Wosia aliouacha prof Muhongo mmeuelewa?

Wameficha mikataba waliofunga na makampuni ya kuchimba gesi na mafuta leo hii anakuja kusema tuwe makini. Angeanzia kuiweka wazi hiyo mikataba.
 
Tatizo la dhahabu ni uhuni wa mzee mkapa na genge lake.
Kwanza kabisa kipindi cha kuruhusu uchimbaji wa madini tanzania hatukuwa na wataalam ( hata waliokuwepo hawakuwa na experience na wachache). Kosa lililofanyika na serikali ni kuacha kusomesha au kuwapeleka wataalam kupata ujuzi, kwa maana nyingine hapakuwa na succession plan, hatukuwa na wakaguzi waliobobea kwenye madini (nakumbuka kuna jamaa yangu mmoja alipata kazi ya ukaguzi wa madini wakati yeye ni mkaguzi wa kawaida tu hakuwa na utalaam wa madini).

Pili serikali iliwaamini sana wazungu kupitia rushwa na akina mzee mkapa wamelamba sana. Na kibaya zaidi serikali haikuwa na mtu mwenye uchungu na maliasili zetu yaani mpaka bungeni.

Ila Muhongo mchango wake mkubwa ni kuacha hiyo successsion plan na kuwezesha umiliki wa mafuta na gesi mikononi mwa serikali kupitia shirika lake.

Madini hata tukisema leo tupewe sidhani kama tunaweza jiendesha kwani waziri wa enzi hizo alikuwa mbumbu hakujua cha kufanya ili kutengeneza successsion plan.

Kuna wa TZ wengi waliokuwa wanafanya kazi katika migodi ya dhahabu ya Geita, Bulyanhulu , Nzega naN/Mara wanafanya kazi Nje ya Nchi mkuu. Wanaogopwa na hawa wezi wa dhahabu, wananyanyasa kwa mshahara midogo licha ya kuwa na qualification na experience kuwazidi wafanyakazi wanatoka nje.
 
Huyu jamaa alipewa ubunge wa viti maalumu ili awe waziri wa nishati na madini, na hii ilitokana na elimu, ueledi ,pamoja na uzoefu wake mkubwa kwenye hiyo sekta.
sasa kutokana na hii scandal ya escrow ambayo yeye aliikuta imeshachezwa na wajanja na yeye ni kama zigo limemwangukia yeye.
Kutokana na level yake ya kielimu, na ukizingatia muda mfupi uliobaki kabla ya bunge kuvunjwa na hategemei kugombea ubunge 2015.
NI HERI YAKO MZEE MUHONGO UJIUDHURI NA HUO UBUNGE WALIOKUPA ILI UWAONYESHE KWAMBA UMEKASIRIKA KWA KUANGUSHIWA JUMBA BOVU LA ESCRO
 
Muhongo hana uwezo wa kufundisha chuo kikuu. Uwaziri umefichua mengi kuhusu huyu muheshimiwa.

Hamewezaje kufika hapo alipo kitaaluma still puzzle to me!
 
Lazima tumkumbuke maana kauli yake kwamba watanzania ni wababaishaji na kwamba wana hela za juice haitafutika leo wala kesho. Unakumbuka aliyetuambia tule nyasi ili...Hivi kuna nchi yenye rekodi ya kuwa na viongozi wanaodharau wananchi wao kama yetu ??
Mkuu kama watanzania wenyewe ndo hao wenye akili kama zakina Roho Mbaya kwa nini wasitudharau?
 
Wameficha mikataba waliofunga na makampuni ya kuchimba gesi na mafuta leo hii anakuja kusema tuwe makini. Angeanzia kuiweka wazi hiyo mikataba.
Muhongo ni panya kama panya wengine ndani ya ccm.apuuzwe tu hana jipya zaidi ya hadaa.
 
Akapumzke tu kama Nyerere naye alikuwepo na wosia ameacha mia kidogo na nchi bado inaendlea sembuse Muhongo ndio ataitikisa?? Labda kwa lipi hlo? Yeye ni nani labda mpaka tuogope kujiuzulu kwake? Mbona majembe yapo tele na wana vyuo mahiri wanaendlea toka vyuoni kila mwaka tutapata tu taratibu huo ukombozi koz kuna msemo unasema Rome wasnt build in a Day so Tanzania pia haita jengwa kwa siku moja wala na Muhongo na familia yake. Ila na watanzania wenyewe

Sent from my BlackBerry 9790 using JamiiForums
 
Yes, ni kweli tutamkumbuka kwa kuwa Prof mbabaishaji anayetegemea majivuno na hisia binafsi kwenye mambo ya kitaifa. Lakini hatimaye alidhalilika.
Prof. Muhongo atabaki kuwa mtu ambaye ameitendea haki nchi hii kwa kusimamia vyema wizara yake. Ameleta mabadiliko makubwa sana kwenye idara ambazo zipo chini ya wizara. Ameingia kuna mgawo wa Umeme wa kufa mtu, watu wanapiga dili za udalali wa kuuza majenereta, leo maduka ya majenerata hakuna.

ni bahati mbaya sana kwamba mafisadi wa vitalu, waliokuwa wakiinyonya TANESCO, mafisadi wa mafuta , mafisadi wa elimu (nakumbuka siku anataka kusoma matokeo ya mtu bungeni) wamefanikiwa kumumaliza. Ila ametuonyesha kwamba mgawo ulikuwa wa kutengeneza na mafisadi hawawezi tena kuingilia hapo.
 
Muhongo alitaka kuwamilikisha gesi yote watu wa nje leo baada ya kung'oka ndo anasema gesi iwanufaishe wachache akina nani, afadhali iwanufaishe wachache wazawa kuliko wachache kutoka ughaibuni
Wazawa gani? Madalali?
 
hana lolote sasa hivi ndo anajifanya kuwa na uchungu na rasilimali za nchi... aende uko..

si alisema akijiuzulu nchi itatkisika????????? mbona sijaona mtikisiko wowote tangu jana?? sanasana naona wananchi wana furaha ya ajabu,ni vifijo na nderemo vimetawala mitaani
 
Yeye ametusaidia nini ktk kuisimamia rasilimali hizo ikiwa mikataba hakuiweka wazi. Mpuuzi kabisa huyu, jizi kuu! Sasa anawaonea gere watakaofaidi yeye out!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom