Yahusu kuchanjiwa muku

Class mate wangu alishiriki vita ya Uganda, aliporudi alinihadithia aliyoyaona ni balaa,
Naamini Nyerere alikuwa na lengo zuri sana kuzuia "UMANGARIBI" haya ma TV ndio yametufanya tuone utamaduni ni ushamba, tungeendeleza yetu si ajabu leo tusingekuwa na magonjwa ya ajabu ajabu hivi.. Unaenda kuongea na babu anakupa dawa mambo yanakuwa fresh, siku hizi mpaka mionzi, na unakufa
 
Dawa nyingi zinatokana na miti shamba, binafsi natumia remedies tu maishani ni tiba asilia mpaka wanangu
 
napenda kufahamu kama ukichanjiwa unaweza ukatolewa au kuiondoa mwilini mwako
 
Mkuu umenikumbusha kisa cha bibi yangu mzaa baba, alikufa kifo cha mateso sana!! Alianza kuugua 2004 akafa mwaka jana 2015... Cha ajabu wakati yupo hospitali ameoza upande mmoja hatamaniki baba akaota ndoto aende kijijini kwao kuna kitu kipo kwenye sanduku la huyo bibi akakichome moto...
Kweli alikwenda na kukikuta alipokichoma moto tu huku akapigiwa simu toka mbeya mjini bibi kakata roho!! Japo hakuwahi tusimulia ni nini hasa alichoma but hali ndo hiyo.
 
yaani hii thread nimeipita mara nyingi, na kila nikipita hilo neno muku nilikua naliona tofauti...
hahahaha....aisee.kuna wengine nadhani wameshajaribu kuligeuza ili kuona kama litaleta maana waitakayo.
nimeshaisikia sana habari za watu kuchanjwa dawa za kujikinga na kifo na wengine kuwa na hirizi zinazo uhai.
 
Lakini pia hii ya kuugua mpaka kuoza lakini mtu hafi inatokana na maagano nadhiri na viapo hasa na nguvu za giza...huyo mtu hafi mpaka atengue hayo mambo
 
Mkuu natamani niseme kitu lakin mdomo unakuwa mzito....
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…