Keen
JF-Expert Member
- Sep 27, 2007
- 617
- 170
Mimi sisikitiki kuachiwa kwa zombe na team yake. Pengine kweli hawana hatia kwa mujibu wa sheria. Pengine wana JF mnisaidie kujua nani mkweli kati ya vyombo hivi vya dola: Plisi au tume iliyopeleleza hiyo kesi na jaji masati aliyetoa hukumu. Nani anaamini kipi kati ya hivi viwili na kwa nini? Mimi nadhani baada ya hukumu kutolewa jana serikali inawajibika kupitia vyombo vyake husika kuwaeleza wananchi kuwa nani waliwaua hao vijana au hatua zipi zinafata baada ya wale iliodhani walihusika kugundulika kuwa siyo!!!. Vinginevyo wananchi wataanza kukosa imani na ama polisi kwa kutoa upelelezi fake ama mahakama. Tujiandae kusikia pia kesi zote za mauji ya ndugu zetu albino zimekosa wa kutiwa hatiani!!!
Tafadhali mwenye nafasi ya kujibu swali langu la msingi "nani mkweli wapelelezi au jaji mtoa hukumu na kwa nini unaamini hivyo?"
Tafadhali mwenye nafasi ya kujibu swali langu la msingi "nani mkweli wapelelezi au jaji mtoa hukumu na kwa nini unaamini hivyo?"