Huu mjadala unatakiwa uwe haufungamani na upande wowote ili uweze kutenda haki.
kwanza wanao tuhumu wasichukuliwe hatua za kisheria kwani ni haki yao.
Wanaotuhumiwa waendelee kutoa ufafanuzi maana wapo watu wenye uelewa wa kuchambua chuya na mchele.
CIG amebainisha kisomi mno ni lazima wanaojibu watumie usomi wenye kiwango kilekile.
Mimi nimesikiliza hoja za pande mbili tatizo linabakia sehemu moja tu kwamba ni kwanini majibu mazuri yaliyotolewa leo hayakutolewa kipindi cha ukaguzi??mpaka mzee wa watu kuamua kutoa riport baada ya kukosa maelezo?
Hatahivyo naamini hakuna nia ovu wala hakuna wizi bali ni technicalities za kiuandishi na watu kupata hoja ili kujiinua kisiasa na hii ni sawa na padre kukutwa anafanya dhambi au Mwalimu kufeli mtihani.