Wizi wa wahudumu wa kwenye vituo vya kujaza mafuta

jana mbichii... nimeenda petro station. nikamwambia weka elfu 30, basi akaclear number akaandika 3,000... nikamwangalia tu akachomeka mpira wake mafuta yakaanza kutoka akajifanya bize akazunguka upande wa pili... mashine imeshakata yeye anajifanya bize.... akaenda funga kifunik akatoa risiti akaniletea, nikampa 30,000 akapokea na kuniambia karibu tena... akashangaa siondoki nikamwambia bado mafuta yangu hayajakamilika umeweka ya elf tatu.... bila hata kuangalia akajifanya kujichangamsha eti samahani daaa kumbe nimeandika elfu tatu.... dah... nina mawazo.... akakuta nimekunja uso namwangalia tu.... nikafungua tank akaandika 27,000 akajaza yaliyobaki..... nikaondoka bado anajichekesha mie simjibu kitu. Huu ni wizi kuweni waangalifu.

Hatari na nusu.

Kwa hiyo kuna uwezekano pia wa kupewa risiti isiyo ya kwako?
 
Wizi wao kwasasa ni kua na pampu ilio jikunja ndefu mafuta yanabaki kwenye pampu na anarudisha pampu vizuri tu ukiondoka anamimina kwenye dumu dogo la lita tano likija wanauzia bodaboda ndo wizi wao kwa wasasa.

Haya wanafanywa kwenye vituo ambavyo supervision sio nzuri, hao pampu attendants hawakosi 20,000 to 30,000 kwa siku hususani wanao fanya night shift wanahudumia walevi wengi na watu wakusafiri usuku.
Hii nilishapigwa Segera pale kuna kakituo mshenzi😂😂😂 mafuta ya 20K sikufika nayo Mombo yameshakata halafu highway ambako gari inakula vizuri😝😝😝 matusi niliyomtukana yule mshenzi dereva wangu alikuwa anakufa mbavu maana nilisema nijazie tu ili nimalizie safari 😁 gauge ikishuka sana economy inapungua
 
Kuna siku nilimsingizia muhudumu hapo kaniibia mafuta kumbe gauge yangu ina tabia za ajabu. Baadae nikagundua hakuniibia ilibidi siku ingine nirudi nimuombe samahani.
Mimi iliwahi kunitokea,ameweka mafuta gauge yangu haikuamka ikawa inasoma zero,nikamshukia nikawasha moto vibaya kuwa hakuingiza mafuta,yule dada akasema ngoja aingize tena labda pump ina shida,wakati naondoka ilikuwa imenyanyuka kidogo sana,nikawa naondoka huku maneno yananitoka kuwa ni wezi sana wale wahudumu,ilipofika kama km 1 hivi gauge ikapanda mara mbili ya kipimo cha kwanza,nikabakia naona aibu mimi...
 
Hakikisha huwi na haraka wala madoido ufikapo kituo cha kujaza gari mafuta.

Usizubaishwe na uzuri wala story za kuzuga za mhudumu...

Epuka kukodolea macho msambwanda wa mhudumu Miele yako.

Macho yako yote kwenye pump reader hakikisha kabla hujawekewa mafuta isome 0000

Asante sana kwa nondo Boss
 
Hela za kutafuta kihalali hazitoshi. Ukisikia kujiongeza ndiyo huko.

Tatizo ni pale mtu unagundua kwamba pale fulani kanipiga. Wapo wanaojenga kwa pesa za sheli.

Maisha ni kupigana na kupiga ndiyo huko uonavyo
Kaka tatizo sisi tunaozipata kwa kuungua jua na kunyeshewa mvua tuna hasira sana, ingekuwa zinakuja kwa ulaini wala isingekuwa tatizo, ingekuwa ni kugawana neema tu, lakini sasa jinsi tuzipatavyo ni mtihani ndio maana tuna hasira sana!
 
Kwa hesabu za haraka haraka ni kwamba: anaibiwa mwenye kituo cha mafuta kwa sbb yale mafuta yameuzwa bila mashine ya risiti kurekodi, pia anaibiwa mwenye chombo anaewekewa mafuta maana analipia mafuta ambayo hakuwekewa! Hii kwa kifupi inaitwa DOUBLE IMPACT!
Mafuta hayawezi kuuzwa bila mashine ya risiti kurekodi. Ndo mana huwezi hata cku moja kumharibia kazi pump attendant kwa kumchongea kwa manager kwasababu manager anajua anaibiwa ni mteja sio boss
 
Hatari na nusu.

Kwa hiyo kuna uwezekano pia wa kupewa risiti isiyo ya kwako?

ilitoka risiti ya 3,000 lakini wanajua wengi hatunaga muda wa kusoma au hata kuchukuwa hizo risiti. Wanajiaminigi sana... nahisi kwa mtindo huu wengi wanapigwa
 
Yaani ndio hivyo hivyo, na sijui ni nani aliebuni mbinu ya kuweka hawa wahudumu wa jinsi ya kike, maana akijichekesha tu unamsamehe, mimi nimeshikwa sana na hasira asubuhi, nikatamani kumpa walau kelbu mbili aamke, nikawaza jela, nikakumbuka familia yangu nikajikuta narudisha moyo nyuma!

Na ukifika anakupokea kwa tabasamu na masalamu ya kukuzuga! Ukishaondoka huko mbele ya safari hata ukigundua umeibiwa inakuwa ngumu sana kwako kurudi kuanzisha ligi!!! Cha kuzingatia ukiingia pale angalia kilichokupeleka na utagundua janja janja zao
 
Hii style nimepigwa jana Bp ya Sinza super star .....pia ilitoka bodaboda nikafatia mm bahati mbaya sikuangalia.Nimekuja kugundua leo asubuh.Ipo cku yake atakanyaga waya...atajuta siku hyo.

Sent from my Infinix X571 using JamiiForums mobile app
 
Huwa wanaitegesha tu ukija wanakupa maneno mazuri na porojo ukizubaa wanaliunga zipo sana hizo.
... how possible is this? Kwa sababu, unless ulimkuta ile handle kaishikilia mkononi, ila ikisharudishwa mahali pake na kunyanyuliwa tena automatically ina-clear digits zote to zero. Yaani anawezaje kuanzia kiwango tofauti na zero? Naomba kuelimishwa.
 
Huwa wanaitegesha tu ukija wanakupa maneno mazuri na porojo ukizubaa wanaliunga zipo sana hizo.
... nikiingia sheli macho breki ya kwanza kwenye meter reading; nakuwa interested sana kujua aliyetangulia kanunua lita ngapi (sijui kwanini). Then nashusha kioo huwa salamu zao siitikiagi natoa order ya kiasi nachohitaji na kwa kutaja kabisa aina ya mafuta (mf. weka petroli ya elfu 30) huku macho yamekomalia kwenye reading na kuhakikisha ananyanyua handle sahihi (petro vs diesel); meter imeanzia 0000 na kaingiza kiasi sahihi.

Ukihangaika na mawigi sijui misambwanda uko kwenye mazingira hatarishi ya kuibiwa.
 
Hujui kitu nyamaza
Hivi ni Umeandika bila kujua unachoandika na sijui hujui kweli au unafanya makusudi kupotosha ili uchangamshe jukwaa..

Wizi unaosema haupo na hakuna namna yoyote uneweza ukaibiwa Kwa staili hiyo uliyoileta .mkono wa pampu ukirudishwa kwenye mashine wakati wa kutoa unaanza zero mpaka bei uliyoset au utakapoishia

Kuibiwa ni kama ataendelea kupima bila kurudishwa mkono kwenye mashine tena ikiwa mwanzoni hakuset bei wakati anampimia mteja wa kwanza
.
 
Hizo Petrol Station za ajabu ajabu huwa sijazagi mafuta labda itokee gari imenizimikia karibu na hizo sheli. Kwa sasa sheli za uhakika ni Oryx na Total zimekaa ki proffessional zaidi ila kwengine ambako napaamini ni Lake Oil!
Mie Moro huwa najazia TOTAL pale Msamvu, hakuna janja janja kabisa...
 
Back
Top Bottom