Ya Adebayor yapo kila familia TZ?

Ya Adebayor yapo kila familia TZ?

kuna wengine ni mizigo hata uwasaidie kiasi gani bado wana demand toka kwako kama vile wewe ndio umewaumba ukisoma addebayor aliyoeleza haitaji kutoa tena msaada kwa hao ndugu kabisa kama mbaya wacha ewe mbaya watu unawabeba na mbeleko hadi linachanika
familia nyingi hapa TZ zinapitia matatizo haya sana unampa ndugu wa damu mtaji wa biashara anaonyesha ufahari bar baada ya siku kadhaa anarudi umsaidie tena ukimnyima ndio maneno hayaishi mwisho anaweza panga mchezo mchafu na watu kwa vile hawaelewi kinachoendelea wanakuwa upande mmoja inakera sana
 
Halafu unamtazamaje mtu kwa nje na kusema 'ana hela'?
what if nina mikopo bank inayonipeleka mbio kiasi kwamba kila kitu ni bajeti kali?
au what if kazi ninayofanya inahitaji nipate mda wa kukaa peke yangu au with few people ili nipumzishe kichwa?
halafu unamletea mtu watu wengine tele kisa tu kwa nje unamuona ana pesa

kosa uwe na kausafiri ndio balaa ukisema huna unaambiwa mbona una gari daahh
 
Sasa usipowasaidia ndugu zako hapa duniani,utamsaidia nani tena?au unaona raha gani wewe unatanua mjini na malaya,wkt ndugu zako huko bush wanashindia uji usio na sukari?
 
Mkuu hawa hawa ndugu wa sasa hivi ndio wanakuwa maadui wako wakubwa. kuna baadhi ya ndugu hata umjali vipi ataona haitoshi . nikweli familia ya adebayo ilikuwa kwenye hali ya umaskini na kiasi anacho kipata adebayo anapaswa kusaidia ndugu zake. ila sio kila kitu ambacho atatima watakalo kuwa wanasema.

tuchukulie ni wewe unauwezo una ambiwa ili familia migongano yote ishe utujengee nyumba na kutulipa mishahara kwa mwezi .utaweza?

Mkuu, i normally do that, and i can not stop doing it, huo ndio mzigo mtu uliopewa for the rest of your life, hao ndio watu wako, hapa duniani.....wengine wote wanaweza wakakuacha lakini hao hawana option ya kukukataa au kukuacha, mke, rafiki wa kike, au wa kiume , wanaweza kukuacha lakini ndugu hao ni kwa maisha ya mtu hapa duniani...
 
Ndugu sio watu wa kuwaendekeza kabisa mara mia hata marafiki ambao wanaona na ku-appriciate struggle yako.

Mwanzoni nilikuwa namshangaa sana mzee alipoamua kuwapotezea ndugu zake wa damu mazima. Baada ya kukua na kupata akili nikaelewa ni kwanin aliamua kufanya hivyo.

Kila siku akawa anatuambia komaeni kivyenu mtoke, ndugu sio watu kabisa. Unaweza kumsaidia na bado akakulaumu au akakuona humfanyii haki kabisa.

Kuna ndugu kibao wamedaidiwa kabla hata hatujazaliwa lakini ni mmoja kati na makumi ndo ambae ameonesha appeciation kwa kile ambacho amesaidiwa na anawasaidia ndugu zake. Utakuta una ndugu ana miaka 40 bado anataka msaada.

Mara mia nipoteze ndugu wote na kubaki mimi mke wangu watoto na marafiki kuliko kuendekeza ndugu wasio na kichwa wala miguu.
 
Sasa usipowasaidia ndugu zako hapa duniani,utamsaidia nani tena?au unaona raha gani wewe unatanua mjini na malaya,wkt ndugu zako huko bush wanashindia uji usio na sukari?

Kama nisingetoka na kuwa na maisha mazuri hao ndugu wangeishije?
 
Miaka hiyoooo nikiishi na Wadhungu, akaja Mama na Kitoroli cha Mtoto kuingia kwenye Bus.

Akaomba msaada kwa dada mmoja amsaidie kukinyenyua kuingiza kwenye Bus.

Dada akamjibu kwa lugha ya kihuni kabisa "....ilitakiwe usingonoke....." Bus lote kimya.

Ni ukweli mchungu ila ni ukweli. Msaada ni msaada tu. Nduguyo akikataa kukusaidia ni uamuzi wake.

Kama una moyo wa kusaidia, siku mambo yatabadilika, basi utamsaidia maana wewe una moyo wa kusaidia.

Ila kwa hali na mila za kwetu, wewe saidia bana. Haya ya kutokusaidia tuwaachie wenye sehemu za kutunzi Vikongwe.

Na wengine anakuhesabia watoto wako kabisa...
eti we una mtoto mmoja mie nna wanne lazima nisaidie..
utafikiri ulimtuma wewe kuzaa hao wanne......
 
Ndugu ni watu wa kwanza ambao Mungu amempa mtu hapa duniani, sasa kama hao pia hutawajali , binadamu ambao unashare nao damu na dna, sidhani kama una faida ya kuwa hapa duniani, NI LAZIMA kusaidia ndugu hilo halina ubishi, wala mjadala.
Si lazima kusaidia ndugu, ni hiari na utashi wa mtu na ukisoma stori ya adebayo, kasaidia sana ndugu zake, ingawa ni stori ya upande mmoja, ila si laza awasaidie.
 
Ndugu ni watu wa kwanza ambao Mungu amempa mtu hapa duniani, sasa kama hao pia hutawajali , binadamu ambao unashare nao damu na dna, sidhani kama una faida ya kuwa hapa duniani, NI LAZIMA kusaidia ndugu hilo halina ubishi, wala mjadala.

Sina uhakika kama usemacho unamaanishaa, una ndugu wangapi wewe ukiangalia family tree???? unaweza kuwamudu wote?????? na je ni walemavu?????? kama ni watu na akili zao na nguvu zao aisee, tutaonana wabaya, undugu sio sababu yakunyonyana, mtu akwame aombe support ila sio mtu kila siku apige hodi kwangu nimlele familia ili hali nami nina shida zangu lol. kama pesa ni rahisi kupatikana basi nao wafanye kama mimi wapate wagawe kwa foleni.

"""WATU tunashida zetu tusikilize zako ili iweje???????????'"
 
Roho mbaya tu, wanakufa wanaviacha hapa vinatumika na hata hao amabao hukutaka wakusogelee, kuna watu na roho zao nzuri, kama unavyoona kina bill gates hapa na misaada yao tunayoitanulia na mavx hapa, wangekua na roho kama yako hao leo nchi kama hii ya kimaskini ingeendelea?? roho mbaya hamfikishi mtu popote zaidi ya kuongeza wasiwasi wa laana, ukitoa ni kama kafara hupungukiwi.
 
Asante sana, umenena.
Ndugu ni watu wa kwanza ambao Mungu amempa mtu hapa duniani, sasa kama hao pia hutawajali , binadamu ambao unashare nao damu na dna, sidhani kama una faida ya kuwa hapa duniani, NI LAZIMA kusaidia ndugu hilo halina ubishi, wala mjadala.
 
Ndugu wa Adebayor wanakosea.... kwanza wanaonyesha kua undugu kati yao na Adebayor haupo ndio maana wanademand hela namna hiyo..sasa kama zile blood relations zinaonyesha zimekufa ingekua mimi ndo Adebayor ningeacha kuwasaidia.
Hapo ndipo wangejua umuhimu wa Adebayor. Tatizo wenzetu hawa walivyo na ushirikina hawakawii kumfanyia ubaya.
Ila pia nawaza ndugu anaekusaidia hivi unaanzaje kumtreat vibaya hivo? i thought wangepasa kuwa close nae zaidi.au mnasemaje wadau?
 
Roho mbaya tu, wanakufa wanaviacha hapa vinatumika na hata hao amabao hukutaka wakusogelee, kuna watu na roho zao nzuri, kama unavyoona kina bill gates hapa na misaada yao tunayoitanulia na mavx hapa, wangekua na roho kama yako hao leo nchi kama hii ya kimaskini ingeendelea?? roho mbaya hamfikishi mtu popote zaidi ya kuongeza wasiwasi wa laana, ukitoa ni kama kafara hupungukiwi.

Acha kujishaua nyuma ya keybord wewe, nyumbani kwako unaishi na watoto wa shangazi zako wangapi??????? watoto wa wajomba wangapi????? achilia mbali misaada unayotuma kila mwezi huko kijijini. rahisi kuongea ni ngumu kutenda.
 
hili ndiyo huwa linaniumiza pale mtu anapogeuza msaada kuwa haki
 
The Boss

Sadaka huanzia nyumbani.

Samahani hii post imekuwa ndefu kidogo kwa kuwa nnahisi hapa kuna darsa linalotuhusu sote, katika kutowa amma kwa kusaidia amma kwa furaha tu:

Binafsi hupenda sana kuona walio karibu waki demand kwangu kama vyao. Ni raha ilioje, ukiwa nao wa kudeka kwako ni raha sana na kutoa ukawapa ni raha zaidi kila niwezapo huwa siishi kuwapa na kuwadekeza. Nikiwa sina basi kweli.

Raha ya kutowa si lazima uwe ni msaada tu, huwa nnatowa zawadi za kila aina kwa kukumbuka tu ngoja nimpelekee zawadi fulani, huwa nnafurahi sana nnapoona mtu akiifurahia zawadi, iwe ya pesa taslim au chochote kile cha thamani kubwa au ndogo. Binafsi huthamini sana mtu anaenikumbuka kwa zawadi hata iwe kashata tu.

Binafsi nnahisi ni haki yao ku demand kwangu na binafsi sina haja ya kujuwa watafanya nini na huo msaada. Its their business, mimi kama nimetoa kwa kuambiwa kwa sababu fulani halafu akaenda akafanya mengine si kosa langu wala lake ni priorities tu. Na wala huwa siulizi kafanya nini wala sina muda huo, hiyo itakuwa masimango, sitarajii kufanya hivyo hata siku moja na wala simuwekei kinyongo, ili iweje? kwani inawezekana kabisa alidanganya kwa sababu zake tu na alihisi akikwambia kuwa nnahitaji kwa ajili hii utamkatalia, ni upunguani wake si wangu, kwanini nimhukumu kwa upunguani wake tu?

Nikitowa natowa tu, singoji shukurani wala sitaki kujuwa niliyempa kafanyia nini, nimempa na nikimpa mtu yeyote, wa karibu au wa mbali huwa sitazami tena kafanya nini, na starehe yake na furaha yake huwa ni furaha kwangu pia.

At the same time, kama nimemtuma nifanyie hiki akafanya kingine, hapo huwa nnauliza.

Hiyo ni mimi binafsi sijuwi wengine.

Nnawaasa vijana, msiwe kama Adebayor anatowa halafu anataka kujuwa wanafanyia alichotowa, si vyema hata kidogo, unless awe kawatuma nifanyieni hiki hawakufanya.

Mfano, analalamika, nilimpa fulani nauli akazike hakwenda, sasa hakwenda unalalamika nini? si ujinga huo? hakwenda ndiyo hakwenda wala usimuulize kwanini hakwenda.

Mamake na nduguze ku demand nyumba na mshahara wa kila mwezi kutoka kwake ni haki yao kabisa, na kama anauwezo angefanya tu bila kulalamika na kama hataki pia angesema bila kulalamika ni haki yake.

Anautangazia ulimwengu ili iweje? wamuone ni mwema sana? au wawaone waliokaribu yake ni wabaya? hata sijaelewa mantiki yake, lakini inaonesha "psychologically" inamtesa na anatafuta relief.

Binafsi nnawajuwa watu fulani (tena si mmoja wala wawili) Tanzania hiihii, wamewapa nyumba ndugu zao na wanawapa mshahara kila mwezi, bila kuwafanyia kazi yoyote, na huwatazama kwa kila shida zao na life goes on, raha mustarehe.

Faida gani ya kuwa na mali na fedha kama nduguzo na walio karibu yako hawawezi kudeka na kujifaraguwa nazo? Siioni.
 
Last edited by a moderator:
Acha kujishaua nyuma ya keybord wewe, nyumbani kwako unaishi na watoto wa shangazi zako wangapi??????? watoto wa wajomba wangapi????? achilia mbali misaada unayotuma kila mwezi huko kijijini. rahisi kuongea ni ngumu kutenda.
Hatufahamiani kwahiyo hakuna haja ya kubishana, tunaweza kesha hapa mkuu...
 
Back
Top Bottom