Wote wanaoponda Uteuzi wa Muhongo, Mwakyembe na Nape, wapo nyuma ya Lowassa na Mengi

Ccm ni ile ile ....oooh. Ni...ile ile hamna mpya...nilikuwa nasubiri baraza la mawaziri kwa hamu...!!!!Sasa nishaona usanii wa JPM....NAPE..MWIGULU...MAKAMBA ...MUHONGO...MWAKIEMBE...Hawa watu si wana kashfa mbalimbali..?????!!!!!!! Ina maana hamna watu wengine????!!!!!!Sasa watu hawa wakifanya wizi tena MAGUFULI ataweza kuwafukuza hawa?????
 
CCM ni ile ile ndio maana wananchi wametuchagua.
 
hizo 2500 ni eneo la ukanda wa bahari kwa ajili ya kujijengea bandari yake kwaiyo ukijumlisha na hizo za eneo la mradi utapata 3200 angalipewa mzalendo watu wa aina yako mngetembea uchi!!! lakini wamakonde na wana ccm walifanya tafrija na kucheza ngoma

Mkuu kuna watu wana uhulka za kuwahudu wa nje ya tanzania na kuona watanzania wanzao kama vile ni wajinga vile. Kwa ujumla nchi haiwezi kujengwa na wageni. Tanzania itajengwa na wa zawa tu na siyo wakuja.
 
Ni kutokana na uteuzi wa Dr. Harrison Mwakyembe na Prof. Sospeter Muhongo kwenye baraza lake la mawaziri.
Sakata la ESCROW liliwaweka karibu sana Mengi wote waliokuwa wakipigana usiku na mchana kuhakikisha Prof. Muhongo anajiuzulu kufuatia sakata hili. Kwa sababu ya Prof. Kuminya mianya ya watu kutaka kuwa madalali wa kuwekeza kwenye gesi, Reginald Mengi akiwa mmoja wao, nguvu nyingi zilitumika kuhakikisha Mzalendo huyu na mtetezi wa Wanyonge anaenguliwa, Pesa ni kila kitu, Prof hakuona sababu ya kushindana na kwa kuzingatia msemo, "MWENYE NGUVU MPISHE" aliamua kukaa pembeni.

Mwakyembe naye hatasahau uchaguzi wa Mwaka huu. Kati ya majimbo ya CCM yalikuwa magumu mwaka huu , basi ni jimbo la Kyela. Nguvu ya pesa ni mbaya sana. Mwakyembe alitumiwa kila aina majeshi kuhakikisha kwake siasa inaishia hapo. Mungu siyo Athumani , Kapenya. Kwa mujibu wa mtonyaji wangu, kati To every action there is an opposite action.
 
Ni kutokana na uteuzi wa Dr. Harrison Mwakyembe na Prof. Sospeter Muhongo kwenye baraza lake la mawaziri.
Sakata la ESCROW liliwaweka karibu sana Mengi wote waliokuwa wakipigana usiku na mchana kuhakikisha Prof. Muhongo anajiuzulu kufuatia sakata hili. Kwa sababu ya Prof. Kuminya mianya ya watu kutaka kuwa madalali wa kuwekeza kwenye gesi, Reginald Mengi akiwa mmoja wao, nguvu nyingi zilitumika kuhakikisha Mzalendo huyu na mtetezi wa Wanyonge anaenguliwa, Pesa ni kila kitu, Prof hakuona sababu ya kushindana na kwa kuzingatia msemo, "MWENYE NGUVU MPISHE" aliamua kukaa pembeni.

Mwakyembe naye hatasahau uchaguzi wa Mwaka huu. Kati ya majimbo ya CCM yalikuwa magumu mwaka huu , basi ni jimbo la Kyela. Nguvu ya pesa ni mbaya sana. Mwakyembe alitumiwa kila aina majeshi kuhakikisha kwake siasa inaishia hapo. Mungu siyo Athumani , Kapenya. Kwa mujibu wa mtonyaji wangu, kati ya Majimbo ambayo Lowassa alikuwa tayari kutumia pesa yake yote ila wabaya wake wang'oke ni pamoja na Jimbo la Kyema. Lingine ni jimbo la Mtama.

Mwakyembe ndiye aliyeongoza Kamati ya Bunge la tisa kuchunguza Kampuni tata ya kufua umeme wa Dharura ya Richmond. Ripoti ya Kamati hii ndiyo iliyomng'oa LOWASSA kutoka kwenye uwasiri mkuu.
Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye ndiye aliyeibua ufisadi katika ujenzi wa JENGO la Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM) lililoko makutano ya barabara za Morogoro na Lumumba.

Matukio ambayo kipindi cha kampeni yalihusishwa na vita ya LOWASSA na hawa wabaya wake wawili ni matukio mawili katika jimbo la Mtama, moja likiwa ni ajali ambayo NAPE aliipata kweupeee kama ile ya Mch. Mtikila na lingine ni Nape kusingiziwa kujihusisha na rushwa wakati wa Kampeni.

Wakati hayo akitokea huko jimboni Mtama, Jimboni Kyela, Mbunge wa Ubungo kupitia CHADEMA ambaye ndiye aliyeandika Makala zaidi ya 70 kupitia zageti lake la MWANAHALISI kuwa LOWASSA ni FISADI alitumwa kwenda kumshambulia Mwakyembe. KUBENEA alishinikizwa na Chama chake kwenda kumshambulia Mwakyembe kwa vile kati ya Maadui wakubwa wa LOWASSA kwenye ulingo wa siasa, yeye alikuwa wa pili baada ya Mwakyembe.

TAHADHARI: Kwa uteuzi huu wa MUHONGO, MWAKYEMBE NA NAPE. Ni lazima Rais Magufuli afanye kazi na akina Mengi na Lowassa kwa tahadhari kubwa sana. Watamchekea kwa kumuonesha Magego yao, lakini mioyo yao haitakaa imchekee kamwe.

Wote tunaoponda Uteuzi wa Muhongo, Mwakyembe na Nape tuko nyuma tu ya akina Lowassa na Mengi. Tunafuata tu Mkumbo. Kosa la hawa ni nini? Hawana dhambi yoyote zaidi ya kuchukiwa na hao kwa sababu tu ya ukwasi wao fedha. Wanyonge wote hawa ndiyo wa kufanya nao kazi , tuwakumbatia ili wamsaidie rais wetu kufikia matamanio yetu.
Kwanza Lowasa hana Tatizo na Muhongo hilo weka pembeni kabsa nje ya Siasa ni rafiki yake Mkubwa na kama wana Ugonvi na mengi watasuruhishwa watapatana, kuhusu Mwakyembe na Nape hao ki Ukweli ni maadui wa Lowasa lakini ni Marafiki wa Mengi, Uadui wa Nape ulianza siku nyingi lakini ukaja kuchochewa zaidi na Membe kumnunua Nape Kwa kumpatia mapesa kibao toka kwenye Handaki alikoficha Mabilioni ya marehemu Gadafi hizo pesa zilitumika kuwanunua DR Slaa na lipumba huku Mwakyembe akivuta kote kote yaani alivuta pesa toka ikulu kwa JK na kwa Membe akasaidia kuwarubuni Slaa na lipumba, hivyo Uadui wao kwa Lowasa umechochewa na Membe kutokana na vita ya Urais.
 
Wote nyinyi mpo nyuma ya fisadi Lowassa tu. Watanzania tumewadharau wote. Mnapinga wazalendo walio likataa fisadi kwa maslahi ya taifa! Laana ya Mungu ipo juu yenu UKAWA wote.

Lowasa si Fisadi kwani Richmond ni Kikwete na Tambua kuwa Lowasa hana mda na nyingi, wananchi ndiyo wanalalamika tena wengi hawana itikadi ya chama chochote kile, kama kumdharau unamdharau ww mwenyewe na hawala yako kwani Lowasa ndiyo kakutuma kuiba pesa za Escrow? Lowasa ndiyo alinunua kivuko chakavu cha 1978 kwa billion 8 ? Zipo wapi billion 250 zilizopotea wazara ya Ujenzi zilipelekwa kwa Lowasa? Vp ile chenji ya Rada na ile ya bunge la katiba nayo alipelekewa Lowasa? Naona Umekariri Akili za Nape kila kitu ni Lowasa hata Kama hahusiki.
 
sidhani Dr Magufuli alikuwa anamaanisha kwawezesha wazalendo ili wawe madalali. Kilichopo ni watanzania kuoneana wivu na kuwatukuza wageni-Unajua Dangote mazingira aliyopewa Mtwara? Unajua mambo yake hayakuwa na mikwamo? Kapatiwa hekari 2500 za zaidi ajenge bandari yake , na huenda amepewa muda kabla ya kuanza kulipa kodi . Hivi ingalikuwa mangi ama bakhressa nyie watanganyika si mngepasuka kwa hasira? Mengi aliwahi kumkasirikia waziri masilingi kwa kuwabania wazalendo na kuiuza kilimanjaro hotel kwa wageni je mnadhani wawekezaji wazalendo wawe mafisi na wageni wawe masimba? yaani tubaki na masazo? tumieni uzalendo acheni chuki na ukabila ama kuwaogopa wachagga -ni upuuzi-Hamfurahi kuona azam yupo juu-je unategemea vyombo vyote vya habari vilalie ccm tu? kama star tv inayo take side na kutangaza habari za kikanda? Mbona ITV ilitoa fursa sawa na mwandishi wa ITV alikuwa begakwa bega na magufuli? Tuache umajitaka tuwe wazalendo nchi yetu inakaushwa na wageni sio wachagga ama mengi kama inavyotaka kuaminishwa -tuache u-intarahamwe

Asante sana mkuu. Watu wana uvivu wa kufikiri sana hii nchi. Hapo wanaweza kukuambia matajiri wa hii nchi wanatumia uchawi. Yani tuna kazi kubwa sana ya kuondoa ujinga
 
Lizaboni sioni tatizo kwa Mengi kuwa dalali wa vitalu vya gas as well as udalali wake unakuwa upo kisheria...mengi anamiliki makampuni mengi tu yakiwemo ya uchimbaji madini...#

Ni kwanini Muhongo hataki wazawa wahusike kwny biashara ya gas na mafuta???

Sospeter muhongo ni waziri msomi, namkubali sana, lakinj kwa hili la kuleta dharau kwa wazawa niko tofauti nae sana#

Kwanini Watanzania hata kuwa madalali wa vitalu vvitalu na badala yake udalali udalalinywe uwageni:rolleyes:imwe

Madini anayochimba Mengi urefu wake ni sawa na mashimo ya vyoo. Gesi hawezi
 
Last edited by a moderator:
Lizaboni sioni tatizo kwa Mengi kuwa dalali wa vitalu vya gas as well as udalali wake unakuwa upo kisheria...mengi anamiliki makampuni mengi tu yakiwemo ya uchimbaji madini...#

Ni kwanini Muhongo hataki wazawa wahusike kwny biashara ya gas na mafuta???

Sospeter muhongo ni waziri msomi, namkubali sana, lakinj kwa hili la kuleta dharau kwa wazawa niko tofauti nae sana#

Kwanini Watanzania hata kuwa madalali wa vitalu vvitalu na badala yake udalali udalalinywe uwageni:rolleyes:imwe
Mengi na wafanya biashara wengine hawakunyimwa vitalu waliambiwa hata kesho waende wizarani wakapewe vitalu kama wafanya biashara wengine. Wazawa wao wanamiliki vitalu kupitia TPDC (Gesi na Mafuta) na STAMICO (madini). Ukitaka umiliki binafsi maana yake una misuli ya hela kushindana kibiashara kwa hiyo ingia ushindane usitake kubebwa ili kuwa dalali
 
kijana unapaswa kuelewa nia njema ya Mengi nayo ni wananchi kumiliki uchumi msikilize magufuli

raia wetu wanapaswa kumiliki uchumi wajiunge pamoja hata kama ni gesi wanaweza kumiliki na tutawawezesha -na hiyo ndio hoja ya mengi-

muhongo-nyie wazalendo mnaweza kuuza juice tu.

Tata nilidhani ni GT kumbe nawe una tusiasa twa uchochoroni unataji tanzania nzima iwe inshangilia kila kitu -fikra huru ndio zitatujenga sio ukibaraka na umkiamkia
Mengi ni mwizi na mbinafsi. Nenda Norway kama utakuta njia kuu za uchumi kama zinamilikiwa na watu kama mengi. Watu wengine mmekulia tanzania tu hamjawahi kutoka na akina mengi wao wanajua kabisa akipewa yeye kama mengi haiwezi kufaidisha nchi. Kwa ufupi nchi zote zenye mafuta miradi yake huendeshwa na multinational kushirikiana na serikali. Kwa sababu sisi tunaanza acha tpdc ishike ila with time tutakuwa na tpdc kama mdau mkuu. Akina mengi wao waanzishe related industry ambazo gharama yake siyo kubwa
 
Baraza la mawaziri Nape??? Mhongo??? Mwakyembe na makontena??? Haihitaji degree kushangaa!!!

Masikini bado tunaamini Magufuli siyo jibu letu.
1. Tambua urais siyo mtu ni taasisi hivyo kuwa na fisadi chini ya taasisi makini na safi"CHADEMA" Ni bora kuliko Magufuli ndani ya fisiemu

2. Sheria bado ni zilezile hazitoa nafasi kushughulika na mafisadi .......
Poleeeeeeeee wewe uliyemuamini Magufuli mapema mimi badooooo!!!
 
Maneno mengiiiii
Ukweli unabaki Muhongo alishiriki kwenye wizi Ws Escrow
 
Tatizo la Mengi ni kuwa anataka kuwa dalali wa vitalu vya gesi. Kama ni serious investor, asingetaka mbeleko
Ni kweli mkuu,na kilichomfanya mengi amchukie zaidi muhongo ni pale alipotangaza kuwa mengi anamiliki vitalu zaidi ya 20 vya dhahabu ameacha mapori hajaviendeleza anasubiri kudalalia.muhongo futa kabisa hizo leseni
 
Endelea kuzungusha mikono. Subiri raisi wa moyo wako ateue baraza lake.
Kumbuka, tuko katika utawala mwingine.
 
Endelea kuzungusha mikono. Subiri raisi wa moyo wako ateue baraza lake.
Kumbuka, tuko katika utawala mwingine.

Braza mbona huwa unakuwa mkali sana pale ambapo watu ama wanapomkosoa Magufuli au wanapoelezea mashaka yao?
 
attachment.php

Baada ya Profesa Sospeter Muhongo kutangazwa kuwemo katika Baraza la Mawaziri la Serikali ya awamu ya Tano lililotangazwa na Rais Dk. John P Magufuli, kumezuka maneno mengi katika mitandao na vijiwe vya siasa kukosoa uteuzi huo kwa kile kinachotajwa kuwa ni tuhuma zake za kuhusika katika sakata la Escrow ambapo alilazimika kujiuzuru.

Aidha, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, aliyekuwa anagombea urais kwa tiketi ya CHADEMA kwa kuungwa mkono na UKAWA alijiuzuru mwaka 2008 baada ya kutuhumiwa kuhusika katika sakata la Richmond.
Je, uwezo wa kulitumikia Taifa hili wa wawili hawa unapimwa kwa kipimo kipi? .... ni ufisadi .... ni kuwajibika kisiasa .... au ........

Chanzo : Dar24
 
Attachments

  • 12316392_442464939271861_4285613504877249354_n.jpg
    12316392_442464939271861_4285613504877249354_n.jpg
    18.1 KB · Views: 896
Ni kutokana na uteuzi wa Dr. Harrison Mwakyembe na Prof. Sospeter Muhongo kwenye baraza lake la mawaziri.

Sakata la ESCROW liliwaweka karibu sana Mengi wote waliokuwa wakipigana usiku na mchana kuhakikisha Prof. Muhongo anajiuzulu kufuatia sakata hili. Kwa sababu ya Prof. Kuminya mianya ya watu kutaka kuwa madalali wa kuwekeza kwenye gesi, Reginald Mengi akiwa mmoja wao, nguvu nyingi zilitumika kuhakikisha Mzalendo huyu na mtetezi wa Wanyonge anaenguliwa, Pesa ni kila kitu, Prof hakuona sababu ya kushindana na kwa kuzingatia msemo, "MWENYE NGUVU MPISHE" aliamua kukaa pembeni.

Mwakyembe naye hatasahau uchaguzi wa Mwaka huu. Kati ya majimbo ya CCM yalikuwa magumu mwaka huu , basi ni jimbo la Kyela. Nguvu ya pesa ni mbaya sana. Mwakyembe alitumiwa kila aina majeshi kuhakikisha kwake siasa inaishia hapo. Mungu siyo Athumani , Kapenya. Kwa mujibu wa mtonyaji wangu, kati ya Majimbo ambayo Lowassa alikuwa tayari kutumia pesa yake yote ila wabaya wake wang'oke ni pamoja na Jimbo la Kyema. Lingine ni jimbo la Mtama.

Mwakyembe ndiye aliyeongoza Kamati ya Bunge la tisa kuchunguza Kampuni tata ya kufua umeme wa Dharura ya Richmond. Ripoti ya Kamati hii ndiyo iliyomng'oa LOWASSA kutoka kwenye uwasiri mkuu.

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye ndiye aliyeibua ufisadi katika ujenzi wa JENGO la Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM) lililoko makutano ya barabara za Morogoro na Lumumba.

Matukio ambayo kipindi cha kampeni yalihusishwa na vita ya LOWASSA na hawa wabaya wake wawili ni matukio mawili katika jimbo la Mtama, moja likiwa ni ajali ambayo NAPE aliipata kweupeee kama ile ya Mch. Mtikila na lingine ni Nape kusingiziwa kujihusisha na rushwa wakati wa Kampeni.

Wakati hayo akitokea huko jimboni Mtama, Jimboni Kyela, Mbunge wa Ubungo kupitia CHADEMA ambaye ndiye aliyeandika Makala zaidi ya 70 kupitia zageti lake la MWANAHALISI kuwa LOWASSA ni FISADI alitumwa kwenda kumshambulia Mwakyembe. KUBENEA alishinikizwa na Chama chake kwenda kumshambulia Mwakyembe kwa vile kati ya Maadui wakubwa wa LOWASSA kwenye ulingo wa siasa, yeye alikuwa wa pili baada ya Mwakyembe.

TAHADHARI: Kwa uteuzi huu wa MUHONGO, MWAKYEMBE NA NAPE. Ni lazima Rais Magufuli afanye kazi na akina Mengi na Lowassa kwa tahadhari kubwa sana. Watamchekea kwa kumuonesha Magego yao, lakini mioyo yao haitakaa imchekee kamwe.

Wote tunaoponda Uteuzi wa Muhongo, Mwakyembe na Nape tuko nyuma tu ya akina Lowassa na Mengi. Tunafuata tu Mkumbo. Kosa la hawa ni nini? Hawana dhambi yoyote zaidi ya kuchukiwa na hao kwa sababu tu ya ukwasi wao fedha. Wanyonge wote hawa ndiyo wa kufanya nao kazi , tuwakumbatia ili wamsaidie rais wetu kufikia matamanio yetu.

uko kwenye mstari chief.
 
Back
Top Bottom