Ya Adebayor yapo kila familia TZ?

Ya Adebayor yapo kila familia TZ?

Kiafrica zaid, unapoanza safari ya maisha kwa kusaidiwa inaleta 'ulazima' wa wewe kusaidia wengine behind.Jamii itahoji mbona yeye alisaidiwa.yaan utakuwa mkopo mithil ya heslb,shart u pay back.kama maishan hujawahi kusaidiwa unakuwa na ubavu wa kusema 'kwani mim nilisaidiwa na nan?'. Kumbuka msaada siku zote ni ndoano, ukimeza ndo bas tena.
 
The Boss

Sadaka huanzia nyumbani.

Samahani hii post imekuwa ndefu kidogo kwa kuwa nnahisi hapa kuna darsa linalotuhusu sote, katika kutowa amma kwa kusaidia amma kwa furaha tu:

Binafsi hupenda sana kuona walio karibu waki demand kwangu kama vyao. Ni raha ilioje, ukiwa nao wa kudeka kwako ni raha sana na kutoa ukawapa ni raha zaidi kila niwezapo huwa siishi kuwapa na kuwadekeza. Nikiwa sina basi kweli.

Raha ya kutowa si lazima uwe ni msaada tu, huwa nnatowa zawadi za kila aina kwa kukumbuka tu ngoja nimpelekee zawadi fulani, huwa nnafurahi sana nnapoona mtu akiifurahia zawadi, iwe ya pesa taslim au chochote kile cha thamani kubwa au ndogo. Binafsi huthamini sana mtu anaenikumbuka kwa zawadi hata iwe kashata tu.

Binafsi nnahisi ni haki yao ku demand kwangu na binafsi sina haja ya kujuwa watafanya nini na huo msaada. Its their business, mimi kama nimetoa kwa kuambiwa kwa sababu fulani halafu akaenda akafanya mengine si kosa langu wala lake ni priorities tu. Na wala huwa siulizi kafanya nini wala sina muda huo, hiyo itakuwa masimango, sitarajii kufanya hivyo hata siku moja na wala simuwekei kinyongo, ili iweje? kwani inawezekana kabisa alidanganya kwa sababu zake tu na alihisi akikwambia kuwa nnahitaji kwa ajili hii utamkatalia, ni upunguani wake si wangu, kwanini nimhukumu kwa upunguani wake tu?

Nikitowa natowa tu, singoji shukurani wala sitaki kujuwa niliyempa kafanyia nini, nimempa na nikimpa mtu yeyote, wa karibu au wa mbali huwa sitazami tena kafanya nini, na starehe yake na furaha yake huwa ni furaha kwangu pia.

At the same time, kama nimemtuma nifanyie hiki akafanya kingine, hapo huwa nnauliza.

Hiyo ni mimi binafsi sijuwi wengine.

Nnawaasa vijana, msiwe kama Adebayor anatowa halafu anataka kujuwa wanafanyia alichotowa, si vyema hata kidogo, unless awe kawatuma nifanyieni hiki hawakufanya.

Mfano, analalamika, nilimpa fulani nauli akazike hakwenda, sasa hakwenda unalalamika nini? si ujinga huo? hakwenda ndiyo hakwenda wala usimuulize kwanini hakwenda.

Mamake na nduguze ku demand nyumba na mshahara wa kila mwezi kutoka kwake ni haki yao kabisa, na kama anauwezo angefanya tu bila kulalamika na kama hataki pia angesema bila kulalamika ni haki yake.

Anautangazia ulimwengu ili iweje? wamuone ni mwema sana? au wawaone waliokaribu yake ni wabaya? hata sijaelewa mantiki yake, lakini inaonesha "psychologically" inamtesa na anatafuta relief.

Binafsi nnawajuwa watu fulani (tena si mmoja wala wawili) Tanzania hiihii, wamewapa nyumba ndugu zao na wanawapa mshahara kila mwezi, bila kuwafanyia kazi yoyote, na huwatazama kwa kila shida zao na life goes on, raha mustarehe.

Faida gani ya kuwa na mali na fedha kama nduguzo na walio karibu yako hawawezi kudeka na kujifaraguwa nazo? Siioni.
FaizaFoxy

kusaidia ndugu unaongeza thawabu katika maisha yako ya kila siku pale unaposaidia kwa faida na sio hasara,

swala la Addebayor kulalama inawezekana ndugu wamelalama hawapati msaada kutoka kwake, je kama umeshirikiana na nduguzo mali uliyopewa na Mungu wao hawataki kuona kama unashiriki nao wana demand zaidi na hawajishughulishi kutafuta za kwao unatakiwa kuendelea kuwapa kwa vile tu ni ndugu?

hakuna furaha kama kuwa karibu na ndugu ukamgawia ulichonacho naye akaendeleza zaidi hilo ndio lengo la yeyote anayetoa mali zake kwa mwingine......mfundishe mtu kuvua samaki na sio kumpa samaki mara kwa mara

usipokuwepo wataishi vipi?
 
Last edited by a moderator:
Kitanzania????
Ukiwa na chenji kidogo umeumia...utasaidia hadi majirani wa kijijini
 
Hahahah my dea The Boss acha hizo aisee

Nimekabidhiwa mtoto toka ana mwezi mie ndio mlezi.....

Hivyo na uzee wangu maziwa, pampez, nguo nk ni juu yangu (ila katoto kanazuri, sijui kwa kuwa napenda vichanga)

Hapa najiandaa miaka 2 baadae aanze shule..


Na wengine anakuhesabia watoto wako kabisa...
eti we una mtoto mmoja mie nna wanne lazima nisaidie..
utafikiri ulimtuma wewe kuzaa hao wanne......
 
Last edited by a moderator:
Hahahah my dea The Boss acha hizo aisee

Nimekabidhiwa mtoto toka ana mwezi mie ndio mlezi.....

Hivyo na uzee wangu maziwa, pampez, nguo nk ni juu yangu (ila katoto kanazuri, sijui kwa kuwa napenda vichanga)

Hapa najiandaa miaka 2 baadae aanze shule..

Halafu kakifika umri kama wako (wakati huo umezeeka na kaka kazeeka) utaona jinsi kaka anavyokalazimisha kakupige chini kwenye misaada
 
Huyo inaonesha ndugu wamemfanya ATM Dada yangu
 
Kwa upande wangu nnahisi kuwatatulia matatizo yao ni haki yao, hususan kwa walio karibu nawe.

Utaona kuwa nimekwepa neno "msaada" kwani sikubali kuwa wa karibu yako unawapa "msaada", wa karibu yako ni haki yao kwako kuwatatulia shida zao zote, hata iwe mara 70 kwa siku. Waende wapi wakazitatuwe kama wewe una uwezo wa kuzitatuwa? Hata jirani yako, rafiki yako, mwenye shida yeyote wana haki zao kwako, seuse ndugu zako wa damu.

Na usichukulie wakija kwako wakisema "nisaidie" basi nawe ukachukulia huo ni "msaada", la hasha! hilo ni tatizo na ni wajibu wako kulitatuwa kama liko kwenye uwezo wako.

mkuu inavyo onekana adebayo alikuwa anasaidia ndugu zake. sasa kinacho tokea ambacho adebayo ni ile hali kutumia mali na pesa vibaya.

kunasehemu pia amesema alimfungulia mama yake sehemu ya kupika vyakula na atumie picha yake ili kuwavutia mateja. kwangu mimi hapa alifanya kitu kikubwa sana

kwa mfano unamtoto tuchukulie jinsia yoyote ile unampa kiasi kikubwa cha fedha alafu mwisho wasiku unakutana na mwanao anatungua kwenye mastare na hapo haja fanya chochote na ile hela. ukimkuta kwenye hali hiyo bado utakuwa na nia ya kumpa fedha?
 



Mliolelewa na kijiji na msio na kucha miguuni mna shida, poleni, na Bado mpaka msululu uishe mmeshastaafu!

​
 
Na wengine anakuhesabia watoto wako kabisa...
eti we una mtoto mmoja mie nna wanne lazima nisaidie..
utafikiri ulimtuma wewe kuzaa hao wanne......

Washenzi sana! Aina fulani ya ndugu hawafai hata kuwakaribisha katika maisha yako binafsi, unaweza ukapata presha, ni bora mfarakane tu muwe mbalimbali tu, inakuwa nafuu zaidi.
 
Very true . ni shida kweli kitaa wanangu.
 
kila mwana familia ajengewe nyumba na apewe mshahara kila mwezi
hahahaha! hiyo ni kali.

Hii kama ina ukweli, wallah ilipitiliza...Wazungu wanasema..that was asking for too much...
 
Duh hii imenigusa binafsi. Nimesomesha wadogo zangu wa mama tofauti hadi University level. Walikuwa wanaona kama haki yao. Ilikuwa namna ya kumsaidia mzee.

Haikuwa shida na ninashukuru mke wangu alikuwa very supportive. Tatizo sasa waheshimiwa baada ya kupata kazi imekuwa matusi mtindo mmoja wakiongozwa na mama yao. Mke wangu sasa wanamwita shemeji ile heshima ya mama imekufa sasa amekuwa mwanga.

Wanasema tenda wema uende zako, na usingoje shukurani. Ni kweli kabisa lakini at least wangekuwa na moyo washukurani ingetosha.

Yote kwa yote, bado napata faraja kusaidia (kutoa) kuliko kusaidiwa (kupokea). Hakuna faraja kubwa kama Mungu anakuwezesha kumsaidia mtu.

yaani shukuru mkeo kaitwa mwanga, manake bado wewe uko nae na maisha yanaenda.
wenzio wansaidiaga ndg wa mume afu mwishowa siku analetewa zengwe mumewe amuahe na wanasapoti kabisaa kwamba ndg yetu kakosea kukuoa wewe.
ndg jaman ni mzigo usiobebeka hata mimi ni ndg pia
 
The Boss binafsi najua kusaidia ni sehem ya maisha ya kila mtu, na si msaada wa mali tu bali hata wa hali na zawadi pia. sipendi kutoa misaada ya masharti, wala sipendi kukumbuka nilimsaidia nini mtu as nikitoa nimetoa na ikitokea umeniboa sina haja ya kusema nilimtendea huyu hivi leo kanilipa hivi noo

silazimish kusaidiwa na hata kama sina nitaomba ukinipa poa usiponipa bado nitaish tu so sio ishu sana kwangu.

haya ya adebayor kwangu mie naona tumetafsiri vby ama hatujaelewa ila ukweli ni kwamba mama mzazi anapaswa kulipwa fadhila as well as baba, na fadhila hizi wengine ndio tunazitafsiri kama msaada lkn huu sio msaada kabisa hii ni haki yao.

sawa hukuwalazimisha kukuzaa lkn pia wali dare kukuzaaa na kukutunza if you have why ant you make them happy? onyesha kushukuru kwa kile walichokufanyia na sio vzr kusubiri walalamike.

itaeleweka kama huna ila kama unacho jaman toa kwa wazazi.

lijapo swla la ndg hapa mie huwa siangalii yaani nafunga macho natoa basi, ingawa ni mhanga wa bitter returns adi muda mwingine najikuta nahitaj kujipa self counseling ili nisahau maisha yaende mbele....

ninayo a very bitter experience ya kwenye msaada nilio wah kuutoa kwa ndg na mpaka leo ni kidonda ambachop sijakipatia tiba....................ninaamin with time nita heal.
 
Last edited by a moderator:
Watu wengi ukiwaambia hasa sisi watanzania ukiwaambia kuwa hata ukizaliwa baba mmoja mama mmoja na Bill Gates huna 'haki' ya kulazimisha akusaidie, hatuelewi kabisa. Nimeona uzi wa Adebayor watu wengi wengine wanapiga hadi hesabu za kipato cha Adebayor na kuona 'ana ulazima' wa kusaidia ndugu zake nimeshangaa sana.

Ndio maana tuna ndugu ukiwaambia 'sina hela' inakua ugomvi kumbe washapeleleza hadi kujua mshahara wako au kipato cha biashara zako na kuanzia siku hiyo 'mahesabu ya maisha yao yote' yanaanzia na wewe huku huna hata taarifa kuwa kuna watu washajipa 'haki za kipato' chako simply sababu ni 'ndugu zako'.

Hapa ningependa nieleweke watu kusaidiana hasa ndugu ni kitu kizuri saana binaadamu jinsi tulivyo kutegemeana na kuombana misaada ni kitu hakikwepeki ninachokipinga hapa ni ile hali ya mtu kuona 'ana haki na ni lazima umsaidie' na usipomsaidia huyu mtu ananuna au wengine mnakua maadui na kukutangaza vibaya kama ndugu zake Adebayor.

Mbaya zaidi weengi wanaosaidiwa huwa hawana uchungu wa pesa na wengi hutumia kwa starehe huku wakitegemea zikiisha watasaidiwa tena haya mambo kila familia yapo TZ ni bora sasa tuanze wote kukumbushana kuwa hata mtu awe pacha wako kwa kuzaliwa kukusaidia ni hiari yake na asipokusaidia huna haki ya kumchukia na kumuona mtu mbaya.

'Kipato cha mtu ni haki yake peke yake' wengine ikitokea tumesaidiwa sawa isipotokea pia ni sawa 'yule ambae wote tuna haki ya kumuomba na kumlilia na kujiuliza why hatusaidii ni MUNGU peke yake'.

The Boss, hii mada yako imenigusa na kana kwamba umeyaandika maisha yangu yote…Hii stori imenitokea na inanitokea…
Familia yangu ni ya kimaskini lakini nilifanikiwa kujipinda huko Ulaya na kupata vijisenti vya kuwatoa ndugu zangu ktk umaskini…..sasa msaada woote ambao nilikuwa nawapelekea wao misaada yote ilikuwa inaelekezwa ktk matumizi ya kistarehe na kuandika majina na kila mtu alikuwa anaijua familia yangu kwa matumizi…wadogo zangu wakaoa kisiri japo mwenyewe nilikuwa sijaoaa nikitaka kuwatoa kwanza ndugu zangu…. na maeneo na mashamba ambayo waliniambia wameshaninunulia siku yakuta na mbaya zaidi siku sevu wakati nikiwa huko majuu…Baada ya kurudi si walinikimbia na sikupata hata wa kunisaidia na haohao wakaja kunisimanga kuwa nimerudi mtupu!!!!Ilichukua mwaka mmoja na kitu mpaka nilipoanza tena kusimama tena katika my feet…!!!na rafiki zangu wali nisaidia na nashukuru Mungu kwa kipindi hicho kilinifanya nifikire ki undani na kugundua kuwa
1.Huwezi ukapata dhambi kama huja msaidia ndugu yako…sababu mimi sio niliowaleta hapa duniani na kama kuwasaidia nimeshawasaidia na wao hawajanisaidia
2.Mbele ya Mungu wote ni watoto wake ndugu au sio ndugu na wote ni sawa, hivyo basi kumsaidia mtu ambae anahitaji na hatapanyi unachomsaidia nafikiri Mungu nae anafurahia badala ya kumpa NDUGU msaada ambae anakwenda kujitanua ktk baa..
3.Jenga familia yako kwanza…hakikisha watoto wako ambao umewaleta hapa duniani wanapata malezi mazuri, shule nzuri nk…sababu wewe umewaleta hapa duniani na ni LAZIMA uwasaidie mpaka watakapo jitegemea..na huo ndio urithi mzuri

Sasa ndugu zangu wakaanza kuniletea tena risala za maombi ya shida zao…na mimi naenda kwa stori kuwa "sina hela" na hicho kinawakera sana na nashangaa kwa nini wameshasahau misaada niliokuwa nawasaidia??
 
Hahahah my dea The Boss acha hizo aisee

Nimekabidhiwa mtoto toka ana mwezi mie ndio mlezi.....

Hivyo na uzee wangu maziwa, pampez, nguo nk ni juu yangu (ila katoto kanazuri, sijui kwa kuwa napenda vichanga)

Hapa najiandaa miaka 2 baadae aanze shule..


Kusaidia ni jambo zuri sana hasa kama inatoka moyoni

wataalam wanasema sometimes 'tunajisaidi sisi tunaposaidia wengine'
mimi ninachopinga mtu 'kulazimisha kusaidiwa' hasa mazingira yanapokuwa hayaruhusu
 
Back
Top Bottom