Yaani tamasha la Tulia limeendelea bila kujali maombolezo!!

Yaani tamasha la Tulia limeendelea bila kujali maombolezo!!

Dah! Hata kuigiza maombolezo hawawezi! Bahati mbaya sijawahi kumsikia waziri Mwakyembe akikubali kosa lolote lile zaidi ya kuwatishia wanaomkosoa. Hili nalo anasababu ya kushiriki tamasha, hata baada ya kutangaziwa siku za maombolezo? Eti akashiriki nyimbo za maombolezo! Kweli?
Hiyo ndiyo ccm tunayo ijua hayo mengine ni maigizo
 
Sawa lakini akili yenyewe ni hiyo? Kama rais alivyosema, huu siyo mtaji wa kisiasa lakini mtindo huu wa kutojali mambo makubwa ya kitaifa, ana tatizo.
Hata hivyo huyo Tulia akisimama na Sugu kwenye uwanja ulio sawa basi Tulia atatulizwa mapeema sana
 
Na kibaya zaidi ilo tamasha ni kwa ajili tu ya Ubunge, yani madaraka matamu kuliko uhai wa watu, na sitoshangaa kuona hakuna mtu anajiudhuru kwa hivi vifo, wakati kama serikali ingesimamia vyema kupakia watu na mizigo kulingana na uwezo wa kivuko, leo tusingekua tumepoteza ndugu zetu kwa kiwango hiki. Ila hawajali sana sana watakwambia ulitaka sisi ndio tuwazuie kupanda?
Hayo ndiyo majibu yao mepesi kwenye mambo ya kuuzunisha
 
Hii ni aibu kubwa.. Mh. Rais mkemee kabisa huyu Tulia mroho wa madaraka hadi kasahau tuko ktk maombolezo.. Huyu hafai kabisa kuwa kiongozi, hafai kabisa..
 
Wabongo kwa siasa, huku kwetu unyakyusani huwa tunaimba misibani

"Kwa kyala akajapo ntali, nsekele nnini," *3
 
Back
Top Bottom