Hivi ukiishaachana na mtu kuna umuhimu wa kuwasiliana tena? Mm niko tofauti na mi no sikumbuki hata moja.
Kuachana kupo kwa aina nyingi sn.
Kama utakuwa umejiwekea msimamo huo bila kuubadili kwa njia ya kutafakari, kwamba mtu ukishaachana naye hauwezi hata kumsalimia, basi una tatizo la kisaikolojia lihitajilo ushauri nasaha.
Kibuti kinaweza kuwa ni shamba darasa la kurekebisha dosari za kimahusiano na kuimarisha.
Pia kibuti chaweza kutokana na shinikizo nje ya wapendanao, kwa mfano kuna badhi ya mila kulazimisha ndoa za kikabila nk, wakati shinikizo likifanyika huvuruga kwa muda mahusiano yaliyopo, wakati kiukweli penzi huvunjwa na wapendanao wenyewe.
Je ma x wa "kabila" hii huwa wameachana kiukweli?
Na kunavibuti vingine hutengenezwa na tamaa za kijinga tu. Ambapo mtu akishafika katika mahusiano mapya huanza kuyajutia mahusiano yake ya zamani na kukosa amani katika mahusiano yake mapya.
Mtu aina hii hujitahidi sana kumuangukia x wake kwa gharama zozote.
Na mahusiano hayo yakirejea huwa yana afya sana na ni vigumu tena kutetereka.
Hayo ni mambo ya kibinadamu mtu kuachana na kuweza kurejeana tena, ni mambo ya kawaida.