Kinkunti El Perdedo
JF-Expert Member
- Nov 28, 2020
- 4,539
- 11,120
International Women's Day ni siku muhimu sana katika kuweka uzani Sawa wa kijinsia. Kutokana na hapo mwanzo kuwepo kwa mifumo ambayo haikutoa fursa Sawa, katika nyanja mbalimbali za kimaisha, lakini leo hii kila mtu ni shaidi kwamba taifa letu limepiga hatua nzuri na hadhimu katika kuwaleta wanawake pamoja ili kufaidika na fursa zote, mpaka kushika sehemu muhimu na nyeti mfano ni katika mihimili miwili ya serikali yaani utawala (Mh. Samia Suluhu Hassan) na Bunge (Dr. Tulia Ackson).
Tunapofanya maadhimisho haya kila mwaka, kwa kueleza mafanikio ya wanawake katika hatua mbalimbali hasa katika njia kuu nne za maisha yaani kisiasa, kiuchumi, kijamii na sayansi na teknolijia, Tusijikite katika kutoa fursa Sawa ili kuleta usawa bila kuzingatia uwezo, uwajibikaji na weredi.
Kwa kuzingatia mambo hayo, nimekuja na swali. Je, katika taifa letu Tanzania tuna wanawake wenye uwezo kama Margaret Hilda Thatcher ambaye kutokana na uwezo wake, uwajibikaji na weledi wake akapatiwa jina la "Iron lady" na Angela Dorothea Merkel ambaye naye kutokana na uwezo wake, uwajibikaji na weredi wake amekuwa "Icon lady" katika Siasa za Ulaya Magharibi.
NB: Margaret Hilda Thatcher na Angela Dorothea Merkel sio wanawake pekee waliofanya mambo makubwa duniani, bali nimefanya kama mfano tu.