Ya moyoni ni siri ya moyo

Ya moyoni ni siri ya moyo

moto nkali

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2012
Posts
378
Reaction score
216
MWANAMKE mmoja wa Kitanzania
aliyefanya ukabaha kwa miaka 18 katika
miji mbalimbali ya Tanzania, likiwemo Jiji
Kuu la kibiashara la Dar es Salaam na
mingine ya Namibia, ameibuka na
kueleza jinsi alivyotenda dhambi ya
kusambaza Ukimwi kwa wanaume
wakware.
Licha ya kukiri kufanya hivyo, akisema
kwa siku alipanga hadi wanaume
watano,tena bila ya kutumia kinga
akisema alidhamiria kuusambaza
ugonjwa huo hatari alioambukizwa
akiwa katika shughuli za ukahaba.
Alijigundua ameathirika mwaka 2006.
Hata hivyo, katika maelezo yake
ameelezea kuijutia dhamira yake hiyo,
akisema alisambaza kutokana na hasira
aliyokuwa nayo dhidi ya mwanamume
aliyemwambukiza.
“Nilimchukia sana kila mwanamume,
yeyote aliyejiita mwanamume…
nilishindwa tu kuwawinda na kuwaua,
lakini dhamira yangu ilikuwa kutumia
silaha yoyote kuua wanaume kwa
sababu mmoja wao aliniua… “Ndani
mwangu nilijisemea kamwe
sitawaambia hali ya afya yangu, yeyote
anayekuja kwangu nammaliza. Kwa
namna walivyoambukiza lazima
niwaambukize’. Sijui nimewaambukiza
wanaume wangapi, lakini ni maelfu,”
alisema mwanamke huyo ambaye kwa
sasa ana umri wa miaka 32, alipotoa
ushuhuda wake kanisani nchini Nigeria
hivi karibuni
source habari leo
 
dah! Sasa pale uwanja wa fisi yale mafisi yatakuwa yamewaambukiza wangap? Tamaa za mwili znatuponza wanaume aisee alafu mzee akishanyanyuka mtu hawazi hata kondom
 
dah! Sasa pale uwanja wa fisi yale mafisi yatakuwa yamewaambukiza wangap? Tamaa za mwili znatuponza wanaume aisee alafu mzee akishanyanyuka mtu hawazi hata kondom

Hizi tamaa mwisho mwake vilio, kiukweli hali inatisha sana, sema wengi hatujapewa uwezo wa kuona hata nyuma ya pazia.
 
Huyo amejitangaza je hao wangine ambao hawajajitangaza?

unajua vitu vingine vya kutumia akili ndogo sana, wengi wanasema ugumu wa maisha ndio chanzo cha ukahaba kwa akina dada, sasa swali la kujiuliza ni je, huyu dada yuko tayari kuhatarisha maisha yake sababu ya ugumu wa maisha ili aupate UKIMWI? Je ukimwi ni bora kuliko maisha magumu?
Kumbe huyu dada anakuwa tayari ana UKIMWI,hivyo hajali lolote.
Hivyo, uzuri wa paja, kalio na umbo kwa ujumla usijeukauziba ubaya wa HIV aliyepo ndani.
 
Kuna wanawake wana maji kichwani kwao, eti nawachukia wanaume wote kisa wamempa ukimwi. WTF??

Angetulia nyumbani na kutumia kinga huo ukimwi angeupataje?

Uingereza wamechelewa sana kuleta sheria ya kumuwaisha mgonjwa kufa, hawa ndo walitakiwa wawe wa kwanza
 
Back
Top Bottom