World Economic Forum yaja - wadaresalama mtapita wapi?

WomanOfSubstance

JF-Expert Member
May 30, 2008
5,457
956
KUNA TANGAZO TBC1 kuwa kuanzia tarehe 4 May 2010 WAGENI WA WEF wanakuja nchini hivyo tuwapishe barabara - sasa tutapita wapi na ilhali hata bila ugeni barabara hazipitiki!
 
Wawape likizo msiende kazini. Pia hakikisheni mnanunua mahitaji yenu ya kila siku mapema. Pia ombeni umeme usikatike ili vyakula vyenu kwenye majokofu visiharibike. Ni hayo tu.
 
tena nimepita leo mlimani nimecheka sana..yaaani wanapanda miti /minazi sijui ile wameing'oa wapi huko ili ionekane imeoteshwa siku nyingi..kweli upumbavu ni kitu kibaya sana
 
tena nimepita leo mlimani nimecheka sana..yaaani wanapanda miti /minazi sijui ile wameing'oa wapi huko ili ionekane imeoteshwa siku nyingi..kweli uoumbafu ni kitu kibaya sana
Kigogo,
Umenichekesha. Lakini kweli upumbafu kitu kibaya sana.
 
Wawape likizo msiende kazini. Pia hakikisheni mnanunua mahitaji yenu ya kila siku mapema. Pia ombeni umeme usikatike ili vyakula vyenu kwenye majokofu visiharibike. Ni hayo tu.

Jasusi,
Unajua kuna watu "wasipotoka" familia zitalala njaa?
 
Upumbavu mtupu! wanajua Dar ilivyokuwa na msongamano mkubwa wa magari halafu bado wanataka kufanya forum kubwa kama hii Dar. Itakuwa raha sana mvua kama ya wiki iliyopita ipige tena kwa siku nne tu labda watapata fundisho kwamba Dar haina infrastructures ya kufanya kikao chochote kikubwa duniani, Afrika au hata katika East Africa tu. Kwa nini hawakupeleka kikao hichi Arusha? Ni nani aliyeamua kikao hiki kifanyike Dar? Hivi makao makuu ya nchi yetu ni wapi vile? Kwanini hawakupeleka kikao hichi kule?
 
tena nimepita leo mlimani nimecheka sana..yaaani wanapanda miti /minazi sijui ile wameing'oa wapi huko ili ionekane imeoteshwa siku nyingi..kweli upumbavu ni kitu kibaya sana

Kigogo! hata mimi nilipoiona Ikanikumbusha enzi zile tunatembelewa na wakuu wa nchi mashuleni tunapaka mawe choka! Ha ha ha! Yaani mvua ikinyesha usiku ni balaa maana chokaa yote kwish nehi!!!

By the way nimepita hapo tena few minute ago bado wapo wnapanda hizo Royal palms usiku huu! na other shrubs kwa chini itapepewa mpaka hiyo kesho kutwa iwe imesimama. As if wamepewa taarifa za huo mkutano jana jioni! Hivi ni upuuzi wa namna gani? Au waandalizi walioletwa kuangalia hali ilivyo wamesema panatakiwa royal palms la sivyo hakuna mkutano!

Sasa hilo la Lukuvi kusema barabara zinatumika na wageni kati ya saa moja na tatu asb na tena saa tisa mpaka saa moja usiku...mmmmmmmh! Sijui tunapita wapi siku hizo! Ikianguka na mvua kama ile ya wiki iliyopita mashaka ya mji huu ndio yatakuwa yamefika mahali pake.
 
Upumbavu mtupu! wanajua Dar ilivyokuwa na msongamano mkubwa wa magari halafu bado wanataka kufanya forum kubwa kama hii Dar. Itakuwa raha sana mvua kama ya wiki iliyopita ipige tena kwa siku nne tu labda watapata fundisho kwamba Dar haina infrastructures ya kufanya kikao chochote kikubwa duniani, Afrika au hata katika East Africa tu. Kwa nini hawakupeleka kikao hichi Arusha? Ni nani aliyeamua kikao hiki kifanyike Dar? Hivi makao makuu ya nchi yetu ni wapi vile? Kwanini hawakupeleka kikao hichi kule?

ndugu yangu labda wangepeleka Dodoma, sie huku tumeshachoshwa na hiyo mikutano.......wakishajazana ndio basi tena barabara zetu hizi mbili wakishazimiliki ndio huwa tunajifehemu,msongamano wa hatari, maisha yanakuwa ghali, kijimji chenyewe badala wakipanue ndio kiko vile vile kila siku..kwa kweli tumechoshwa na hali hii, kwani makao makuu ya nchi kazi yake ni nini?
 
Upumbavu mtupu! wanajua Dar ilivyokuwa na msongamano mkubwa wa magari halafu bado wanataka kufanya forum kubwa kama hii Dar. Itakuwa raha sana mvua kama ya wiki iliyopita ipige tena kwa siku nne tu labda watapata fundisho kwamba Dar haina infrastructures ya kufanya kikao chochote kikubwa duniani, Afrika au hata katika East Africa tu. Kwa nini hawakupeleka kikao hichi Arusha? Ni nani aliyeamua kikao hiki kifanyike Dar? Hivi makao makuu ya nchi yetu ni wapi vile? Kwanini hawakupeleka kikao hichi kule?

Hili nalo neno!
HUU MKUTANO haukuja ghafla. Ulipangwa kwa muda mrefu. Viongozi wetu wanajua fika adha inayowapata wakazi wa Dar - in short quality of life imeshuka sana kwa maana ya muda mtu anaotumia barabarani .Kuamka ni saa kumi za alfajiri ili angalau kumi na moja na nusu uanze safari ya kwenda kwenye mihangaiko.

Jioni nayo mtu hutumia masaa kibao hadi ufike majumbani. Kuingia ni kwenye saa 2- 3 usiku. In short unatoka kombora unarudi chombeza. Ni saa ngapi mtu ataangalia maendeleo ya nyumbani? Kusimamia watoto wafanye homework, kuangalia familia kwa mahitaji mbalimbali - bado mahusiano ya wanafamilia na wana ndoa.Hii ni kwa upande wa masuala ya kijamii. Bado hatujaangalia mambo ya kiuchumi - masaa yanayopotelea barabarani kwenye foleni, petrol/diesel inayotumika bure katika foleni etc. Sasa tunaambiwa kuna wageni tuwapishe - itakuwa ngumu kweli.Yetu macho.
 
Sasa tunaambiwa kuna wageni tuwapishe - itakuwa ngumu kweli.Yetu macho.

WOS, tatizo la hiyo kauli ya kuambiwa tuwapishe hatutakuwa na la kufanya maana wazee wa favour wakikupiga mkono wanasahau kugeuka upande huo kwa hayo masaa waliyosema wanawapitisha wakuu. Ugumu utakuwa masaa tutakayosimamishwa wamalize kupita! Pengine mgomo wa wafanyakazi hapa utasaidia...maana ni tarehe hiyo haswa 5th may:behindsofa:
 
hiii nchi kama tuko kwenye speed train to hell.......
yaani utasema huwa tunafaidika na mikutano kama hiyo......
ni porojo tu kwa kwenda mbele......

it is very depressing na viongozi kama hawa....
 
Hivi hii WEF ni kama ile inayofanyikaga Davos au hii ni mdogo wake? Maana ile ya Davos kama sikosei huwaga inafanyika mwezi wa kwanza au wa pili....sasa hii imetoka wapi?
 
Preparations for this meeting is in top gear! Whatever that means!
200 DELEGATES expected to arrive... most probably each will have own vehicle... patakuwa hapatoshi!
 
Tatizo letu waTZ tunapenda sana misifa na vitu vilivyo nje ya uwezo wetu na kumbe wakati mwingine tunajidhalilisha.
 
Nimeisikia hii habari katika radio leo asubuhi kuwa barabara ya Nyerere na Ali Hassani Mwinyi zitafungwa ili kuwapisha wageni wanaokuja kwenye mkutano wa maedeleo Africa.

Je,hii imekaaje waungwana?
 
Back
Top Bottom