Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 360,681
- 830,653
Hili jambo miaka mitatu nyuma lilikuwa maarufu sana, yaliibuka makanisa ya mitume na manabii kwa kasi ya ajabu yaliyokuwa kila wakati yakituonyesha picha za wafu waliokufa kimazingara na baadae kufufuliwa nao.
Karata hii isiyo na chembe ya haya wala soni ya udanganyifu ikawapatia waumini wengi na umaarufu mkubwa.
Gwajima bingwa wa haya mazingaombwe kwa kujiamini kabisa aliutangazia uma wa waumini wake kuwa angemfufua Marehemu Amina Chifupa RIP, watu wakausubiri kwa hamu muujiza huu, Chifupa mpaka leo hajafufuka.
Maumivu yalibaki kwa mtoto wake na ndugu zake ambao jina la ndugu yao lilitumika kwa malengo binafsi huku magazeti ya udaku yakiwa kichocheo kikuu
Watu wote tuliowaona wakifufuliwa hatujawahi kuonyeshwa ndugu zao na historia zao, sijawahi kuona mtu wa Dar akifufuliwa au mtu ninayemfahamu, bali mtu wa dar alifufukia Arusha, wa mwanza alifufukia dar nk.
Upofu wa imani ukawafanya wengi wakimbilie kwenye haya makanisa, lakini sasa mambo yamebadilika na uongo wao umejulikana! Siku hizi kufufua misukule sio dili tena, kilichopo ambacho nacho kinakufa ni kutoa mapepo! Hivi mapepo yanakaa kwa akina mama tuuu!?
Imani ni kitu kizuri pale tu unapojitambua kuwa unaamini nini na kwa nini! Hawa manabii na mitume wa uongo wamechuma Mali nyingi kwa waumini wapumbavu! Serikali iliangalie hili kwa makini yasije kutokea yaliyotokea Uganda, Kenya na ulaya kule watu waliojiuwa kwa maelfu kwa maagizo ya viongozi wao wakiamini kwa kufanya hivyo watakwenda peponi.