Ndiyo aina ya akili za wengi zinavyoishia kuwaza.
Dhulumadhuluma tu kwa kwenda mbele. Kudhulumu ni kuhujumu. Na ndiyo maana watu wengi wenye pesa zao, husita kuwezesha watu wenye uhitaji wa kweli.
Fikiria sana unapotaka kutoa ushauri wako kwa mtu, hasa anapokuwa kahitaji ushauri.
Wizi, dhulma, utapeli si njia sahihi za ushauri.
Wewe hata kama ni mwizi, hauwezi kutoa ushauri wa ukibaka kwa mtu aliyetaka ushauri kwako.
Utatoa ushauri kwa kuficha hulka zako na kuweka mbele ulichoombwa kushauri.
Wizi ni hulka za kishetani kwa ajili ya kuharibu na si kujenga ama kuendeleza.
Hivi huyo dada angekuwa dhulmati, angekaa nyuma ya keybord kutafuta ushauri jinsi ya kudhulumu?
Yeye kauliza afanyie kazi ombi la x wake au amrejeshee? Tungejikita kwenye hadidu hizo za rejea pekee na siyo kuvuka nje ya mada na kuanza kushauri "usambo", jambo ambalo mtoa mada hakuliombea ushauri.