Tunakuuliza wewe utajibu vipi?.. au wataka hao Chadema wakujibu vipi.. frankly kama mimi ni kiongozi wa Chadema sintakuwa na jibu, ikiwa wewe hukupata jibu toka ktk katiba,sera, na ilani za chama - sijui unategemea jibu litoke wapi kujibu swali lisilojulikana..
Chadema ni tumaini kubwa sana kwa wengi wetu na kwa muda mrefu limekuwa kwangu ni tumaini vile vile. Lakini bado haijataka kuvuta mstari ule wa kiungozi kwa miaka kadhaa sasa. Siamini kama ndani ya siku chache zilizobakia wataweza kuvuka mstari huo. Na watakapogundua kuwa walipaswa kuuvuka watajikuta wanagalagazwa kwenye uchaguzi mkuu huku wakilalamika "CCM", "Tume ya uchaguzi", "Wizi wa kura", "Vyombo vya dola".
MM
Chadema ni tumaini kubwa sana kwa wengi wetu na kwa muda mrefu limekuwa kwangu ni tumaini vile vile. Lakini bado haijataka kuvuta mstari ule wa kiungozi kwa miaka kadhaa sasa. Siamini kama ndani ya siku chache zilizobakia wataweza kuvuka mstari huo. Na watakapogundua kuwa walipaswa kuuvuka watajikuta wanagalagazwa kwenye uchaguzi mkuu huku wakilalamika "CCM", "Tume ya uchaguzi", "Wizi wa kura", "Vyombo vya dola".
MM
Kwa kadiri ya kwamba lengo ni kutaka tu kuwang'oa CCM madarakani halafu ndiyo mfikirie mtafanya nini kwa taifa na kutuambia basi mtaendelea kuwa wasindikizaji kama ilivyokuwa kuanzia 1995 hadi sasa na itakavyokuwa milele na milele.
Bila ya shaka, lakini tushikamane kwenye kitu gani? bado naambiwa "kuing'oa CCM madarakani"; nauliza ili kiwe nini? jibu "ili itoke madarakani", nauliza halafu kifuate nini? naambiwa "hilo si la msingi kwa sasa kujua, tukishawatoa madarakani ndiyo tutawaambia"! Well.. mshikamano wa namna ndugu zangu nyie shikamaneni na ng'anganianeni kabisa na mgandane kama yule sungura alivyojagandishwa kwenye sanamu akidhania anaikomoa kule shambani.
Mzee mimi sijaelewa unaposema wanataka kuiondoa CCM halafu basi, ni nani atakayewapa kura? je hii CHADEMA haina manifesto, watakayotumia kusema watawafanyia nini watanzania? ni kweli hawana wanachokipanga? mimi siamini hilo. Labda mzee tusubiri mkutano mkuu wa CHADEMA ni lazima watatuambia watatufanyia nini. Hakuna shaka kwamba CHADEMA ndio wamekuwa mstari wa mbele kupinga ufisadi wa Meremeta, Tanggold, Kagoda, Mwananchi Gold, EPA etc,na wamekuwa wakiishinikiza serikali mpaka dakika ya mwisho ichukue hatua, halafu wasituambie kuwa wakiingia madarakani watawafanya nini hawa watu? Hapana mzee tuvute subira, kama kwenye ilani yao hawataweka hilo, mimi nitakuwa wa kwanza kuwakataa.
Nadhani labda unafikiria namaanisha CCM ising'olewe madarakani. Mbali kutoka hilo. Ninachomaanisha ni kuwa CCM kuondolewa madarakani haliwezi kuwa lengo na ajenda ya uchaguzi kwa sababu kuondolewa kwa CCM kunakuwa ni matokeo ya kukubalika kwa sera, mipango, na ahadi za CHADEMA. Sera, mipango na ahadi hizo ni lazima ziweze kuwashawishi wananchi kuwa CCM ni mbaya na hafai; ni lazima ziwe bora na zinazowezekana kuliko zile za CCM. Nje ya hapo CCM haiwezi kuondolewa madarakani kwa kuunganisha chuki dhidi yake. Kwa sababu kama mnavyoona kuna watu wanaoipenda CCM kwa kiasi cha ajabu zaidi na wengine licha ya kujua ubovu wa CCM bado wanajipanga mstari na kuishangilia.
Hivyo, ni mambo gani Chadema inaahidi kuyafanya na kwa muda gani ambayo ni bora kuliko ya CCM ambayo yatafanya wananchi waikatae CCM na hivyo kuing'oa madarakani? Maana kama leo JK anasema atajenga Chuo Kikuu kingine, Hospitali, barabara na akaonesha "mafanikio" ya CCM Chadema wataonesha nini au kuahidi nini zaidi ya kile cha CCM?
Kwa mfano, mkisema ufisadi JK atasema wamepeleka watu kadhaa mahakamani, fedha za EPA zimerudishwa, watu wamefukuzwa kazi n.k Chadema itasema nini juu ya hilo ambalo ni bora kuliko hilo? Si tumeona wapinzani kama kina Mrema wakisifia juhudi hizo na hata baadhi ya wana Chadema wenyewe?
pole pole karibu unanipata...
mwenzenu Obama alisema mapema kabisa kuwa akiingia madarakani atafanya nini... watu hawakuwa na kukisia kuwa sera yake ilikuwa ni kuwaondoa tu republican madarakani halafu mengine yangekuja mbele ya safari. Wapiga kura waliambiwa sera za Obama kuhusu Guantanamo, vita, uchumi n.k
Msiulize ulize maswali mengi kwenye kazi za watu!. Wata wanauliza tuu, wanauliza tuu, wanauliza tuu na hawajibiwi, hivi hamuelewi tuu!.
Na wewe endelea kuuliza.
Mkuu wangu wewe ndio hujui dhamira ya Marekani kwenda Iraq lakini sisi tunajua na haina kificho isipokuwa wamekutana na vichaa wenye historia ya kutotawaliwa. Hawapewi pumzi ya kuyafanya waliyokusudia kuyafanya..
Hata siku moja Marekani haendi mahala pasipo malengo na wanaweza hata kutunga itikadi ili mradi malengo yao yakubalike kwa wajinga kina sisi tusioona nje ya CNN. Kumbuka mwisho wa yoote haya siku zote - TRUTH wil prevail!
.........this reminds me of a certain Comical Ali (Sadam Hussein's defence minister).well kama inakufanya ujisikie vizuri "asante"..
Pengine Mwanakijiji unatumia lugha ngumu kueleweka.Pengine tatizo liko kwangu kwamba ni mgumu kuelewa.Lakini hadi sasa nashindwa kabisa kukuelewa unapojaribu kuonyesha kuwa ufumbuzi wa matatizo yaliyopo nchini mwetu hautopatikana kwa kuing'oa CCM madarakani.
Inawezekana pia japo nilifaulu PS 101 pale Mlimani katika mwaka wangu wa kwanza,sikumwelewa Mhadhiri aliyekuwa akifundisha somo hilo (wakati huo) Dkt Max Mmuya ambaye katika mihadhara yake alikuwa akitueleza kuwa mmoja ya maelngo makuu ya kuanzisha chama cha siasa ni kukamata dola.Na hiyo,kwa namna flani,ndio inatofautisha political parties from interest and pressure groups.
Lakini hata kama wakati huo akili yangu ilikuwa changa kukamata mafundisho hao muhimu kuhusu siasa,nimetumia muda mwingine wa kutosha kusoma na kutafiti siasa kama stadi (hasa katika namna theory zinavyoendana au kukinzana na uhalisia uliopo).Na katika muda wote huo sijakutana na maandiko au njozi kwamba moja ya malengo ya msingi ya kuanzisha chama cha siasa sio kukamata dola.Umuhimu wa chama cha siasa kukamata dola unatokana na ukweli kwamba ili sera zake ziweze kufanya na/au kufanyiwa kazi ni lazima kiwe na mamlaka ya kiutawala na dola kwa umma.Na mfano mwepesi ni namna "sera za kipekee za CCJ" zitakavyoendelea kubaki "sera nzuri tu" pasipo namna ya "kulazimisha utekelezaji wake" kwa vile chama hicho hakijakamata dola.Na ni katika namna hiyohiyo,tunalazimika kukubali mabaya mengi tusiyotaka kuhusu CCM kwa vile tu chama hicho kina mamlaka ya kutekeleza matakwa yake-tupende tusipende.
Kwa vile wewe ni mchambuzi mzuri wa siasa zetu,naamini unafahamu fika kwamba kikwazo kikubwa cha maendeleo yetu ni CCM.Sasa pasipo kuondoa kikwazo hicho tutawezaje kufikia mema tunayotaka kuyafikia?Au mwenzetu utuelezeje njia mbadala ya kufikia malengo yetu wakati CCM imekumbatia dola,na kutumia vyombo vya dola kukandamiza vyama vingine vya siasa na walalahoi kwa ujumla.
Siasa na utabibu ni fani mbili tofauti lakini zinaweza kuafikiana katika namna hii:kama una matatizo ya kiafya yanayosababishwa na uvimbe unaokwaza damu kufika mahala fulani,ufumbuzi pekee ni kuundoa uvimbe huo unless kwa kuuondoa mgonjwa atakufa.Ni katika namna hiyhiyo ndio maana baadhi ya majeruhi wa ajali au vita hushauriwa kukatwa viungo vyao ili waendelee kuishi hususan kama sehemu zilizoathiiriwa zinaweza kupelekea usaha au kuoza na kuusababishia mwili madhara makubwa zaidi.Na katika siasa,ufumbuzi ni kuondoa kikwazo kinachokwaza nchi kupiga maendeleo.Na ndio maana ufumbuzi wa kadhi na uonevu wa mkoloni dhidi ya wenye nchi ulikuwa kumg'oa mkoloni.Na pia Nduli Idi Amini alipovamia Tanzania,ufumbuzi pekee tuliobakiwa nao ni kumtimua,na pel tulipoweza tukamng'ao kabisa katika utawala.
Sasa iweje kuindoa CCM madarakani kusilete ufumbuzi?Unauliza tukishaing'oa CCM itafuata nini?Kwani mwanamke anayeishi kwenye manyanyaso katika ndoa akishamtaliki mumewe mnyanyasaji kinafuata nini?Au kama gogo limeziba barabara na hivyo kukwaza magari kupita,likishaondolewa kinafuata nini?
Kuna wakati tunaoaswa kuangalia uhalisia na kukepuka matamanio ya kutaka njozi zigeuke kuwa uhalisia.Kuna wanaotaka Watanzania "waende darasani kwanza" kabla ya kuanzisha jitihada za kujikomboa.Wanachosahau ni kwamba kuna uwezekano mkubwa "tutakapohitimu somo la mbinu za kujikomboa na kujitawala" tunaweza kukuta hakuna mahala pa kufanyia kazi "kanuni tulizofundishwa darasani" kwani nchi itakuwa imeshauzwa.
Na jibu jepesi kwa swali "je CCM ikishatoka madarakani kinafuata nini" linaweza kupatikana kwenye mfano halisi wa je baada ya kumuondoa mkoloni au kumtimua nduli Idi Amin kilifuata nini.
inanikumbusha kisa cha jamaa walioenda kuwaokoa watu waliokuwa katika shida; watu wale kwa vile walikuwa katika shida walikumbatia kwa haraka "waokoaji" wao hao ambao walisema wamekuja kuwatoa katika shida zao. Baada ya kutoka kwenye shida wakawauliza waokoaji wao "sasa mnatupeleka wapi"? waokoaji wakasema "msiwe na wasiwasi tutajua baada ya muda si mrefu, nyie tufuateni tu".. guess what happened?
Sera ya Utawala
Utawala wa Ukiritimba na Urasimu, ukoje?
Ii this not good enough as an answer to your 'what then' question? Labda tatizo ni wewe kudhani kuwa unajua zaidi ya wengine!
- Serikali kuu inaingilia mamlaka ya Serikali za mitaa. Katiba haipo wazi juu ya mamlaka ya serikali za mitaa.
- Serikali ni kubwa mno na haina ufanisi.
- Halmashauri za Wilaya zimebanwa, hazina uhuru wa kutosha na zinaingiliwa na watawala kutoka Serikali kuu.
- Wakuu wa wilaya wanaingilia utendaji wa halmashauri za wilaya na kudhoofisha demokrasia.
- Mikoa ni mingi sana na haina ufanisi kiutawala na kiuchumi.
- Mfumo wa Muungano ni tata na hautoi nafasi kwa Muungano mkubwa zaidi wa shirikisho la Afrika Mashariki.
Serikali ya CHADEMA itaondoa ukiritimba na urasimu kwa kufanya yafuatayo.
- Cheo cha Mkuu wa Wilaya kitafutwa na kazi zote za Ofisi ya Mkuu wa Wilaya zitajuimshwa na Kazi za Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya/Mji/Manispaa/Jiji pamoja na Meya.
- Halmashauri za Wilaya zitapewa mamlaka na uhuru zaidi kwa mujibu wa Katiba Mpya itakayotungwa kwa ushiriki wa wananchi.
- Mfumo wa serikali za mitaa utaimarishwa kwa kuimarisha serikali ya Kijiji kama chombo cha msingi cha uongozi (governance).
- Mameya watachaguliwa na wananchi moja kwa moja na watakuwa na majukumu ya utendaji pia.
- Mikoa ya sasa itaunganishwa na kuwa na mikoa kumi tu ili kuwezesha ufanisi wa kazi na pia kuleta ushindani wa kiuchumi miongoni mwa mikoa ndani ya nchi.
- Mikoa itakayoundwa itakuwa na mabunge yao na kuchagua viongozi wao kidemokrasia.
- Tutarekebisha mfumo wa Muungano ili kuiweka nchi tayari kwa shirikisho la Afrika Mashariki bila kuathiri uhuru na dola ya Zanzibar na Tanganyika.
- Mabadiliko yote ya mfumo wa Utawala wa nchi yatafanywa kufuatia zoezi la kutunga katiba mpya nchi kufuatia
- Mkutano Mkubwa wa Katiba utakaoshirikisha wananchi wote.
- Nafasi za uongozi wa serikali zitakuwa na mtazamo mkubwa wa kijinsia.
- Serikali itakayoongozwa na CHADEMA itahakikisha nafasi za Mawaziri, Manaibu Mawaziri na Makatibu Wakuu zinashikiliwa na idadi ya kutosha ya Wanawake ili kuweka uwiano wa kijinsia katika utawala wa nchi.
- Serikali ya CHADEMA itahakikisha kunakuwa na usawa wa kijinsia katika nafasi za uongozi katika Mahakama na
- Bunge kwa kutoa kipaumbele kwa wanawake wengi zaidi kusomea sheria na kuajiriwa kuwa mahakimu wa mwanzo, wa wilaya na mahakimu wakazi na baadae kuwa Majaji.
Nilifahamu juu ya mazungumzo ya baadhi ya uongozi wa juu wa CCJ na Chadema kwa muda kidogo; Yalitokana vile vile na ushauri wa watu mbalimbali kuwa CCJ iunganishe nguvu na Chadema. Hata hivyo hadi hivi sasa kilichofanyika ni baadhi tu yaviongozi wake kujiunga na Chadema na siyo CCJ nzima. Kuna sababu.
Wapo wanaosema kwa vile hawa ndugu zetu wameingia Chadema basi CCJ na wazo la CCJ nalo limekufa kwa hiyo sote tuliounga mkono CCJ tuinamishe vichwa vyetu kwa kushindwa na kujiunga na Chadema. Hizi ni fikra potofu. Ni potofu kwa sababu zinafikiria Chama kikifa au kikishindwa ina maana mawazo yake nayo yameshindwa. Yanafikiria kuwa kama watu wakitoka kujiunga na chama kingine au kutoka katika siasa maana yake siasa za chama hicho nazo zimeshindwa.
Ukweli unabakia kuwa ukweli kwamba siasa za kutaka ushirikiano wenye lengo la kuitoa tu CCM madarakani halafu ndiyo tujue tunataka kufanya nini ni siasa ambazo katika dhamira yangu siwezi kuziunga mkono. Siasa za kutosema nini unataka kufanya, kwa vipi na kwa muda gani ukionesha ukali kuhusu ufisadi miye siziwezi kwa sababu niaamini tatizo la Tanzania ni ufisadi kuliko kitu kingine chochote kile.
Kutuambia kuwa "panya hawakamatani" lakini hutuambii wewe utawakamata vipi na kwa namna gani, haitoshi vile vile.
Chadema ni tumaini kubwa sana kwa wengi wetu na kwa muda mrefu limekuwa kwangu ni tumaini vile vile. Lakini bado haijataka kuvuta mstari ule wa kiungozi kwa miaka kadhaa sasa. Siamini kama ndani ya siku chache zilizobakia wataweza kuvuka mstari huo. Na watakapogundua kuwa walipaswa kuuvuka watajikuta wanagalagazwa kwenye uchaguzi mkuu huku wakilalamika "CCM", "Tume ya uchaguzi", "Wizi wa kura", "Vyombo vya dola".
Ninawatakia kila la kheri wale wanaojiunga na Chadema wakiamini kitabeba matarajio yao. Hiyo ni demokrasia na kwa hakika kabisa nawatakia mafanikio.
Kwangu mimini bora nirudi na kutokuwa na chama nikiendelea kusimamia fikra na itikadi na mambo ninayoyaamini kuliko kupanda treni ambalo siju linakwenda wapi na kwa nini ati kwa sababu wengine wamepanda na wanashangilia!
Kundi zima la wabunge wa CCM wanaweza kutoka baada ya bunge kuvunjwa na kujiunga na Chadema na kutoka hao akapatikana mgombea wa Urais wa Chadema kama inavyotarajiwa. Hii inaweza kuwa habari kubwa sana na mtikisiko kwa jukwaa la siasa. Kwa wengine hilo laweza kutosha kabisa kufanya waamini kuwa saa ya mabadiliko imefika. Kwangu mimi bado nitaangalia kwa macho ya shuku hadi nijue wanataka kufanya nini. Wakisema wanataka tu KUINDOA CCM MADARAKANI au KUONGEZA IDADI WA WABUNGE, nitawaangalia halafu nitacheeeeeeeka!
Chadema kinaweza kabisa kuwa chama ambacho kitachukua uongozi wa nchi mwaka huu, endapo tu KITATAKA.
MM