Uhuni aliofanya Muhongo leo hata Mimi niliwahi kuufanya pale Vwawa, nilimpiga jamaa nikamtoa manundu halafu nikakimbia fasta kwenda kushtaki polisi. Jamaa alipopata nguvu na kwenda kushtaki akakuta tayari askari wanajipanga kwenda kumkamata. Ndio ya Muhongo leo, alijua fika kuwa anapigwa chini na mawaziri wapya wameitwa kuapishwa, akawahi kuitisha press conference kabla ya muda wa Ikulu kuzuga kuwa amejiuzuru. Tujiulize, je asingejiuzuru angebakia kwenye baraza jipya? Je hao mawaziri wapya walioapishwa walipewa notice ya masaa manne kati ya kujiuzuru Muhongo na kuapishwa kwao?