Women after 50 years: ...Good news to both sides...!!

Women after 50 years: ...Good news to both sides...!!

Dark City

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2008
Posts
16,252
Reaction score
11,653
Kwa wale ambao wanakaribia kufikisha umri a miaka 50 au wamepita, watakuwa wameshasikia au wamapitia kwenye kipindi cha msongo wa mawazo juu ya maisha yao na wenzi wao kwa ujumla. Kumekuwa na taarifa kwamba wanawake wanapofikisha umri huo hupata matatizo makubwa ya aina mbali mbali kiasi kwamba hawawezi tena kufurahia maisha...

Hata hivyo, kuna habari kwamba hizo taarifa za wali hazikuwa sahihi kwani wanawake wengi hufurahia maisha wanapofikia umri wa miaka 50 au zaidi...

Soma zaidi hapa,

http://www.dailymail.co.uk/femail/article-2292798/Life-begins-50-Older-women-better-sex-exercise-feel-happier-somethings-survey-reveals.html?ito=feeds-newsxml

Kwa kuwa kukosa furaha kwa wanawake huwa ni tatizo kubwa kwa wenzi wao, kwangu mimi naona huu ni ushindi wa pande zote mbili.

Nawatakia Jpili njema,

Babu DC!!
 
Safi sana,ngoja waje wausome!


Unajua linaweza kuonekana ni jambo dogo, ila kwa wale ambao tuko kwenye timu hiyo...ama tumekaribia au kuvuka, ni jambo la kutia moyo sana.

Mke anapokosa furaha ni tatizo kubwa kwenye ndoa...ukizingatia kuwa hiki ni kipindi ambacho katika familia nyingi watoto wanakuwa tayari ni wakubwa au wameshaanza maisha yao.

Binafsi nimefurahia sana hii kitu...I hate to see Bibi in low mood!



Babu DC!!
 
Kweli babu DC nakubaliana nawe kwa kuwa jambo hili ni la muhimu sana kwa wale wenye umri huo
'
Unajua ili ujue umuhimu wa sindano ni mpaka pale utakapopata malaria
 
twende kiafrika afrika babu,

Maisha ya mama wa kiafrika yanaghubikwa na tabu nyingi sana istoshe pia na uzazi usiokuwa na usimamizi mzuri, nisemapo uzazi namaanisha kwamba pre natal care na hata post natal care. mara nyingi sana utakuta mtu kwenye umri huo wa 50+ wa kike amesha jitakia tamaa kabisa kwasababu hizi hapa.
1) karaha alizopewa na mume toka walipoanza maisha hadi alipofikia.
2)ugumu wa maisha incluiding lishe duni, kazi ngumu kutokupumzika, nishati mbovu nk
3)mazingira hatarish anayoish mama huyu yaani kupikia kuni, kupanda baiskeli pikipiki, kuvuka mito kwa kukanyaga maji, matumizi ya vibatari na kandili etc
4) ugumu wa malezi ya watoto anaoupata mama huyu, muda mwingine anakuwa yy ndo mama na ndio baba, stress anazopewa na watoto, kama vile kulazwa wodini na mtoto nk
5) uzazi wa shida sana, lishe mbaya, risk kubwa wakati wa mimba hadi kujifungua
6) upendo wa dhati toka kwa wakaribu yake hakuna na inaonekana ni haki yake kufanya hayo

sasa mama kama huyu anapaofikia umri wa miaka 40+ hapo ndipo mawazo huanza kumjia akilini kwani unakuta umri wa miaka 35 tu esha choka kabisa hatamaniki kilichomchosha ni hayo hapo juu.
kwasababu ya mawazo ya huko anakoelelkea mama huyu hujikuta akikabiliwa na matatizo ya kushindwa kuwa mlaini ukeni na hili linasabbaishwa na hormones na akili kutotulia. kwasababu ya hali hii hujikuta hataman tena kufanya tendo la ndoa na maisha kuanza kuwa na risk tena.

mbaya zaid babu mama huyu anapofkia umri huu kuna aina ya maisha anatakiwa ayaish ili kupunguza maudhi ya menopouse like aina ya pacage yake ya kuogea na kujipaka, aina za nguo hasa za ndani. aina za matandiko nk. wa wachache sana huweza kuyamudu haya ila wengi hushindwa kuyamudu haya.

wito wangu kwenu waume zetu, tsaidieni manake uwezo wa kuendelea kuwa na furaha ndani ya ndoa mnao nyie hapo. tushaurini, tushirikiane hata kwenda wa wataalam ili tuwee kupatiwa ufumbuzi wa yale yaliyo magumu kwetu.

ukisoma hiyo makala wote waliosema wana enjoy life ni wasababu wamewezeshwa na spouses wao na wao kuamua kwa dhatii kwamba wanataka kufurahia maisha.

kwetu akina mama tusikubali kujiachia yaani tusikubali kujiachia hadi tukachusha. mie japo mzee lkn bado nalipa kama vile 20+ hahahaahahahha!...................na ukikutana na mm nanukia babu sitaki mie baba Klein anisambu.
sikatai nakaribia 40 bado kidogo sana lkn umri wa menopouse haunisumbui kabisa as najua sio threat kwangu tena ndio umri nitakula bata hata mara 5 kwa siku khaaa!
 
Ahsante teacher gfsonwin kwa mchango wako,

Ni muhimu sana na unahitaji muda kuutafakari...

Nitarudi baadaye ngoja nimalize hiki kibarua na wajukuu...

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Naamni kukiwa na good life kiujumla
hadi 60 still ni miaka safi tu ya kuishi
boss usisahau kwamba maisha tunayoish tukiwa vijana ndiyo yatakayo tuchagulia aina ya uzee.
hapa namaanisha kwamba kama mama/baba hawatulii wanajiexpouse kwenye risk behaviours ukadhani watakuwa na uzee mzuri.

nimekulia kijijini nimeona haya, wale wazee ambao ujanani walijipenda sana waajitunza wanaish mpaka leo. wale ambao walidhani life ni kula bata kuisha maisha ya kujiachia manyama ya kuchoma, mapombe makali na bado wakapuliza masumu kwenye kahawa wote wameondoka. ama kwa gauti, ama kansa na visuari na presha.
 
Last edited by a moderator:
boss usisahau kwamba maisha tunayoish tukiwa vijana ndiyo yatakayo tuchagulia aina ya uzee.
hapa namaanisha kwamba kama mama/baba hawatulii wanajiexpouse kwenye risk behaviours ukadhani watakuwa na uzee mzuri.

nimekulia kijijini nimeona haya, wale wazee ambao ujanani walijipenda sana waajitunza wanaish mpaka leo. wale ambao walidhani life ni kula bata kuisha maisha ya kujiachia manyama ya kuchoma, mapombe makali na bado wakapuliza masumu kwenye kahawa wote wameondoka. ama kwa gauti, ama kansa na visuari na presha.


very very true
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom