Hiyo bei ni ya wapi?
Kama shida yako ni Oppo, hiyo chukua tu kwa bei hiyo, nimeangalia hapa kuna mambo kadhaa yamenivutia kulingana na hiyo bei ( Oppo A17 sio Oppo A17K)
- Kwanza, ina option moja tu 4GB RAM na 64GB ROM haitamchanganya mnunuaji
- Halafu kamera yake ni nzuri kuliko simu nyingi za bei hiyo
- Brightness ya display yake inafikia 480nits
- Ina fingerprint pembeni (sio nyuma)
- Muonekano wake kiujumla unavutia
- Inatumia Android 12
Japokuwa ichukue kama perfomance kwako sio kipaumbele, inatumia chipset ya MediaTek Helio G35, hii ni weak chipset ila kuna option ya kuexpand RAM mpaka 4GB zaidi. Kwa hiyo unaweza kuexpand RAM kutoka 4GB hadi 8GB na kuexpand ni rahisi tu


. Ukiexpand RAM haitoweza kuboost perfomance sanasana itasaidia multitasking
Ila amezingua kutumia storage ya eMMC 5.1, bora angetumia UFS 2.2. Ila pia anatumia microUSB charger ila ingependeza kama angetumia USB Type C 2.0.
Hakuna simu iliyokamilika kila kona


kama unataka Oppo, chukua tu hiyohiyo ( kwa 370,000Tsh)