WOMEN'S DAY: Tunao wanawake wenye uwezo kama Margaret Thatcher na Angela Merkel?

Kinkunti El Perdedo

JF-Expert Member
Nov 28, 2020
4,485
11,036
International Women's Day ni siku muhimu sana katika kuweka uzani Sawa wa kijinsia. Kutokana na hapo mwanzo kuwepo kwa mifumo ambayo haikutoa fursa Sawa, katika nyanja mbalimbali za kimaisha, lakini leo hii kila mtu ni shaidi kwamba taifa letu limepiga hatua nzuri na hadhimu katika kuwaleta wanawake pamoja ili kufaidika na fursa zote, mpaka kushika sehemu muhimu na nyeti mfano ni katika mihimili miwili ya serikali yaani utawala (Mh. Samia Suluhu Hassan) na Bunge (Dr. Tulia Ackson).

Tunapofanya maadhimisho haya kila mwaka, kwa kueleza mafanikio ya wanawake katika hatua mbalimbali hasa katika njia kuu nne za maisha yaani kisiasa, kiuchumi, kijamii na sayansi na teknolijia, Tusijikite katika kutoa fursa Sawa ili kuleta usawa bila kuzingatia uwezo, uwajibikaji na weredi.

Kwa kuzingatia mambo hayo, nimekuja na swali. Je, katika taifa letu Tanzania tuna wanawake wenye uwezo kama Margaret Hilda Thatcher ambaye kutokana na uwezo wake, uwajibikaji na weledi wake akapatiwa jina la "Iron lady" na Angela Dorothea Merkel ambaye naye kutokana na uwezo wake, uwajibikaji na weredi wake amekuwa "Icon lady" katika Siasa za Ulaya Magharibi.

NB: Margaret Hilda Thatcher na Angela Dorothea Merkel sio wanawake pekee waliofanya mambo makubwa duniani, bali nimefanya kama mfano tu.

download-1.jpg
download.jpg
 
Wanawake hao wawili wa shoka ninawatazama kwa mfano. Binafsi naamini ipo siku nitafanya/kuwa wa mfano mahali.
Sio katika uongozi, popote pale nitakapokuwa nitaacha alama.

Hata hapa JF si nina alama ya ubuyu jamani? Lols
 
Wanawake hao wawili wa shoka ninawatazama kwa mfano. Binafsi naamini ipo siku nitafanya/kuwa wa mfano mahali.
Sio katika uongozi, popote pale nitakapokuwa nitaacha alama.

Hata hapa JF si nina alama ya ubuyu jamani? Lols
Kwanini usiingie katika siasa? maana uwezo,nia na nguvu unazo ili uje kuwa kama hao wawili.
 
Kwa jinsi mambo yanavyokwenda sasa hivi kama sio hesabu zake mbovu na tamaa alikuwa na nafasi kubwa ya kuja kuwa Mwenyekiti wa kwanza mwanamke Chadema baada ya kuiongoza Bawacha kwa mafanikio.
Atakuwa Katibu mkuu wa CCM Baada ya Nchimbi Kuwa Rais 2030
 
Wakiacha fikra za kuongeza matako na kusaka mikorogo new model tunaweza kupata vizazi vijavyo, kutoka kwa wajukuu zao
 
Happy women's day ni siku muhimu sana katika kuweka uzani Sawa wa kijinsia.kutokana na hapo mwanzo kuwepo kwa mifumo ambayo haikutoa fursa Sawa,katika nyanja mbalimbali za kimaisha.Lakini leo hii kila mtu ni shaidi kwamba taifa letu limepiga hatua nzuri na hadhimu katika kuwaleta wanawake pamoja ili kufaidika na fursa zote,mpaka Kushika sehemu muhimu na nyeti mfano ni katika mihimili miwili ya serikali yaani utawala (Mh SAMIA SULUHU HASSAN) na Bunge (Dr Tulia Ackson).

Tunapo fanya maadhimisho haya kila mwaka,kwa kueleza mafanikio ya wanawake katika hatua mbalimbali hasa katika njia kuu Nne za maisha yaani kisiasa,kiuchumi,kijamii na sayansi na teknolijia,Tusijikite katika kutoa fursa Sawa ili kuleta usawa bila kuzingatia uwezo, uwajibikaji na weredi.

Kwa kuzingatia mambo hayo,nimekuja na swali Je,Katika taifa letu Tanzania tuna wanawake wenye uwezo kama Margaret Hilda Thatcher ambaye kutokana na uwezo wake, uwajibikaji wake na weredi wake akapatiwa jina la "Iron lady" na Angela Dorothea Merkel ambaye nae kutokana na uwezo wake,uwajibikaji wake na weredi wake amekuwa "Icon lady" katika siasa za Ulaya Magharibi.

NB:Margaret Hilda Thatcher na Angela Dorothea Merkel sio wanawake pekee waliofanya mambo makubwa duniani,bali nimefanya kama mfano tu.

Trust me!
SSH is so powerful and the best political Navigator!

Courageous
Politically Stable
Resilient and daring!

TA
High IQ
Learned
Focused
Exposed

Acha wanawake watuongoze kama ulivyosema Angela Michael and more others!

Sent from my SM-A307FN using JamiiForums mobile app
 
Trust me!
SSH is so powerful and the best political Navigator!

Courageous
Politically Stable
Resilient and daring!

TA
High IQ
Learned
Focused
Exposed

Acha wanawake watuongoze kama ulivyosema Angela Michael and more others!

Sent from my SM-A307FN using JamiiForums mobile app
Kuongozwa na wanawake sio tatizo.swali tunawapa nafasi kwa kuzingatia uwezo,uwajibikaji na weredi ?

Au tunawapa nafasi ili kukizi tu sifa ya gender equality.
 
Tuweke usawa. Hii ni awamu ya kwanza ya mwanamke Tanzania. Bado tuna awamu nne mbele yetu tuendelee kuongozwa na mwanamke. Baada ya Samia, 2030 tunampa kijiti Tulia Ackson Mwansasu kuwa na Rais wa pili wa Tanganyika.
 
Back
Top Bottom