Yafuatayo yafanyike Simba SC kuelekea 'Derby' yetu na Wao Jumapili tarehe 16 April, 2023

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,694
109,126
1. Wachezaji wote wa Simba SC wapokonywe Simu zao.

2. Timu iweke Kambi sehemu ya Siri mno na Waandishi wa Habari wasiruhusiwe kufika.

3. Wachezaji wote wa Simba SC, Benchi la Ufundi na wale Makomandoo (watu wa maandalizi na kamati za kimkakati) walishwe Yamini ya Kiapo na Uaminifu.

4. Aliyekuwa Kocha wetu Msaidizi Seleman Matola, Wachezaji Aishi Manula, Jonas Mkude, Henock Inonga pamoja na Meneja Rweymamu bila kumsahau na Mkuu wa Itifaki, mzee wa suti 24/7 Makoye watizamwe kwa jicho la umakini/kiungalifu mno.

5. Watumike hasa wataalam (mafundi) wa Zanzibar na yule mtu wetu muhimu mwenye mamlaka makubwa ya kiimani na kimaamuzi katika dini/imani fulani nchini (ambaye pia ni mwana Simba SC lia lia na ndiyo alitusaidia kumfunga Horoya FC zile Goli 7) waicheze hii mechi na tusimtumie yule mtu wetu wa Morogoro na Rukwa kwani ni wepesi kushawishika kama matapeli na wafujaji wa pesa za Tanzania Kampuni ya MSG wakiwafuata kuwapa pesa ili watoe siri za Simba SC.

6. Kikosi cha Simba SC kitakachoanza (First Eleven) kisitajwe (kisiwekwe) mtandaoni haraka isipokuwa dakika 15 kabla ya mechi kuanza.

7. Mzigo wa Timu (watu wa mpira na fitna mtakuwa mmeshanielewa) asipewe Mchezaji wa Kigeni na Mkristo bali apewe yule yule Mzawa na Muislamu, ila ajitahidi mno Siku ya Mechi amkwepe sana Bakari Mwanyeto au Farid Musa au Mudathir Yahaya ambao ndiyo huwa Wabeba Mikoba Wao Wakuu.

Kwa Kujiamini kabisa GENTAMYCINE leo tarehe 11 April, 2023 hapa hapa JamiiForums nasema kuwa kwa 100% Yanga SC anaenda Kufungwa na Simba SC tarehe 16 April, 2023 na naziona Goli 3 au 4 kama Wakijaa katika Mfumo wetu japo najua Goli 2 kwa 0 ziko na Wakibahatika basi na Wao wataambulia Goli 1 tu ila all in all Safari hii Yanga SC inaenda Kufungwa na Simba SC na naomba huu Uzi wangu Utunzwe na tukutane hapa Jumapili Usiku baada ya Mechi au Jumatatu ijayo.

Kila la Kheri sana Simba Sports Club.
 
Kila la Kheri Simba Sports Club.
Kila mechi mnafanya hizi mambo na tunawakanda kama kawa.
 
Tuliopo magroup ya yanga kule wanachangishana pesa kila derby kuloga baadhi ya wachezaji wetu muhimu, na mchezo wao unaendelea nnavyokwambia kwa sasa wanashugulila na beleke, chama, kanoute na manula, na simba wanalijua hili ila mpo kimya mnafungwa kindezi ndezi kila mwaka, akiroga rogaaa
Tunalijua hili Mkuu na ndiyo maana unaona GENTAMYCINE leo Siku Tano kabla ya Derby nimeamua Kutahadharisha / Kuwatahadharisha haya Mambo muhimu na ya msingi ili haraka sana wayafanyie Kazi.
 
Kama mnaamini uchawi unacheza Mimi nitawachangia pesa pia pia tuone uchawi unavyoifunga Widas Casablanca.

Ni ujinga wa hali ya juu karne ya 21 kuwaza ushirikina, mbona Sumbawanga hawana timu? Handeni hakuna timu? Ngende hakuna timu?
 
Baleke amepelekwa kwa mkopo Simba baada ya kutokuwa na kiwango na kukosa namba TP Mazembe.

Wachezaji bora wote huwa wananunuliwa hawaendi sehemu kwa mkopo.
Tuisila Kisinda alivyokuja Yanga SC kutoka FC Berkane ulimnunua au Ulikopeshwa tu?

Jibu lako ndilo Kipimo changu kama Mpira unaujua au Unabwabwaja ( unapig Porojo ) tu.
 
Back
Top Bottom