Yaani kukaa bila ajira ni noma, kwa muda mrefu

Yaani kukaa bila ajira ni noma, kwa muda mrefu

Hii ni aibu sasa kwa wanachuo.
Hivi unashindwaje kuomba mtaji wa Elfu ishirini ukanunaa Machungwa au matikiti kwa jumala Pale Burguruni ukauza mtaani?
Kama mnatembea na vyeti hii hali ni mbaya sana,unakuwa na Bachelor yako kisha muuza mahindi wa njiani unamuona kama Do king unatamani umuombe kipande cha muhindi ili angalau upate stim za kunywa maji mengi.
Tatizo ni Aibu nakuona kwamba ni wasomi na wengine kufanya kuishi maisha Fake eti kisa wasomi

Boss unaongea tu but in practice haiko hivyo fikiria mtoto wa maskini anamaliza chuo huo mtaji atapata wapi, je mtaji wa elfu ishirini !? hiyo biashara ya machungwa ina kipato gani? labda utupe ushuhuda boss,
 
Toeni michango yenye solution, vijana wanataka muongozo sio kuwakejeli we were in the similar situation sometimes back
 
Ajira ni ngumu sana. Madogo wamerudi home kwa ajili ya likizo wamenikuta hapa sina kazi yani hakuna cha heshima mpaka nianze kuwasalimia kila siku. Mtaji nilinyimwa na mzee kwani ningekuwa mbali. Sitamani kuishi hapa tena na mpaka nimepata vidonda vya tumbo.

pole sana mkuu..hop siku it will done
 
Ajira ni ngumu sana. Madogo wamerudi home kwa ajili ya likizo wamenikuta hapa sina kazi yani hakuna cha heshima mpaka nianze kuwasalimia kila siku. Mtaji nilinyimwa na mzee kwani ningekuwa mbali. Sitamani kuishi hapa tena na mpaka nimepata vidonda vya tumbo.
Daah pole yako ndugu. Msamehe bure mzee wako. Tatizo huwaga wanafikiria maisha rahisi kama wao kipindi hicho. Mimi mwenyewe nilikusanya hela ya kutosha ili niweze kujiajiri nikitegemea mzee atanipa tag kunipa zana muhimu kwa ajili ya biashara hiyo. mwisho wa siku alinitosa asee nilisikitika sana!
 
Kipindi ukiwa chuo unakuwa unajipa, hope, baada ya miaka mitano nikimaliza chuo nitakuwa na maisha mazuri sana! Kumbe baada ya miaka mitano unakuwa bado hujapata ajira tokea umalize chuo ni noma.... Baada ya miaka mitano kumbe hata kupata mulo ni bahati na bachelor degree yako!!! Hivi kijana kama huyu akisikia dili lolote lile lazime afanye ili hata apate uhakika wa kupata mulo! Kama unabisha kuwa hata kupata mlo ni bahati, baada ya kumaliza chuo acha kukaa kwa wazazi wako uone!kama ujashindia uji na mihogo! Ndio maisha ya watanzania wanaomaliza bachelor degree na kukaa gheto! Nawakilisha.

Mm mwenyewe nlijifanya mjuaji kubaki town il nipiganishe mishe,thubutuu ilifikia kipind ile asubuh nanunua mihogo yang ya kukaanga mingi hiyo ndio nitolee had kesho yake, nkasalit mwenyewe amri
 
Daah pole yako ndugu. Msamehe bure mzee wako. Tatizo huwaga wanafikiria maisha rahisi kama wao kipindi hicho. Mimi mwenyewe nilikusanya hela ya kutosha ili niweze kujiajiri nikitegemea mzee atanipa tag kunipa zana muhimu kwa ajili ya biashara hiyo. mwisho wa siku alinitosa asee nilisikitika sana!

Tena umkute ndio mzee wa kikoloni ni shidaa hadi na kodi ya meza anakudai bila noma
 
Shule inakufanya uwe mtumwa wa kufikiria kuajiliwa. Ila amini hakuna tajiri (asiye mwizi) aliyeajiriwa.
Tumia akili yako iliyonilewa shule kufanya kitu hata cha mtaji mdogo sana ila kwa ustadi mkubwa sana tofauti na wenhine. Zaidi jiamini kwamba kina maisha nje ya kuajiliwa.
 
Tatizo wamekariri kuwa ukimaliza lazima ukaajiriwe TRA, bank taller and so on lakini kujiajiri wanashindwa au wengine wanaona Aibu ana degree anauza duka kwa Muhindi, endelea kukaa hivyohivyo ukigombania maandazi na mdogo wako!

""Ndugu punguza ukali wa maneno""
Jamani maneno makali sana haya alaaa!
 
Tatizo ni mindset zetu ambazo sie wa tz esp hawa wenye degree, kuna baadhi ya vijana wanania ya kujiajiri ila hao wazee na nduguzo wanataka kijana wao aajiriwe.. hapo ndipo hali inakuwa tete kijana anafunga safar anaenda mjini kutafuta kazi at the end ndo hayo yanamsibu ya pass ndefu, kusota na kuteseka... bila kujali kuwa muda unaenda umri unasonga mbele wazee wanamujitaji aoe, kijana akiwa katika lindi la mawazo huku akiwaza atawezaje kuishi na mke huku anakumbana na challanges ya kuzitafuta fursa..
Kiukweli bila kipingamizi vijana wetu wanateseka mno... kuna kipindi nawaza kuwa je huko vyuoni hamna kozi za ujasiria na ujasiri(confidence) , vijana wetu hawana confidence katika ugunduzi na ufumbuzi..

Mimi nafikir hizo degree hizo za course work zifikie muda ziboreshwe, vijana wetu hawaijui nature..the real enviroment ya wanapo elekea .na hili ni tatizo mno kwa hizi skuli za social science na baadhi ya skuli zingine...
Kwa mtizamo wangu kuna muda naona mwalimu wa sekondar wa somo la kilimo anauwezo mkubwa wa ku mfinyanga mwanafunzi akawa mjasiriali mzuri kuliko hata mchumi au mwanabiashara wa chuo kikuu...

Wito wangu.. kwa yeyote yule ambaye elimu ya tanzania imemuathiri kwa namna moja au nyingine katika swala zima la maendeleo basi aichukulie challangs hio kama case study ya kubadilisha kizazi kijacho cha ki tanzania kutozama ktk dimbwi hili kwa kuwashauri na kuwasisitizia watoto wetu kusoma hesabu mno .. maana ktk hesabu ingawa itaonekana haina reality bali itamsaidia kijana kuwa na utambuzi wa mambo kwa haraka na pia kusolve problems nyingi at a time, tuwashaur watoto wetu wapende masomo ya sayansi tangu utotoni kwa faida yake haya masomo ni kubwa mno hata kama huto ajiriwa kipitia masomo haya, masomo ya biashara, sayansi kimu na kilimo na angalau siyasa yawe ndo uti wa mgongo kuliko hata historia, lugha nk kwa kufanya haya tutaongeza idadi ya wajasiria na tutapunguza idadi ya wanasiasa then life will be smooth........,,,,,,,,,,🙂
 
Mpatapo mkopo wa bodi mkiwa chuo acheni kuwekeza kwe uzinzi,ulevi,ulimbukeni na anasa za dunia. Wapo waliotumia mikop hyo kuanzia maisha. Hakuna lisilo wezkana ukiwa na vission na kujitambua mapema. Zaidi ya hapo hakuna maisha mjini ila kilimo kijijini.
 
umenena mkuu
 
Kipindi ukiwa chuo unakuwa unajipa, hope, baada ya miaka mitano nikimaliza chuo nitakuwa na maisha mazuri sana! Kumbe baada ya miaka mitano unakuwa bado hujapata ajira tokea umalize chuo ni noma.... Baada ya miaka mitano kumbe hata kupata mulo ni bahati na bachelor degree yako!!! Hivi kijana kama huyu akisikia dili lolote lile lazime afanye ili hata apate uhakika wa kupata mulo! Kama unabisha kuwa hata kupata mlo ni bahati, baada ya kumaliza chuo acha kukaa kwa wazazi wako uone!kama ujashindia uji na mihogo! Ndio maisha ya watanzania wanaomaliza bachelor degree na kukaa gheto! Nawakilisha.

Inategemea unataka ajira ya aina gani, ukitaka ya kukaa kwenye kiyoyozi huku umefunga tai kubwa nk ni ngumu kupata, unaazia na yoyote ile kisha unaonekana na wengine wanakukubali mara ghafla unaletewa mkataba wa ajira ya heshima hapo hapo ulipo
 
Kipindi ukiwa chuo unakuwa unajipa, hope, baada ya miaka mitano nikimaliza chuo nitakuwa na maisha mazuri sana! Kumbe baada ya miaka mitano unakuwa bado hujapata ajira tokea umalize chuo ni noma.... Baada ya miaka mitano kumbe hata kupata mulo ni bahati na bachelor degree yako!!! Hivi kijana kama huyu akisikia dili lolote lile lazime afanye ili hata apate uhakika wa kupata mulo! Kama unabisha kuwa hata kupata mlo ni bahati, baada ya kumaliza chuo acha kukaa kwa wazazi wako uone!kama ujashindia uji na mihogo! Ndio maisha ya watanzania wanaomaliza bachelor degree na kukaa gheto! Nawakilisha.
Umemaliza degree ya kwanza ndo unaandika hivi! Ni haki usote kitaa
 
Back
Top Bottom