Wosia aliouacha prof Muhongo mmeuelewa?

Wosia aliouacha prof Muhongo mmeuelewa?

Kwa tunaoelewa mambo Muhongo yupo sahihi. Norway ilipopata mafuta haikukabidhi wazawa kuendesha uchimbaji, ilileta wa USA, ila ilichokifanya ni kusomesha watu wake (pia kufungua vyuo vya Trondheim na Stavanger university) ili kusomesha wataalam. Ilichokifanya ni kuwa na umiliki kupitia serikali. Ilipofika kipindi wakaona labour force inatosha waliwafukuza wa USA na serikali kupitia STATOIL wakaendea na uchimbaji na wazawa wanachofaidi ni supporting industries (mfano vyakula, repairs za mitambo, ulinzi etc). Hiyo model iko pia uarabuni etc. sasa kwa nchi kama Tanzania hao akina mengi hawana ubavu na niwabinafsi. Model ilioichukua serikali ni sahihi, na uzuri mikataba ilishatiwa sahihi hakuna wa kubadilisha.

huna lolote kijakazi wa muhongo,huwezi kuwa,waziri halafu wizara unatufanyia udalali hela zetu huyu ni mwizi tu,aende tu mwana wa kwenda.
 
Wadau hapo mimi bado nina swali'ivi hizo rumbesa(mihela)bado si za umma?na km jibu ni ndio iweje viongoz wa umma kuachia ngazi?
 
huna lolote kijakazi wa muhongo,huwezi kuwa,waziri halafu wizara unatufanyia udalali hela zetu huyu ni mwizi tu,aende tu mwana wa kwenda.

Kwanza wewe utakuwa na matatizo ya kutokuelewa, na pili ni mvivu wa kusoma kilichoandikwa na wenzako. Mimi nimechangia kichwa cha habari, wewe unakurupuka tu. Jichunguze!
 
Katika series ya zilizala la escrow linaloendlea kupukutisha vigogo,leo ktk zamu ya prof Muhongo kufungasha virago kuna maneno machache kawaachia watz kwamba yeye anaondoka lakn wananchi muwe makini na RASILIMALI YA GESI HUENDA IKAWAFAIDISHA WATU WACHACHE NA FAMILIA ZAO TU..sasa me najiulza hivi kile kiporo kimechacha kabla ya kuliwa au ndo "UKIMWAGA UGALI NAMWAGA MBOGA".

Huyu jamaa ana mambo mengi sana ya uozo wa wizara, but yaelekea wamemtisha hasijaribu kusema.
 
Kwa tunaoelewa mambo Muhongo yupo sahihi. Norway ilipopata mafuta haikukabidhi wazawa kuendesha uchimbaji, ilileta wa USA, ila ilichokifanya ni kusomesha watu wake (pia kufungua vyuo vya Trondheim na Stavanger university) ili kusomesha wataalam. Ilichokifanya ni kuwa na umiliki kupitia serikali. Ilipofika kipindi wakaona labour force inatosha waliwafukuza wa USA na serikali kupitia STATOIL wakaendea na uchimbaji na wazawa wanachofaidi ni supporting industries (mfano vyakula, repairs za mitambo, ulinzi etc). Hiyo model iko pia uarabuni etc. sasa kwa nchi kama Tanzania hao akina mengi hawana ubavu na niwabinafsi. Model ilioichukua serikali ni sahihi, na uzuri mikataba ilishatiwa sahihi hakuna wa kubadilisha.

Mkuu hayo Yote yaweza kuwa mema, kosa la muhongo lilianzia pale alipo kubali kushiriki ukwapuaji wa hela tunazo languliwa kwenye umeme.
 
Kwanza wewe utakuwa na matatizo ya kutokuelewa, na pili ni mvivu wa kusoma kilichoandikwa na wenzako. Mimi nimechangia kichwa cha habari, wewe unakurupuka tu. Jichunguze!
Mkuu binafsi sijaona wosia wowote kutoka kwa aliyo sema.
 
Wewe ni miongoni mwa Watanzania wasiojielewa. Unampongeza kwa lipi? Kwa aibu aliyoaibisha leo? Baada ya kujua kuwa katemwa ndo anakimbilia kuitisha Press Conference kabla ya Ikulu?

Angekuwa mzalendo angejiuzuru bungeni siku maazimio yalipotolewa.

Nadhani ni wewe usioelewa alochofa na muhongo ni kuwahadarisha wananchi kuwa mafisadi papayananguvu hapa nchini na kwamba tujihadhari na watu kama wewe
 
Kwa tunaoelewa mambo Muhongo yupo sahihi. Norway ilipopata mafuta haikukabidhi wazawa kuendesha uchimbaji, ilileta wa USA, ila ilichokifanya ni kusomesha watu wake (pia kufungua vyuo vya Trondheim na Stavanger university) ili kusomesha wataalam. Ilichokifanya ni kuwa na umiliki kupitia serikali. Ilipofika kipindi wakaona labour force inatosha waliwafukuza wa USA na serikali kupitia STATOIL wakaendea na uchimbaji na wazawa wanachofaidi ni supporting industries (mfano vyakula, repairs za mitambo, ulinzi etc). Hiyo model iko pia uarabuni etc. sasa kwa nchi kama Tanzania hao akina mengi hawana ubavu na niwabinafsi. Model ilioichukua serikali ni sahihi, na uzuri mikataba ilishatiwa sahihi hakuna wa kubadilisha.

ndugu acha kuleta propaganda zako hapa serilikali ilisema hayo yatafanyika Mtwara matokeo yake ikaja na majibu hakuna wasomi kitu cha uongo kabisa, huyo muhongo bora alivyong'oka kiongozi gani anakashifu anaowaongoza
 
Huo ujenzi wa bomba la gesi bora wangekabidhiwa dawasco au duwasa tungeokoa mamilioni
 
Labda muhongo angekuwa mwanasiasa angeongea kisiasa ndio angeeleweka,kwani watalaamu hawajui siasa wanaongea fact il a tatizo la watanzania wanaaamini sana akin a kafulila na wenzake so tuwe wakweli nafsi zetu penye kuhitaji siasa na penye kuhitajika watalaamu tuache ,kwani ukisoma wachangiaji wengi hapa wpo kishabiki zaidi

facts zipi kashfa? hakuna jipya aliloonesha zaidi ameharibu cv yake ya taaluma
 
Labda muhongo angekuwa mwanasiasa angeongea kisiasa ndio angeeleweka,kwani watalaamu hawajui siasa wanaongea fact il a tatizo la watanzania wanaaamini sana akin a kafulila na wenzake so tuwe wakweli nafsi zetu penye kuhitaji siasa na penye kuhitajika watalaamu tuache ,kwani ukisoma wachangiaji wengi hapa wpo kishabiki zaidi
Kwahyo escrow ni siasa si kweli?,na wale waliofikishwa mahakaman wa TRA NA BOT?ni wanasiasa?sijui ukwel gan unaonaanisha hapa
 
Tatizo la dhahabu ni uhuni wa mzee mkapa na genge lake.
Kwanza kabisa kipindi cha kuruhusu uchimbaji wa madini tanzania hatukuwa na wataalam ( hata waliokuwepo hawakuwa na experience na wachache). Kosa lililofanyika na serikali ni kuacha kusomesha au kuwapeleka wataalam kupata ujuzi, kwa maana nyingine hapakuwa na succession plan, hatukuwa na wakaguzi waliobobea kwenye madini (nakumbuka kuna jamaa yangu mmoja alipata kazi ya ukaguzi wa madini wakati yeye ni mkaguzi wa kawaida tu hakuwa na utalaam wa madini).

Pili serikali iliwaamini sana wazungu kupitia rushwa na akina mzee mkapa wamelamba sana. Na kibaya zaidi serikali haikuwa na mtu mwenye uchungu na maliasili zetu yaani mpaka bungeni.

Ila Muhongo mchango wake mkubwa ni kuacha hiyo successsion plan na kuwezesha umiliki wa mafuta na gesi mikononi mwa serikali kupitia shirika lake.

Madini hata tukisema leo tupewe sidhani kama tunaweza jiendesha kwani waziri wa enzi hizo alikuwa mbumbu hakujua cha kufanya ili kutengeneza successsion plan.

Upo sahihi kabisa uyo mkapa madini kayamaliza yeye
 
Mwivi mkubwa huyo..akafie mbele..dalali tu hana maana atupishe
 
Kaniudhi sana kuwanyima tender ya kujenga bomba dawasco
 
Anyway Goodbye Muhongo! sijui wizara ya nishati na madini kuna mzimu gani?
 
Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni! Mimi binafsi namkubali Muhongo ktk utendaji kazi, nimeona mabadiliko makubwa toka achukue wizara in terms of kupungua kwa mgao wa umeme na Tz maeneo yenye mwanga yameongezeka kwa kiasi kikubwa!! Tunapoangalia 'mabaya' yake, tujaribu kuangalia na kukumbuka na mazuri pia!

usisahau na kuongezeka kwa gharama za umeme maradufu
 
By gones be so. . . . . . . . .!!!!!

Wasomi wengine wa hadhi ya juu watajifunza sasa kufanyia kazi taaluma zao na wajijue kuwa wao na wanasiasa hawawezi kuchanganyika daima!!!

Wajutie madudu yao katika bunge la katiba haswa kuhusu elimu ya wabunge na kutenganisha uwaziri na ubunge!!!

Laana hii iendelee kuwatafuna woote waliobaki wakielewa umuhimu ya kutenganisha fani na siasa lakini wakafumbia macho kwa maslahi yao kisiasa!!!
 
Mnafiki huyu, mpaka rais kamuwekea mashushushu wamegundua ana billions of shillings kwa account yake ya siri ndio akatonywa ajiuzulu mapema kwasababu habebeki.

Why do uneducated people behave in a different way?
 
By gones be so. . . . . . . . .!!!!!

Wasomi wengine wa hadhi ya juu watajifunza sasa kufanyia kazi taaluma zao na wajijue kuwa wao na wanasiasa hawawezi kuchanganyika daima!!!

Wajutie madudu yao katika bunge la katiba haswa kuhusu elimu ya wabunge na kutenganisha uwaziri na ubunge!!!

Laana hii iendelee kuwatafuna woote waliobaki wakielewa umuhimu ya kutenganisha fani na siasa lakini wakafumbia macho kwa maslahi yao kisiasa!!!

Wosia wako huu anapaswa siyo prof Muhongo tu,mtu kama Dr Mwakyembe aliyeikana thesis yake wakati wa BMK, lakini jana kilichomtokea yeye na familia yake wanajua nini maana ya siasa ni SI HASA kweli. Wanataaluma tuzibgatie taaluma zetu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom