celinawetu
JF-Expert Member
- Feb 29, 2016
- 1,330
- 1,059
Tulipokuwa tunawaambia na wabunge hasa wa upinzani kuwa ununuzi wa kivuko cha mv Dar es salaam uligubikwa na ufisadi, tulibezwa sana, wataalamu wakasema hicho kivuko ni kikuu kuu, kina Zitto waliambulia matusi ya ajabu na kuambiwa sio wazalendo.
Lakini muda ulipofika kila mtu anajua kilichotokea sina haja ya kusimulia zaidi.
Leo tena ndani ya kipindi cha miaka miwili tumenunua ndege 7 tayari nne zimeshawasili, lkn mazingira ya ununuzi wake hayana tofauti sana na ununuzi wa iliyokuwa mv Dar es salaam.
Tayari ndege mbili kati ya nne zimeonekana zina hitilafu, tunapohoji upya wa hizi ndege, tunabezwa, tunaambiwa siyo wazalendo, ajabu wanaotubeza ni wale wale waliotubeza tulipohoji ubora wa kivuko cha Bagamoyo, sijui kwanini huwa hawajifunzi.
Mimi siyo mtabiri lakini naona dalili zote za iliyokuwa Mv Dar es salaam kujirudia kwa Dreamliner.
Mkuu I salute you ila risasi Ziogope maana this time wengi zitatumaliza.ndg mbovu jamani yetu macho