Xiaomi 13 pro: Simu bora ya Xiaomi 2022

Xiaomi 13 pro: Simu bora ya Xiaomi 2022

Niko na Note 13pro nimeilaza charge mpaka asubui hafi hivi navyoandika hapa imegoma kuwaka leo wiki sasa. Ukiweka charge inavibrate tu
Kiukweli hiyo Note 13 Pro, sijajua ni simu gani
Ila jaribu njia mojawapo
  • Bonyeza Power button kwa sekunde 10 hadi 30 hivi, halafu tulia kama itakubali kuwaka. Ikishindikana jaribu njia nyingine
  • Au, press hiyo power button kwa muda na usiiachie. Hivyohivyo ukiwa umeihold chomeka chaja na endelea kuhold hivyohivyo hadi iwake. Ikikubali kuwaka irestart
  • Au kama betri yake inatoka basi itoe na uirudishe tena
  • Au iconnect simu yako na kompyuta kwa kutumia waya wa USB, acha ichaji kwa dakika 15. Halafu chomoa waya kutoka kwenye simu (sio kutoka kwenye kompyuta) hakikisha waya wa USB unabaki palepale kwenye kompyuta, we chomoa simu tu waya uache.
Baada ya kuichomoa simu, tulia kwa sekunde kumi na uichomeke tena kwenye chaji. Ichaji tena kwa dakika 30. Baada ya hapo press power button kwa sekunde 5 halafu tap restart. Kama hujaiona restar, endelea kupress na kuhold power button kwa sekunde nyingine 30.
* Ukishindwa njia hiyo jaribu kupress button ya volume down na power button kwa pamoja kwa sekunde 10 hadi 30
Njia zote hapo zikigoma tafuta msaada kwingine, mfano peleka simu kwa fundi au mconsult CHIEF MKWAWA
 
Ni 13 pro.

Nimejaribu njia zote hizo imegoma kabisa Mkuu, mpaka nimefikia uamuzi wa kuifungua nika disconnect betri labda itakubali, imegoma kabisa. Simu hii niliagiza, na ni mwezi wa 12 mwishoni ndio ikafika yaani sijaitumia hata mwezi. Hata pesa sijamaliza kumlipa aliyeileta imeniletea mapicha haya Mkuu. Mimi mwenyewe ni Fundi, wa Software ( Mobile Software ) hardware si sana. Sasa nilikuwa naomba muongozo je hizi zina sensor kwamba iko overcharge inakata ama inaua Display? Kwa sababu nikiichomeka ktk PC inaonekana kisha inatoka, force restart inagoma pia. Nashindwa kusambua mkuu sababu daah hela kibao halaf nimetumia nusu mwezi tu, nimenunua mpya kabisaa
 
Hiyo 13 pro ni Xiaomi au iPhone?
Halafu kama nilivyokuambia hapo mfuate Chief Mkwawa, hata pm. Mambo kama haya yeye ndo anajua shida ni nini anaweza kukusaidia. Hapo ukute simu ni nzima kabisa halafu unaifungia ndani wiki nzima kumbe solution ni simple tu.
So.. tafuta humu JF kuna watu ni maexpert na wengine ni mafundi simu, mimi haya mambo siyajui sana aisee.
Consult experts
 
Mkuu Oppo ni simu nzuri sana lakini kwa bajeti hiyo hapa Bongo sio simu nzuri. Labda uagize nje au ununue used. Ngoja nikupe mifano kulingana na bei za hapa Tanzania (za madukani)
  • Kwa TSh 340,000/= unapata Oppo A16K ya (3GB RAM 32GB ROM) ambayo kwa hii bei umepigwa sana. Simu hii ina chipset ya MediaTek Helio G35, hii chipset ni mbaya na kama una matumizi mazito haitakufaa, pia chipset hii inatumiwa kwenye simu nyingi za Infinix au hata Redmi 9C. Hivyo usitegemee perfomance nzuri. Ukiachana na hapo pia storage yake ni eMMC na bado charger yake ni microUSB. Kamera haina maajabu ni ya kawaida sana. Ukinunua hii simu utakuwa disappointed
  • Lakini kwa TSh 340,000/= hiyohiyo hapa Bongo unaweza kupata Oppo A17K ya (3GB RAM 64GB ROM) hii simu siyo nzuri nayo, inatumia chipset ileile ya Helio G35 ambayo ni weak, kamera yake ya nyuma ni 8MP na haifai hata kwa matumizi ya picha za kila siku, RAM ipo moja tu, ya 3GB RAM hakuna option nyingine. Sasa kwa chipset weak kama hii 3GB RAM ni ndogo sana tena kwa bei hiyo umepigwa. Kikubwa tu ni kwamba display yake inafikia brightness ya 600nits ila hii simu haifai kabisa, tena inatumia microUSB charger, binafsi sikushauri ununue hii.
  • Kwa TSh 440,000/= unapata Oppo A55 5G, yenye (4GB RAM 128GB) kama lilivyo jina lake hii simu inakuja na 5G.Inatumia chipset nzuri ya MediaTek Dimensity 700 na storage ni 128GB. Charger yake ni USB Type C na kamera yake ni ya kawaida sana kwa bei hii. Kwa kuwa bei imefika laki nne na kitu bora ununue Redmi Note 10 (plain) ambayo inarekodi 4K videos hii Oppo inarekodi mwisho 1080p, Redmi Note 10 ina SoC nzuri ya Snapdragon 678, ina kamera kali, display yake ni AMOLED hii Oppo ina LCD, Redmi Note 10 display yake inafikia brightness ya 1100nits, hii OPPO inaishia 480nits, Display ya hiyo Oppo ina resolution ya 720p wakati Redmi ina 1080p, kikubwa tu Oppo ni 5G.
Nisikuchoshe, najua unataka kuihama Xiaomi, ila ni ukweli usiopingika kwa sasa Bongo hii, kwa shilingi 350,000/= hakuna simu nzuri kama Xiaomi Redmi 10C, kwa sababu zifuatazo
  • Redmi 10C inatumia chipset ya Qualcomm Snapdragon 680, ambayo hii ni gaming chipset kabisa. Ni strong kwa hiyo kama una matumizi mazito itakufaa hii. Simu nyingine za bei hii zina MediaTek Helio G25, G35, P22, P35, A25 na kadhalika, hizi zote ni mbaya hazifai kutumika kabisa, unaweza kuexperience laggs, apps kufunguka taratibu n.k. Redmi 10C inafungua applications kwa haraka zaidi kuliko hata simu nyingi tu za laki nne na nusu hadi laki 5.
  • Redmi 10C inatumia storage ya UFS na sio eMMC kama ilivyo kwa simu nyingi za laki tatu
  • Kwa 350,000/= unapata Redmi 10C ya (4GB RAM 64GB ROM) na 380,000/= unapata yenye (4GB RAM 128GB ROM) Tanzania hapahapa.
  • Redmi 10C inatumia charger ya USB Type C 2.0 wakati simu nyingi za laki 3 zinatumia microUSB charger
  • Redmi 10C inasupport GCAM, simu nyingi za laki 3 hazisupport hii kitu. GCAM itakusaidia kuongeza ubora wa picha utakazopiga
  • Redmi 10C ina kamera nzuri kuliko wapinzani wake wa bei hiyohiyo
  • Redmi 10C ina AnTuTu score kubwa, zaidi ya 240,000, simu nyingi za laki tatu score zake zinarange 140,000
  • Redmi 10C ina display kubwa 6.71inch, simu nyingi za laki 3 zina 6.5inches
Ila ukinunua Redmi 10C usithubutu ku-update software, usije ukaja kutukana Xiaomi zote humu ndani
Maamuzi ni yako tu. Labda umuulize CHIEF MKWAWA akushauri simu kali ya Oppo kwa bei hiyo, na wapi unaweza kupata kwa bei hiyo.
Oppo ni tamu sana kama ukitumia hizi Reno Series kama aliyopost huyo jamaa The Monk ila bei yake iko juu kidogo, zenyewe ni midrange. Pia Oppo tamu zaidi ni Oppo Find X-series ila bei zimechangamka sana
Nilitaka kuchukua oppo a17 kwa 370k
 
Nilitaka kuchukua oppo a17 kwa 370k
Hiyo bei ni ya wapi?
Kama shida yako ni Oppo, hiyo chukua tu kwa bei hiyo, nimeangalia hapa kuna mambo kadhaa yamenivutia kulingana na hiyo bei ( Oppo A17 sio Oppo A17K)
  • Kwanza, ina option moja tu 4GB RAM na 64GB ROM haitamchanganya mnunuaji
  • Halafu kamera yake ni nzuri kuliko simu nyingi za bei hiyo
  • Brightness ya display yake inafikia 480nits
  • Ina fingerprint pembeni (sio nyuma)
  • Muonekano wake kiujumla unavutia
  • Inatumia Android 12
Japokuwa ichukue kama perfomance kwako sio kipaumbele, inatumia chipset ya MediaTek Helio G35, hii ni weak chipset ila kuna option ya kuexpand RAM mpaka 4GB zaidi. Kwa hiyo unaweza kuexpand RAM kutoka 4GB hadi 8GB na kuexpand ni rahisi tu. Ukiexpand RAM haitoweza kuboost perfomance sanasana itasaidia multitasking
Ila amezingua kutumia storage ya eMMC 5.1, bora angetumia UFS 2.2. Ila pia anatumia microUSB charger ila ingependeza kama angetumia USB Type C 2.0.
Hakuna simu iliyokamilika kila kona kama unataka Oppo, chukua tu hiyohiyo ( kwa 370,000Tsh)
 
Mimi nina Poco F3 ina mwaka na miezi speed ile ile ubora wa battery bado uko vizuri sitegemei wala sitamani kuhama Xiaomi.

2018 nilianza na Redmi Note 5 Pro ikafata Note 6 Pro Note 7 nikahamia Poco,mwaka huu mambo yamekuwa mengi ningeshabadilisha ila mwakani nitaangalia namna.
Same here, Nilianza na Redmi Note 5 pro yangu naipenda sana, nikaenda redmi Note 8 kisha note 8 pro, Kisha Note 10 pro 5G kisha nikashuka ghafla mpaka Redmi 9A hiki chuma kinakaa na chaji siku mbili plus na data on... Baadae Nikarudi kwenye Redmi note 5 pro yangu ya awali niliyonunua 2018 ikarudi mikononi mwangu what a Joke! Ndio niko nayo mpaka sasa ..... Imepita Mikononi mwa watumiaji wawili na sasa imenirudia ni bado chuma kinapiga kazi haswa... Battery tu ndio limekua dhaifu ila nina mpango wa kulibadilisha... Ni gb 4/64 hivyo inakidhi kabisa mahitaji yangu ya storage.

Kuna wale wanataka simu GB 256 sijui wanajaza mashetani.?

Sent from my Redmi Note 5 using JamiiForums mobile app
 
Sasa hiyo Note 10 Pro ilipotelea wapi
 
Hiyo bei ni ya wapi?
Kama shida yako ni Oppo, hiyo chukua tu kwa bei hiyo, nimeangalia hapa kuna mambo kadhaa yamenivutia kulingana na hiyo bei ( Oppo A17 sio Oppo A17K)
  • Kwanza, ina option moja tu 4GB RAM na 64GB ROM haitamchanganya mnunuaji
  • Halafu kamera yake ni nzuri kuliko simu nyingi za bei hiyo
  • Brightness ya display yake inafikia 480nits
  • Ina fingerprint pembeni (sio nyuma)
  • Muonekano wake kiujumla unavutia
  • Inatumia Android 12
Japokuwa ichukue kama perfomance kwako sio kipaumbele, inatumia chipset ya MediaTek Helio G35, hii ni weak chipset ila kuna option ya kuexpand RAM mpaka 4GB zaidi. Kwa hiyo unaweza kuexpand RAM kutoka 4GB hadi 8GB na kuexpand ni rahisi tu. Ukiexpand RAM haitoweza kuboost perfomance sanasana itasaidia multitasking
Ila amezingua kutumia storage ya eMMC 5.1, bora angetumia UFS 2.2. Ila pia anatumia microUSB charger ila ingependeza kama angetumia USB Type C 2.0.
Hakuna simu iliyokamilika kila kona kama unataka Oppo, chukua tu hiyohiyo ( kwa 370,000Tsh)
Naona kioo chake kizuri kushinda washindani wake wa bei hiyo
 
Nina bajeti ya laki tano na nusu simu gani nzuri ya redmi naweza kupata?
 
Nina bajeti ya laki tano na nusu simu gani nzuri ya redmi naweza kupata?
Laki 5 na nusu unapata "Xiaomi Redmi Note 10 Pro" yenye 4GB RAM na 128GB ROM. Angalia specifications zake hapa Xiaomi Redmi Note 10 Pro: specs, benchmarks, and user reviews

Au ingia Mlimani City, nenda kwenye office za Tigo shop. Nunua "Xiaomi Redmi Note 11" yenye 6GB RAM na 128GB ROM. Bei yake ni exactly 550,000/= fixed ukinunua Tigoshop. Angalia specifications za Redmi Note 11 hapa Xiaomi Redmi Note 11: specs, benchmarks, and user reviews
 
Mkuu nisaidie Mwanza nipate Redmi 11 lite.
 
Mkuu nisaidie Mwanza nipate Redmi 11 lite.
Redmi 11 Lite siijui. Lakini Redmi Note 11 ndio naijua. Kwa kuwa sipo Mwanza siwezi kujua ni wapi utazipata.
Jaribu kwenda Tigoshop ya Mwanza. Wanauza simu bei sawa mikoa yote. Xiaomi Redmi Note 11 ya 4GB RAM 128GB ni 530,000/= na Xiaomi Mi 11 Lite ya 8GB RAM na 128GB ROM inauzwa kwa TSh 850,000/=
 
Simu zao nzuri, tatizo ni hiyo MIUI ina mauzi ya hapa na pale kama ku crush, kuwa slow nk. Mi nawahama sasa, tukutane oppo
Mimi ni mtumiaji wa MI 11 5G. Mwaka pili huu sijawahi pata hizo changamoto unazosema. Kikubwa kinachokera ni matangazo. Software zao nyingi zinakuwa na matangazo ya biashara. Mchina bwana.

Otherwise, ni simu bomba sana kwa hili toleo nililonalo.
 
Mimi nina Poco F3 ina mwaka na miezi speed ile ile ubora wa battery bado uko vizuri sitegemei wala sitamani kuhama Xiaomi.

2018 nilianza na Redmi Note 5 Pro ikafata Note 6 Pro Note 7 nikahamia Poco,mwaka huu mambo yamekuwa mengi ningeshabadilisha ila mwakani nitaangalia namna.
Nina MI 11 5G mwaka pili huu sasa. Sijawahi jutia.
 
Hii, December Xiaomi wameachilia chombo kipya tena, Xiaomi 13 pro. Simu hii inapatikana kwa shilingi za kitanzania kama 2,821,000/= hivi kule AliExpress
Hii ni picha ya Xiaomi 13 pro
View attachment 2446886
Simu hii inakuja na 8/12GB RAM na storage kuanzia 128GB hadi 512 GB, yaani matoleo ya aina tatu: (8GB+128GB), (12GB+256GB) na (12GB+512GB)
View attachment 2446896
Rangi zake ndo hizo hapo juu. Display yake ina 6.73inches na refresh rate ya 120Hz type yake ni LTPO, OLED screen. Display yake ni Corning Gorilla Glass Victus na Resolution yake inafikia 1440×3200p huku aspect ratio yake ikiwa 20:9 na ~522ppi density
View attachment 2446907
8GB/12GB RAM ya Xiaomi 13 pro iko supported na chipset ya Qualcomm Snapdragon 8 Gen 2, ambayo ndio Snapdragon yenye nguvu zaidi kwa sasa.
View attachment 2446910
Xiaomi 13 pro ni IP68 dust/water resistance. Kwa maji yenye kina cha mita 1.5, simu hii inaweza kukaa chini ya hayo maji mpaka dakika zipatazo 30.
View attachment 2446917
Kamera zipo tatu kwa nyuma na kweli zinafanya kazi nzuri, ukipiga picha bustani, unaweza sema ni Eden. LEICA hanaga kazi mbovu. Specification za kamera ya nyuma ni:
50.3MP (f/1.9) 23mm (wide)
50MP (f/2.0) 75mm (telephoto)
50MP (f/2.2) 14mm, 115° (ultra wide), AF.
Features za kamera ya nyuma ni: LEICA lens, Dual LED dual-tone flash, HDR na panorama. Ina uwezo wa kurekodi 8K videos, 4K na 1080p
8K@24fps (HDR)
4K@24/30/60fps (HDR 10+, 10bit Dolby Vision HDR, 10-bit LOG)
1080p@30/120/240/960fps
1080p@1920fps, gyro EIS
View attachment 2446936
Kamera ya mbele yaani Selfie Camera ni moja tu "Single 32MP (wide)" na features zake ni HDR na Panorama na inarekodi video ambazo ziko limited kwenye 1080p@30fps. Inatoa video nzuri sana, ukiwa nayo Tiktok itakukoma
View attachment 2446957
Xiaomi 13 pro inatumia Stereo speakers, yaani wapenzi wa muziki hapa ndio mahala salama
COMMS
WLAN - Wi-Fi 802.11 a/b/g/n/ac/6e, dual band, WiFi Direct
Bluetooth: 5.3, A2DP, LE
Positioning: GPS (L1+L5), GLONASS(GI), BDS (B1l+B1c+B2a), GALILEO (E1+E5a), QZSS(L1+L5), NavIC (L5)
View attachment 2446988
Xiaomi 13 pro ina accelerometer, proximity, gyro, compass barometer na colour spectrum ambazo ni features zake bila kusahau FINGERPRINT SENSOR iko ndani ya display
Xiaomi 13 pro inatumia Android 13 na imebase kwenye software ya MIUI 14 ambayo imedesigniwa na Xiaomi wenyewe. Maoni mengi ya wa watu juu ya MIUI 14 ni kwamba ni software nzuri, ipo faster na ni kweli imeimprove ukilinganisha na MIUI 13, ambalo ndio toleo lililopita. MIUI 14 ni software kali sana, binafsi nimevutiwa nayo
View attachment 2447000View attachment 2447002
Bila kusahau na battery yake, Non-Removable Li Po 4820mAh. View attachment 2447004
Inakuja na wired charger 120W inayochaji simu hiyo kutoka 0% hadi 100% kwa dakika 19 tu. Pia inaoffer 50W wireless charger inayojaza simu hiyo kwa dakika 36 tu, pia ina 10W reverse wireless charger.
View attachment 2447005
Huko China Xiaomi 13 na 13pro zinaendelea kununuliwa na watu wanapata kuenjoy ulimwengu wa MiView attachment 2447007
Xiaomi 13 pro inanifanya niipende Xiaomi kuliko Apple. Hizi simu ni EXTRA FIRE
View attachment 2447009
Angalia specs za Xiaomi 13 pro hapo chini
View attachment 2447022
Sasahivi unaweza kununua simu zao kutoka official Xiaomi store, China online. Bei zake ni nzuri kama hizo hapo chini
"Xiaomi MIX 4" kwa TSh 1,408,809/=View attachment 2447012
"Xiaomi 12S Ultra" kwa TSh 2,012,728/=View attachment 2447017
"Xiaomi Mi MIX Alpha" kwa TSh 6,709,876/=View attachment 2447018
"Xiaomi 13" kwa TSh 1,341,706/=View attachment 2447021
"Xiaomi 11 Ultra" kwa Tsh 1,341,706/=View attachment 2447024
"Xiaomi Redmi K50 Gaming Edition" kwa TSh 804,889/=View attachment 2447025
Pia usisahau, kama unatafuta simu nzuri chini ya laki nne, Xiaomi Redmi Note 10 5G kuna mahali inauzwa around TSh 333,000/= kule AliExpress. Long live Xiaomi.
View attachment 2447029
China feels proud of Xiaomi
Bado nina imani na Xiaomi. Hata hivyo, ili kuepuka stress ninanunulia soko la nje,Ulaya. Mwaka wa pili huu MI 11 5G utasema inetoka dukani leo. Chuma ya ukweli 👏👌
 
MI wanazingua sana , Camera sjui zina maruhan , sometime picha zinatoka clear , sometime zinakuwa blurred, mpak urestart simu ndo inakaa mkao , too much update command , alaf app nyingi zinakuwa na matangazo , kwenye music player ina display sio nyimbo zote , zingine mpak ukazitaftie kwenye file manager ,

Sometime ukiweka laini mbili za mtandao mmoja , inakuwa inachelewa kurespond mpak Kero, ukienda kwenye recently call ni empty mpak baada ya mda ina display .... !! Soon nahamia iPhone series

Unatumia Oppo Gani Mkuu?
 
Back
Top Bottom