- Thread starter
- #81
Naona kama umekwishaelimishwa. Hawa tunaowazungumzia ni viongozi wa kitaifa. Wana dhamana ktk serikali. Kuna watu wanaendelea na sherehe za arusi, wengine wanakunywa pombe, wengine wanaendelea na sherehe za ngoma. Lakini usilinganishe mtu waziri Mwakyembe, mtu ni naibu spika Tulia na watu wa aina hiyo. Waziri analisemea Taifa, TFF wanalisema taifa lipi? Ligi siyo mradi wa serikali. wanajiendesha kwa sheria zao walizokubalina sawa na chama cha kuweka na kukopa.Lea maandalizi mkubwa yaliyofanyika isingewezekana kuahirisha. Mbona hamuwaulizi TFF ligi inaendelea kama kawaida katikati ya maombolezo.
Kibaya zaidi wamesoma sheria na wanajitahidi kuonyesha kwamba ni watu wa busara. Huwezi kuongoza bunge na wizara kwa busara ndogo. Hapa siyo ushabiki na upendo kwa mtu fulani ni suala la kueleza uwezo wa akili ya mtu wa maana na asiye wa maana. Waungwana wote, hata msiba wa kibaka wanaigiza kuumia ili wasivishwe lawama.
Hawa ndugu kwa pamoja wanatakiwa watueleze sababu ya kutumia vyeo vyao vya kitaifa vibaya kwa kuendesha sherehe, wakati Taifa liko ktk maombolezo