Nashukuru sana mimi si mtu wa kutegemea misaada au hisani za wengine.
Na hata niwe na shida gani, ukiondoa labda inayohusu uhai na uzima wangu, mimi huwa ni mgumu sana kuomba msaada na kamwe siwezi kumlaumu mtu ambaye hajanisaidia kwa lolote lile.
I am independent personified.
Na wengine anakuhesabia watoto wako kabisa...
eti we una mtoto mmoja mie nna wanne lazima nisaidie..
utafikiri ulimtuma wewe kuzaa hao wanne......
Inasikitisha sana na kutia hasira. Tabu unapata mwenyewe, ukishachuma mali na kuwa nazo watu wanazipigia hesabu. Mwingine anakuambia kabisa, wewe huwezi kukosa bana ni roho mbaya tu.
Wengine hawachelewi kuwaza unakufa lini ili waje kugawana, haya yanatokea na tunaona sana familia za wenye nazo ambavyo watoto na wake huwa wanapata tabu ikiwa baba atatangulia mbele za haki.
Watu wengi ukiwaambia hasa sisi watanzania ukiwaambia kuwa hata ukizaliwa baba mmoja mama mmoja na Bill Gates huna 'haki' ya kulazimisha akusaidie, hatuelewi kabisa. Nimeona uzi wa Adebayor watu wengi wengine wanapiga hadi hesabu za kipato cha Adebayor na kuona 'ana ulazima' wa kusaidia ndugu zake nimeshangaa sana.
Ndio maana tuna ndugu ukiwaambia 'sina hela' inakua ugomvi kumbe washapeleleza hadi kujua mshahara wako au kipato cha biashara zako na kuanzia siku hiyo 'mahesabu ya maisha yao yote' yanaanzia na wewe huku huna hata taarifa kuwa kuna watu washajipa 'haki za kipato' chako simply sababu ni 'ndugu zako'.
Hapa ningependa nieleweke watu kusaidiana hasa ndugu ni kitu kizuri saana binaadamu jinsi tulivyo kutegemeana na kuombana misaada ni kitu hakikwepeki ninachokipinga hapa ni ile hali ya mtu kuona 'ana haki na ni lazima umsaidie' na usipomsaidia huyu mtu ananuna au wengine mnakua maadui na kukutangaza vibaya kama ndugu zake Adebayor.
Mbaya zaidi weengi wanaosaidiwa huwa hawana uchungu wa pesa na wengi hutumia kwa starehe huku wakitegemea zikiisha watasaidiwa tena haya mambo kila familia yapo TZ ni bora sasa tuanze wote kukumbushana kuwa hata mtu awe pacha wako kwa kuzaliwa kukusaidia ni hiari yake na asipokusaidia huna haki ya kumchukia na kumuona mtu mbaya.
'Kipato cha mtu ni haki yake peke yake' wengine ikitokea tumesaidiwa sawa isipotokea pia ni sawa 'yule ambae wote tuna haki ya kumuomba na kumlilia na kujiuliza why hatusaidii ni MUNGU peke yake'.
mungu anakupa ridhiki ili usaidie na wengine, unapotoa unazidi kubarikiwa na unakuwa na vingi zaidi.
kuna watu mpaka maisha yao yamesimama mstari wamesaidiwa na ndugu tena ile ya kidonation kabisaaa, leo hii ndugu wanaohitaji msaada wanaona si jukumu lao kuwasaidia, wakati unasaidiwa ww mbona hukukataa.
Ndugu wa Adebayor wanakosea.... kwanza wanaonyesha kua undugu kati yao na Adebayor haupo ndio maana wanademand hela namna hiyo..sasa kama zile blood relations zinaonyesha zimekufa ingekua mimi ndo Adebayor ningeacha kuwasaidia.
Hapo ndipo wangejua umuhimu wa Adebayor. Tatizo wenzetu hawa walivyo na ushirikina hawakawii kumfanyia ubaya.
Ila pia nawaza ndugu anaekusaidia hivi unaanzaje kumtreat vibaya hivo? i thought wangepasa kuwa close nae zaidi.au mnasemaje wadau?
Shosti tatizo sio kusaidia.....tatizo msaada unapogeuzwa lazima
Na usipokuwa na kitu inapofanywa i ugomvi
Mbaya zaidi unapomsaidia mtu halafu anatapanya na kukutusi juu
ndio hapo msemo wa tenda wema uende zako unapokuwa applicable. wengi tunatarajia tunaowasaidia nao waje watusaidie na mambo yanageuka mtu anajuta msaada alioutoa. habari za uzima wako lakn? hivi karibuni hakuna sikukuu nije kudowea pilau!