Ya Zombe na ustawi wa mob justice Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ya Zombe na ustawi wa mob justice Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Shadow, Aug 17, 2009.

 1. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  LEO YAMETIMIA MANENO YA ZOMBE KWAMBA UKWELI UTAJILI KORTINI. JAJI MASATI AMEITIMISHA HILI KWA KUMWEKA ZOMBE NA KUNDI LAKE HURU. SWALI KWAKO WEWE MWANAJAMII, JE KUACHIWA KWA ZOMBE NA WENZAKE KUTAKUWA NA ATHARI GANI KWA JAMII HASA KWA MWANANCHI WA KAWAIDA? JE, IMANI NA VYOMBO VYA MAHAKAMA ITAKUWEPO? JE, KATIKA KATIKA IBARA YA 107(?) ya katiba ya URT INAYOONGELEA KUTOLEWA KWA HAKI BILA KUJALI ‘TECHINCALITIES’ IMEZINGATIWA NA JAJI MASATI? JE, TUME ILIYOUNDWA NA MH. RAIS ILIMDANGANYA RAIS NA KUTOWA MAPENDEKEZO YA UONGO? MWISHO, JE ATHARI YA HII UKUMU ITAKUWA NI KUONGEZEKA KWA VITENDO VYA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI?
   
 2. T

  Thadeus JF-Expert Member

  #2
  Aug 18, 2009
  Joined: Nov 24, 2007
  Messages: 267
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Yesteday was a very sad day for the nation. Watu wanne wamechukuliwa nyumbani kwao na polisi wakiwa hai wakakuktwa mochwari lakini hakuna mtu anayejua walikufaje? hata polisi hawajui? Shame!!!!! Watanzania tuna haki ya kujua ni nani aliwaua hao watu, hata kama itachukua miaka mia moja. The truth must be told.
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Aug 18, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,447
  Likes Received: 22,364
  Trophy Points: 280
  imani imekwisha
   
 4. W

  Wakwetu Senior Member

  #4
  Aug 18, 2009
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 157
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hakika kwa yaliyotokea kwenye hukumu hiyo ni kuwapa wananchi ruksa ya kujichukulia sheria mikononi ili wamalize kazi haraka kuliko kusubiri mahakama ichukue muda wa miaka 3 then itoe maamuzi yake ambayo hayapaswi kuingilia na mtu yeyote. Tutegemee askari polisi kuua raia na kuwaibia mali zao kisha kesi mahakamani wataachiwa huru
   
 5. R

  Rutakyamilwa JF-Expert Member

  #5
  Aug 18, 2009
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 1,869
  Likes Received: 1,165
  Trophy Points: 280
  Naomba wasifu wa the so called jaji masati na baadhi ya kesi zilizopitia mikono yake
   
 6. R

  Rutakyamilwa JF-Expert Member

  #6
  Aug 18, 2009
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 1,869
  Likes Received: 1,165
  Trophy Points: 280
  Kuna vitu ambavyo common sense inatosha kuona haki. Kama ulimchukua mtoto wangu kutoka nyumbani mzima kesho akapatikana amekufa, utawajibika kwa kifo chake. Hapa hakuna cha utaalamu wa sheria au nini!!!!! Kweli shaaban robert alisema uanasheria ni elimu ya kupingana na haki!!!!!!!
   
 7. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #7
  Aug 18, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Unajua haya mambo ya ufundi [technicalities] katika sheria ya ushaidi yanatupeleka kubaya.
   
 8. R

  Rutakyamilwa JF-Expert Member

  #8
  Aug 18, 2009
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 1,869
  Likes Received: 1,165
  Trophy Points: 280
  Uanasheria ni profession kama ulivyo udaktari. Huwezi kuwachukua medical assistants (co), assisitant medical officers (amo) ukawapa udakitari bingwa kwa vile madakitari hawatoshi. Ndicho anachokifanya rais wetu kwa kuwachagua majaji eti majaji ni wachache. Matokeo yake ni majaji wa kutoa hukumu kama hii ya zombe. Mungu ibariki tanzania, mungu mbariki baba wa taifa nyerere mwenye heri!!!!
   
 9. M

  Mbelakisa Member

  #9
  Aug 18, 2009
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jaji Masati akasome upya Sheria, Sasa atuambie ni nani aliyeua wafanya Biashara hao pamoja na dereva taxi? Jaji Masati anapingana na mapendekezo ya Jaji Kipenka? Masati damu hawa watu iko juu yako. Jaji ulitaka ushahidi upi ungetosha kukushawishi na hata ukadiliki kuwaachia huru watuhumiwa? Hii ni mbaya sana na inaleta uvunjivu wa amani ndani ya nchi. Atuambie Jaji Masati kama hawa watu walipata ajali au la? ni wazi kuwa Mh. Jaji watu wako uliowaachia huru hawakubariki na jamii ya watanzania. zzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzombe katili wa kutisha yeye ni kama nduli. leo hii ameachiwa huru. Masati hujaitendea haki jamii ya tanzania.
   
 10. R

  Rutakyamilwa JF-Expert Member

  #10
  Aug 18, 2009
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 1,869
  Likes Received: 1,165
  Trophy Points: 280
  masati, kesho una msalaba mkubwa kwa mungu, hukutenda haki na wewe dhamira yako itakuwa inakusuta tu huku uliko.
   
 11. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #11
  Aug 18, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Je, uamuzi huu wa Jaji Masati ndo msumari wa mwisho katika imani ya Mtanzania na vyombo vya sheria kama mahakama na polisi?
   
 12. l

  libidozy Member

  #12
  Aug 18, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe ni kilaza kabisaaaa!
   
 13. M

  Mubii Senior Member

  #13
  Aug 18, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 149
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kabla ya kumlaumu Jaji, tunaomba ufafanuzi wa how the prosecution was done. Huenda hapa tutapata fundisho kwamba kushitaki mtu/watu bila kujipanga vizuri kisheria inaweza kuishia mtu mwenye kosa kuachiwa huru. Hii ni challenge to the prosecutors to improve their cases. Jaji yupo pale kuamua kesi kulingana na kazi inayofanywa na prosecution na defence. Kama mmoja kati yao atazembea atashindwa kesi hata kama issue inaonekana wazi mbele ya jamii. Kama kosa lipo kwa Jaji basi tuambiwe. Kwa kweli kesi hii imewagusa Watanzania wengi kwa kuwa watu innocent wameuawa na kesi kuisha bila watuhumiwa kupata hukumu ya kosa lilofanyika. Jaji anasema walioua hawajaletwa mahakamani, je polisi siku zote hizi wamekuwa wakifanya nini?
   
 14. l

  libidozy Member

  #14
  Aug 18, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo la wengi wenu ni vilaza wa sheria na ndio maana mnahukumu kabla ya jaji kutoa hukumu yake.Mahakama haina kipengele cha kusikiliza maoni ya magazeti na hata nyie vilaza kwani utendaji wake umekamilika.Kwa ujinga na uzoba wenu mlitaka jaji apindishe sheria ili mfanikiwe kwa malengo yenu ya kisiasa,kwa hilo halitawezekana na napenda kuwathibitishia hata kesi ya Mramba na wenzake pia watashinda.Mmekuwa mambumbumbu na mazoba wa sheria kiasi hicho!mnatoa hukumu kwa watuhumiwa wakati si wajuzi wa sheria nyie vipi!?Ondokeni na ushamba wa sheria na anzeni kujifunza mambo ya sheria,pale UDSM sasa wanatoa mafunzo ya cheti nendeni mkasome na si kufuata vilaza wenzenu wa magazeti au vipeperushi uchwara hawana elimu ovyooo!
   
 15. M

  Msindima JF-Expert Member

  #15
  Aug 18, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Jamani nionavyo yawezekana hatujui sheria kabisa na ndo maana kuachiwa kwa Zombe na wenzake kumetuacha katika mshangao,nionavyo tutafute mwanasheria aje atupe japo darasa ili tuelewe jinsi sheria zinavyofanya kazi,maana tunaweza kumlaumu jaji kuwa haki haikutendeka kumbe ni sisi hatujui sheria zinavyofanya kazi,kwa hiyo kwa mtazamo wangu hebu aje mwanasheria hapa JF atupige darasa ili tuelewe jinsi mambo yanavyokwenda.

  Nawakilisha!!
   
 16. H

  Herbert Member

  #16
  Aug 18, 2009
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Ishu ya ukilaza hapa haipo. Ndio maana wanasema ukibishana na mjinga utakua mjinga. Na mchuzi mtamu ukiwa bado wa moto. Mambo mengi yanapokua yanachukua muda mrefu kutafuta ushahidi ili haki ipatikane kuna asilimia kubwa ya haki kupotea kama tulivyoshuhudia kwa zombe. Mi nadhani wakati wa adhabu za papo kwa papo so long as kuna ushahidi physical kufanya immidiate judgement decision.
  Mfano mzuri Adam Alipokula tunda la mti wa kati Mungu alipobaini kosa, hakutaka story eti ni huyu Eva uliyinipa ndio kasababisha, Mara eti Ni huyu Nyoka ndio katurubuni This is typical example ambapo kosa limitokana na mlolongo wa washiriki kama kwa akina Zombe na wenzake. Mungu alitema cheche Instantly Nyoka Utatambaa kwa Tumbo Mpaka Ukome. Na we Adam Utakula Kwa Jasho,Eva Uzae kwa Uchungu. Na haya mambo tumebakia na hii adhabu mpaka kesho hamna wa kuikwepa hata ambao hatukwepo inakula kwetu mpaka kesho. Iweje Kina zombe waachiwe kiurahisi????

  Jamani Mahakama Itulie Maana Imani imeshaisha, Hamna kesi tena huko naona watu wanasubiria Mishahara tu.
   
 17. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #17
  Aug 18, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  kama kuna any irregularities au inconviniences zozote zilizotokea ambazo zinaonyesha occassioning of injustice,nasi Court of Appeal wata-exercise their revisionary powers.
  Ila tukiendelea kupiga kelele bila ya kuwa na elimu ya kutosha kuhusu sheria then ni sawa na bure.
  Ndio maana Prosecuting side wamesema wata-appeal!
   
 18. Mzozo wa Mizozo

  Mzozo wa Mizozo JF-Expert Member

  #18
  Aug 18, 2009
  Joined: May 26, 2008
  Messages: 427
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ...sheria ni mchezo mmoja mchafu sana, hili jambo nazidi kuliamini sasa. Yaani ni kwamba some minor irregularities ndio zinasababisha hawa watu watembee huru. Hii imekuwa ni kama mchezo flani wa kuigiza...ati hawana hatia...sijui labda waliowaua watapatikana hivi karibuni.

  Ukisoma mara mashahidi sijui walikuwa hawaaminiki, testimonies zilishindwa kustand and blaah blah nyingi mno... sasa ndo wawe huru moja kwa moja? Dah.
   
 19. t

  tapeli Member

  #19
  Aug 18, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  when it comes to dealing with GOVT authorities, siku zote ni TATIZO..this zombe guy was a police..tena mwenye cheo tu, unadhani angekaa kimya bila kuhakikisha kuwa ushahidi wote ambao unaweza mletea matatizo umeharibiwa????thats what he did..he tempered with the evidence, and in criminal matters if u cant prove beyond reasonable doubts then hakuna kitu...the prosecution side could not prove thier case, coz kwa ushahidi waliyokuwa nao, haukuweza hata kureduce that murder ofence into manslaughter...yaani ni sawa sawa na bure...hakuna kitu, judgement itakapopatikana tukaisoma mtajua, I was there when it was read...no evidence to prove that those people did kill, now how do you convict? basing on hearsay??
   
 20. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #20
  Aug 18, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160

  Kevo na libidozy,

  Elimu ya kutosha kuhusu sheria ni ipi? Binafsi naomba ufafanuzi kwenye hilo!

  Nahisi nyote wawili mmekaa kwenye madarasa ya Vyuo Vikuu na "mkasomea SHERIA", kwahiyo badala ya kuwaita wachangiaji "vilaza" na majina mengineyo tuchambualie mwenendo wa hii kesi kwa faida ya forums nzima

  Kukaa pembeni na kusema "nyie ni vilaza" na "hamjuai sheria" ni tabia ya ubinafsi na kutaka kujionyesha unafahamu jambo kuliko wengine! (Anyways, ..ndivyo Tulivyo)

  Mwisho, Wakili wa Serikali hakusema kuwa watakata rufaa, bali alisema anawapelekea WAKUBWA (ingawa naye anaifahamu sheria) ile hukumu hili watoe uamuzi ndani ya siku kumi na nne!
   
Loading...