Wosia aliouacha prof Muhongo mmeuelewa?

Boutafrica

JF-Expert Member
Dec 11, 2014
954
2,070
Katika series ya zilizala la escrow linaloendlea kupukutisha vigogo,leo ktk zamu ya prof Muhongo kufungasha virago kuna maneno machache kawaachia watz kwamba yeye anaondoka lakn wananchi muwe makini na RASILIMALI YA GESI HUENDA IKAWAFAIDISHA WATU WACHACHE NA FAMILIA ZAO TU..sasa me najiulza hivi kile kiporo kimechacha kabla ya kuliwa au ndo "UKIMWAGA UGALI NAMWAGA MBOGA".
 
hana lolote sasa hivi ndo anajifanya kuwa na uchungu na rasilimali za nchi... aende uko..
 
Atajiju sasa hivi ndo anawajali sana watanzania, alipokuww anawatukana, ilikuwaje?.
 
Boss Mimi binafsi nampongeza Mhongo kwa maamuzi aliyofanya, hata kama ni kwa kushinikizwa lakini ametekeleza kile ambacho bunge lilipendekeza na ambacho wananchi walikuwa wanakisubiri kwa hamu. Ni moja ya uzalendo na uwajibikaji. Ni mategemeo yangu kuwa waliobaki au walioingia upya katika nyazfa mbali mbali wamejifunza kutoka sakata hili la escrow. Kinachonikera ambacho bado sijapata majibu yake ni fedha hizo zilizopotea, zitarudije ili ziwafae maskini vijijini na wanafunzi wanaokosa hadi chaki ya kuandikia kama hatujataja madawati ya kukalia?
 
hana lolote sasa hivi ndo anajifanya kuwa na uchungu na rasilimali za nchi... aende uko..

Kwa tunaoelewa mambo Muhongo yupo sahihi. Norway ilipopata mafuta haikukabidhi wazawa kuendesha uchimbaji, ilileta wa USA, ila ilichokifanya ni kusomesha watu wake (pia kufungua vyuo vya Trondheim na Stavanger university) ili kusomesha wataalam. Ilichokifanya ni kuwa na umiliki kupitia serikali. Ilipofika kipindi wakaona labour force inatosha waliwafukuza wa USA na serikali kupitia STATOIL wakaendea na uchimbaji na wazawa wanachofaidi ni supporting industries (mfano vyakula, repairs za mitambo, ulinzi etc). Hiyo model iko pia uarabuni etc. sasa kwa nchi kama Tanzania hao akina mengi hawana ubavu na niwabinafsi. Model ilioichukua serikali ni sahihi, na uzuri mikataba ilishatiwa sahihi hakuna wa kubadilisha.
 
Boss Mimi binafsi nampongeza Mhongo kwa maamuzi aliyofanya, hata kama ni kwa kushinikizwa lakini ametekeleza kile ambacho bunge lilipendekeza na ambacho wananchi walikuwa wanakisubiri kwa hamu. Ni moja ya uzalendo na uwajibikaji. Ni mategemeo yangu kuwa waliobaki au walioingia upya katika nyazfa mbali mbali wamejifunza kutoka sakata hili la escrow. Kinachonikera ambacho bado sijapata majibu yake ni fedha hizo zilizopotea, zitarudije ili ziwafae maskini vijijini na wanafunzi wanaokosa hadi chaki ya kuandikia kama hatujataja madawati ya kukalia?

Wewe ni miongoni mwa Watanzania wasiojielewa. Unampongeza kwa lipi? Kwa aibu aliyoaibisha leo? Baada ya kujua kuwa katemwa ndo anakimbilia kuitisha Press Conference kabla ya Ikulu?

Angekuwa mzalendo angejiuzuru bungeni siku maazimio yalipotolewa.
 
Muhogo tutakukumba daima

Lazima tumkumbuke maana kauli yake kwamba watanzania ni wababaishaji na kwamba wana hela za juice haitafutika leo wala kesho. Unakumbuka aliyetuambia tule nyasi ili...Hivi kuna nchi yenye rekodi ya kuwa na viongozi wanaodharau wananchi wao kama yetu ??
 
Kwa tunaoelewa mambo Muhongo yupo sahihi. Norway ilipopata mafuta haikukabidhi wazawa kuendesha uchimbaji, ilileta wa USA, ila ilichokifanya ni kusomesha watu wake (pia kufungua vyuo vya Trondheim na Stavanger university) ili kusomesha wataalam. Ilichokifanya ni kuwa na umiliki kupitia serikali. Ilipofika kipindi wakaona labour force inatosha waliwafukuza wa USA na serikali kupitia STATOIL wakaendea na uchimbaji na wazawa wanachofaidi ni supporting industries (mfano vyakula, repairs za mitambo, ulinzi etc). Hiyo model iko pia uarabuni etc. sasa kwa nchi kama Tanzania hao akina mengi hawana ubavu na niwabinafsi. Model ilioichukua serikali ni sahihi, na uzuri mikataba ilishatiwa sahihi hakuna wa kubadilisha.
Upo sahihi kabisa. Lakini sisi tumbili kawaida yetu kuibiwa tu. Mbona dhahabu imechimbwa na kuondoka hatujafaidi lolote sana sana wazawa wamefukuzwa kwenda sehemu za mashamba yao kupisha uchimbaji, wengine wameuwawa na wengine wanakunywa maji ya sumu (mercury) lakini Muhongo hajafanya kitu hapo. anakuwa na uchungu wa mafuta na gesi wakati rasilimai nyingine inaondoka yupo yupo tu. Hao aliokuwa anawapata mikataba ya gesi ndiyo hao hao walikuwa wanachimba dahabu.
 
Uhuni aliofanya Muhongo leo hata Mimi niliwahi kuufanya pale Vwawa, nilimpiga jamaa nikamtoa manundu halafu nikakimbia fasta kwenda kushtaki polisi. Jamaa alipopata nguvu na kwenda kushtaki akakuta tayari askari wanajipanga kwenda kumkamata. Ndio ya Muhongo leo, alijua fika kuwa anapigwa chini na mawaziri wapya wameitwa kuapishwa, akawahi kuitisha press conference kabla ya muda wa Ikulu kuzuga kuwa amejiuzuru. Tujiulize, je asingejiuzuru angebakia kwenye baraza jipya? Je hao mawaziri wapya walioapishwa walipewa notice ya masaa manne kati ya kujiuzuru Muhongo na kuapishwa kwao?
 
Kwani alifanya Muhongo au Serikali?
Kwa tunaoelewa mambo Muhongo yupo sahihi. Norway ilipopata mafuta haikukabidhi wazawa kuendesha uchimbaji, ilileta wa USA, ila ilichokifanya ni kusomesha watu wake (pia kufungua vyuo vya Trondheim na Stavanger university) ili kusomesha wataalam. Ilichokifanya ni kuwa na umiliki kupitia serikali. Ilipofika kipindi wakaona labour force inatosha waliwafukuza wa USA na serikali kupitia STATOIL wakaendea na uchimbaji na wazawa wanachofaidi ni supporting industries (mfano vyakula, repairs za mitambo, ulinzi etc). Hiyo model iko pia uarabuni etc. sasa kwa nchi kama Tanzania hao akina mengi hawana ubavu na niwabinafsi. Model ilioichukua serikali ni sahihi, na uzuri mikataba ilishatiwa sahihi hakuna wa kubadilisha.
 
Eti alimwomba rais ajiuzulu wakati alikuwa amewekwa kiporo. Nilidhani angesema na ubungr hautaki anarudi zake kwenye kufundisha. Kumbe atabaki bungeni kama mbunge wa kawaida. Pride comes before a fall.
 
Katika series ya zilizala la escrow linaloendlea kupukutisha vigogo,leo ktk zamu ya prof Muhongo kufungasha virago kuna maneno machache kawaachia watz kwamba yeye anaondoka lakn wananchi muwe makini na RASILIMALI YA GESI HUENDA IKAWAFAIDISHA WATU WACHACHE NA FAMILIA ZAO TU..sasa me najiulza hivi kile kiporo kimechacha kabla ya kuliwa au ndo "UKIMWAGA UGALI NAMWAGA MBOGA".

Muhongo alitaka kuwamilikisha gesi yote watu wa nje leo baada ya kung'oka ndo anasema gesi iwanufaishe wachache akina nani, afadhali iwanufaishe wachache wazawa kuliko wachache kutoka ughaibuni
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom