Ya Kalenga: Ombi kwako Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Nitumie busara hii ya juu kabisa katika weledi wangu kukupa SALUTI ya KIJESHI Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu, "Jambo Afandeeee!"

Baada ya salamu ya kijeshi naomba kukuuliza afande, Hivi ACP Ramadhan Mungi ameshindwa kuweka ulinzi pale Kalenga?

Jimbo la Kalenga lenye ukubwa wa kilomita za mraba 401, lenye wakazi wasiozidi 27500, lenye idadi ya wapiga kura 16,000, lenye wazee 75%, lenye akina mama 78%, lenye wageni mahususi wa uchaguzi wasiozidi 1500, lenye umasikini 98%,

Kwanini upeleke vikosi vya kijeshi toka nje ya Mkoa wa Iringa? Vikosi toka Mtwara, Lindi, Songea, Mbeya, Rukwa nk vimewasili jua la jana katika ardhi ya Kalenga vikitajwa eti vimekwenda kuimarisha ulinzi, hivi vikosi vya Mkoa wa Iringa na viunga vyake haviwezi kweli kuimarisha ulinzi katika eneo hilo???

Afande Mangu, ninapata hofu zaidi ninapopata taarifa za kuogofya kuwa JWTZ nao wamevalishwa nguo za kipolisi na kuingia kwenye shughuli za ulinzi wa uchaguzi huo, lakini zaidi inasemekana kile kikosi toka Mtwara kilichohusika na mauaji ya Mwangosi pale Nyololo nacho kimetia timu eneo hilo,

Naomba sana Jah aepushie mbali yasije kutokea mauaji ya raia wasio na hatia kabla na baada ya uchaguzi.
 
Naona siku hizi umekuwa msemaji wa chama, Kwani kuna ubaya gani ulinzi ukiimarishwa mbona CDM wanasema wamechukua vijana 2000 kutoka Arusha kwenda kulinda kura Kalenga au Iringa hakuna vijana?
 
Mwigulu Kazini.Hapa Mangu na Mungi ambao wote ni raia wa SINGIDA ni bendera tu...ila Lema wetu na Mawazo wawe salama tu huko.
 
He he he, huu uombaji wa PO nimeupenda, vere stailishi.

Ndio uone ubaya wa kupigana gizani, hujui mwenzio keshapanga ndita ngapi, unajishtukia tu umekula hedi.

Moral of the story: Usipigane gizani, hujui how far adui yako yuko tayari kwenda, hasa unapokuwa huna nguvu.
 
Nitumie busara hii ya juu kabisa katika weledi wangu kukupa SALUTI ya KIJESHI Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu, "Jambo Afandeeee!"

Baada ya salamu ya kijeshi naomba kukuuliza afande, Hivi ACP Ramadhan Mungi ameshindwa kuweka ulinzi pale Kalenga?

Jimbo la Kalenga lenye ukubwa wa kilomita za mraba 401, lenye wakazi wasiozidi 27500, lenye idadi ya wapiga kura 16,000, lenye wazee 75%, lenye akina mama 78%, lenye wageni mahususi wa uchaguzi wasiozidi 1500, lenye umasikini 98%,

Kwanini upeleke vikosi vya kijeshi toka nje ya Mkoa wa Iringa? Vikosi toka Mtwara, Lindi, Songea, Mbeya, Rukwa nk vimewasili jua la jana katika ardhi ya Kalenga vikitajwa eti vimekwenda kuimarisha ulinzi, hivi vikosi vya Mkoa wa Iringa na viunga vyake haviwezi kweli kuimarisha ulinzi katika eneo hilo???

Afande Mangu, ninapata hofu zaidi ninapopata taarifa za kuogofya kuwa JWTZ nao wamevalishwa nguo za kipolisi na kuingia kwenye shughuli za ulinzi wa uchaguzi huo, lakini zaidi inasemekana kile kikosi toka Mtwara kilichohusika na mauaji ya Mwangosi pale Nyololo nacho kimetia timu eneo hilo,

Naomba sana Jah aepushie mbali yasije kutokea mauaji ya raia wasio na hatia kabla na baada ya uchaguzi.

Ondoeni red brigade kwanza ndio uje ulielie hapa.Serikali haiwezi kuacha wahuni wafanye wanalotaka
 
Mwigulu Kazini.Hapa Mangu na Mungi ambao wote ni raia wa SINGIDA ni bendera tu...ila Lema wetu na Mawazo wawe salama tu huko.

Pamoja na kukulia Singida kwa Mama yake mzazi lkn baba mzazi wa Mangu ni Mchaga, hivyo usiwe na wasiwasi!
 
Niliandika uzi juzi kuhusu matapeli wa siasa wazidi kuichimbia kaburi Chadema bahati mbaya Mods wakaiunganisha. Sasa angalie huyu tapeli anavyorusha ngumi hewani.
 
Hilo jimbo ni muhimu sana, maana David Cameron amesisitiza huyo kijana wake lazima ashinde. Hivyo hata 2015 ulinzi utaimarishwa hivyohivyo.
 
Niliandika uzi juzi kuhusu matapeli wa siasa wazidi kuichimbia kaburi Chadema bahati mbaya Mods wakaiunganisha. Sasa angalie huyu tapeli anavyorusha ngumi hewani.

Max mellow aliwahi nukuliwa akiongea na televisheni mojawapo za tanzania kuwa kuna ma "spinn doctor"

wewe Ritz ni mmoja wapo
 
Last edited by a moderator:
Ondoeni red brigade kwanza ndio uje ulielie hapa.Serikali haiwezi kuacha wahuni wafanye wanalotaka

Uswaite watu wanaohamasisha mabaliko kuwa ni wahuni. Muhuni ni wewe uliyepewa madaraka ukaamua kuhadaa watu eti nchi ni masikini wakati mliopewa dhamana mna utajii usiolingana na vipato yenu. Hatuwezi kuendelea kukumbatia mambo yale yale ya miaka 47 iliyopita. Mie si CDM, CUF wala CCM lakini kweye ukweli nitasema. CDM wamekuwa ni chachu ya mabadliko kwa taifa hili. Jamii kubwa imekubaliana nao. Kuwaita wahuni ni kuwatukana Watanzania wasikubaliana na uzandiki wenu.
 
Ni wahuni na vibaka wanapaswa kushughulikiwa na vyombo vya ulinzi na usalama
 
Naona siku hizi umekuwa msemaji wa chama, Kwani kuna ubaya gani ulinzi ukiimarishwa mbona CDM wanasema wamechukua vijana 2000 kutoka Arusha kwenda kulinda kura Kalenga au Iringa hakuna vijana?

Oxymoronic comment!
 
Niliandika uzi juzi kuhusu matapeli wa siasa wazidi kuichimbia kaburi Chadema bahati mbaya Mods wakaiunganisha. Sasa angalie huyu tapeli anavyorusha ngumi hewani.

Utakuwa uliandikia maimamu
 
Back
Top Bottom