Ya Adebayor yapo kila familia TZ?

Ya Adebayor yapo kila familia TZ?

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,320
Reaction score
117,669
Watu wengi ukiwaambia hasa sisi watanzania ukiwaambia kuwa hata ukizaliwa baba mmoja mama mmoja na Bill Gates huna 'haki' ya kulazimisha akusaidie, hatuelewi kabisa. Nimeona uzi wa Adebayor watu wengi wengine wanapiga hadi hesabu za kipato cha Adebayor na kuona 'ana ulazima' wa kusaidia ndugu zake nimeshangaa sana.

Ndio maana tuna ndugu ukiwaambia 'sina hela' inakua ugomvi kumbe washapeleleza hadi kujua mshahara wako au kipato cha biashara zako na kuanzia siku hiyo 'mahesabu ya maisha yao yote' yanaanzia na wewe huku huna hata taarifa kuwa kuna watu washajipa 'haki za kipato' chako simply sababu ni 'ndugu zako'.

Hapa ningependa nieleweke watu kusaidiana hasa ndugu ni kitu kizuri saana binaadamu jinsi tulivyo kutegemeana na kuombana misaada ni kitu hakikwepeki ninachokipinga hapa ni ile hali ya mtu kuona 'ana haki na ni lazima umsaidie' na usipomsaidia huyu mtu ananuna au wengine mnakua maadui na kukutangaza vibaya kama ndugu zake Adebayor.

Mbaya zaidi weengi wanaosaidiwa huwa hawana uchungu wa pesa na wengi hutumia kwa starehe huku wakitegemea zikiisha watasaidiwa tena haya mambo kila familia yapo TZ ni bora sasa tuanze wote kukumbushana kuwa hata mtu awe pacha wako kwa kuzaliwa kukusaidia ni hiari yake na asipokusaidia huna haki ya kumchukia na kumuona mtu mbaya.

'Kipato cha mtu ni haki yake peke yake' wengine ikitokea tumesaidiwa sawa isipotokea pia ni sawa 'yule ambae wote tuna haki ya kumuomba na kumlilia na kujiuliza why hatusaidii ni MUNGU peke yake'.
 
Hili ni tatizo sana kwenye jamii zetu za kiafrika; Unakuta hata kwenye vikao vya harusi ukitoa pledge labda alf hamsini watu wanaanza kusema aah haiwezekani kwanza wewe ni director wa idara fulani , kwanza juzi tu umetoka London afu nyumbani kwako tu full AC na walinzi wawili; Jamani kipato chango na maisha yangu yasilete ulazima kwenye kutoa michango au kusaidiana.

Niliona pia mama mmoja akigawa watoto wa binti yake huko kijijini kwa wanae walioko mjini na yule asiye na mtoto ndio anapewa adhabu ya kuchukua watoto wawili--bila hata kujua mipango yake pengine hajataka kuzaa sasa ili asave apate watoto baadae ila mama kakomaa wewe bwana huna mtoto sasa chukua wawili maana huna matumizi.

Juzi kwenye redio moja mchana kuna mada inajadiliwa eti inakuwaje ndugu una hela na uwezo halafu ndugu zako wanashida -- to me niliona ni mada isiyo na mashiko. Kufanikiwa kwa mtu mmoja sio factor pekee ya kufanya ukoo wote ufanikiwe , je utayari wao ukoje?
 
Halafu unamtazamaje mtu kwa nje na kusema 'ana hela'?
what if nina mikopo bank inayonipeleka mbio kiasi kwamba kila kitu ni bajeti kali?
au what if kazi ninayofanya inahitaji nipate mda wa kukaa peke yangu au with few people ili nipumzishe kichwa?
halafu unamletea mtu watu wengine tele kisa tu kwa nje unamuona ana pesa
 
Ndugu ni watu wa kwanza ambao Mungu amempa mtu hapa duniani, sasa kama hao pia hutawajali , binadamu ambao unashare nao damu na dna, sidhani kama una faida ya kuwa hapa duniani, NI LAZIMA kusaidia ndugu hilo halina ubishi, wala mjadala.
 
Na wengine anakuhesabia watoto wako kabisa...
eti we una mtoto mmoja mie nna wanne lazima nisaidie..
utafikiri ulimtuma wewe kuzaa hao wanne......

Duh hii imenigusa binafsi. Nimesomesha wadogo zangu wa mama tofauti hadi University level. Walikuwa wanaona kama haki yao. Ilikuwa namna ya kumsaidia mzee.

Haikuwa shida na ninashukuru mke wangu alikuwa very supportive. Tatizo sasa waheshimiwa baada ya kupata kazi imekuwa matusi mtindo mmoja wakiongozwa na mama yao. Mke wangu sasa wanamwita shemeji ile heshima ya mama imekufa sasa amekuwa mwanga.

Wanasema tenda wema uende zako, na usingoje shukurani. Ni kweli kabisa lakini at least wangekuwa na moyo washukurani ingetosha.

Yote kwa yote, bado napata faraja kusaidia (kutoa) kuliko kusaidiwa (kupokea). Hakuna faraja kubwa kama Mungu anakuwezesha kumsaidia mtu.
 
Ndugu ni watu wa kwanza ambao Mungu amempa mtu hapa duniani, sasa kama hao pia hutawajali , binadamu ambao unashare nao damu na dna, sidhani kama una faida ya kuwa hapa duniani, NI LAZIMA kusaidia ndugu hilo halina ubishi, wala mjadala.

Mtanzania halisi huyu.wewe unayesaidiwa unasaidia wangapi???!!
 
Ndugu ni watu wa kwanza ambao Mungu amempa mtu hapa duniani, sasa kama hao pia hutawajali , binadamu ambao unashare nao damu na dna, sidhani kama una faida ya kuwa hapa duniani, NI LAZIMA kusaidia ndugu hilo halina ubishi, wala mjadala.

Mkuu hawa hawa ndugu wa sasa hivi ndio wanakuwa maadui wako wakubwa. kuna baadhi ya ndugu hata umjali vipi ataona haitoshi . nikweli familia ya adebayo ilikuwa kwenye hali ya umaskini na kiasi anacho kipata adebayo anapaswa kusaidia ndugu zake. ila sio kila kitu ambacho atatima watakalo kuwa wanasema.

tuchukulie ni wewe unauwezo una ambiwa ili familia migongano yote ishe utujengee nyumba na kutulipa mishahara kwa mwezi .utaweza?
 
Back
Top Bottom