayoangalia masilahi binafsi kwao inakuwa sahihi tu.
 
Wabunge wa chama cha Jammeh wapo 64, wa upinzani 4, Jammeh alitaka hali ya hatari itangazwe alijua lazima bunge litapitisha.
Kinagaubaga hii siyo hali ya hatari ila ni kujitafutia muda zaidi kipindi anatafuta njia ya kumfanya aendelee kubaki madarakani.

ECOWAS hawataingilia, kwakua wataonekana wameenda kinyume na sheria ambayo inamfanya Jammeh aendelee kubaki kutokaña na kutangazwa hali ya hatari.
Aisee. Huyu jamaa mjanja aisee
 
Hatari yenyewe imeletwa na mtangaza hatari sasa hapo ndio utakapo elekea kuamini kuwa bara la Afrika lipo bado enzi za giza. Na ECOWAS wasipoingilia kwasababu zozote huyo mtangaza hatari hatoki hapo si kwa uchaguzi si kwa lolote hadi atolewe.
 
Back
Top Bottom