Elections 2010 Wizi wa Kura unafanyika hivi...

heko mkuu, jamvini tusiishie kuisoma na kuikumbatia tutakuwa hatujafanya kitu. Tuma hata kwa marafiki kwa njia yeyote ile kuna watu hawapati hizi habari kabisa tena wana kiu zaidi yetu lakini wamefungiwa kila kitu (Landlocked) hawaana access ya information zaidi ya redio mchwara na ccm.
 
Habari za kitetesi zilizosema kwamba makaratasi ya kupigia kura hayakutengenezwa UK kama ilivyoelezwa mwanzoni bali ni hapo Bondeni si za kupuuzwa.

Habari hizo zilieleza kuwa ile karatasi kama ukipiga kwa slaa ukishaikunja inahamia kwa upande wa JK, zinahitaji utafiti kwa wale wote tutakaopiga kura.

Ninaomba baada ya kupiga kura yako na kuikunja, IFUNGUE TENA UONE KAMA KUNA KITU KIMEBADILIKA NDANI KABLA YA KUTUMBUKIZA KWENYE BOKSI

WANANCHI INABIDI WAJIPANGE KUPINGANA NA KILA MBINU CHAFU ZA WIZI WA KURA MAANA TAFITI KAMA ZA REDET ZICHUKULIWE KAMA NI WITO WA KUWA MAKINI JUU YA CCM WALICHOPANGA KUFANYA.

KAMA CCM WAMEJITOKEZA WAZI KUSEMA KUWA NAO WANAJUA WATASHINDA ZAIDI YA HAPO, WAKATI HALI HALISI HAIONYESHI HIVYO, NI WAZI KWAMBA WAMEJIPANGA KUFANYA WIZI WA KURA.

HATA HIVYO HATUA YA NEC KUTANGAZA MATOKEO YA URAISI KWANZA KABLA YA MENGINE NI NZURI LAKINI PIA INABIDI KUPOKELEWA KWA UMAKINI, MAANA WAMESEMA WATAPOKEA MATOKEA KWA NJIA YA MTANDAO..

NATOA WITO KWA VYAMA VYA UPINZANI, HASA CHADEMA WAWE NA INDEPENDENT COMMITTEE YA KUSHUGHULIKIA MATOKEO YA UCHAGUZI AMBAPO WAKALA WAO WAWATUMIE KWA NJIA YA SIMU MARA MOJA MATOKEO YATAKAPOKUWA TAYARI KILA KITUO ILI WAWEZE NAO KUWA NA MAJUMLISHO YAO BILA KUTEGEMEA NEC WAJIFANYIE KILA KITU.

TUNAHITAJI KUELEWA KUWA KUELEKEA DEMOKRASIA HALISI NI VITA, NA TUNAHITAJI KUPIGANA KIROHO, KIMWILI NA KIAKILI
 
Inategemea na namna ya upigaji. Kama ni ule utaratibu wa kuweka alama ya 'tiki' mawakala watashitukia kwa sababu ukishakunja ile alama itakuwa tiki iliyogeuka ambayo definition yake ni sawa na 'kosa'.

Anyway, ni muhimu kuchukua kila tahadhari.
 
MFUMUKO WA KURA ZA MAONI ULIOTOKEA KATIKA VYOMBO VYA HABARI HIVI KARIBUNI Redet, SYNOVATE NA VYOMBO VYA ULINZI POLISI NA JWTZ UNAZUA MASWALI ZAIDI YA MAJIBU KWA MTU YOYOTE MWENYE AKILI TIMAMU ATAGUNDUA HAPA YA KUA CCM INAJARIBU KUWAANDA WANANCHI KISAIKOLOJIA KATIKA WIZI WA KURA KWANU WAMEFAHAMU YA KUA WANANCHI SASA HAWADANGANYIKI.

ILI KUHEPUSHA UMWAGAJI WA DAMU BAADA YA KUIBA KULA WAMEAANZA KUWAANDA WANANCHI KISAIKOLOJIA KWA HIZO KURA ZA MAONI ZA KUPIKWA.

TUNAFATILIA KAMPENI, MIDAHALO N.K TUNAONA NGUVU ZA WAPINZANI.KWA CCM PAOJA NA BURUDANI NA AHADI HEWA BADO WANAPWAYA.

WANANCHI SITUDANAGANYIKE MPAKA KIELEWEKE MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Lakini wakumbuke kuwa matokeo yote (rais, bunge na diwani) yatajulikana na kutangazwa na tume ya uchaguzi jimbo, hapo watanzania tumesogezewa huduma karibu na mtaani kwetu.Tuhakikishe tunalinda kwa juhudi zote.Mianya ya wizi imepunguzwa na nguvu ya wafadhili (Hongera UNDP)kushinikiza yatangazwe jimboni.NEC Taifa kazi yao ni ndogo sana ya kujumlisha na kupata jumla kuu ya kura za rais.

Kazi iliyopo mbele yetu ni kulinda kura tu jimboni JE HII ITATUSHINDA????????????JAMANI .KAMA NI KUKESHA KITUONI TUKESHE WAKE ZETU WATULETEE CHAKULA KITUONI HADI KIELEWEKE.
 
Mara nyingi kumekuwapo na vitendo vya wizi wa kura. Wana JF, tupeane mikakati ya kudhibiti wizi huo; mimi naanza:

Kwa kuwa kila karatasi ya kupigia kura huwa ina namba, na kwa kuwa kila msimamizi wa kituo hukabidhiwa vitabu hivyo kwa namba; yafuatayo yafanyike

1)Kila chama kipate nakala ya namba za vitabu vya kupigia kura vilivyopelekwa kila kituo
2)Mawakala waelekezwe kunukuu namba za vitabu kwenye kituo kabla upigaji kura haujaanza na msimamizi awadhibitishie kuwa hivyo ndivyo vitabu alivyopokea toka msimamzi wa jimbo
3) Iwe ni lazima kwa kila wakala kusaini fomu ya matokeo kituoni na kama ana malalamiko yoyote yale ajaze kwenye fomu ya malalamiko (unajua mkiachia wa CCM pekee akasaini, hata ikijabadilishwa anatafutwa huyo mmoja anasaini na mchezo unakuwa umeisha)
4) Wakati wa kuhesabu kura, iwe vituoni au wakati wa kuhakiki katika ngazi ya jimbo (ambako huwa ndipo matokeo huwa yameshachakachuliwa), kila sanduku la kura lihesabiwe peke yake na ihakikishwe kuwa namba za karatasi zilizozomo zinaoana na namba alizokuwa amekabidhiwa msimamizi wa kituo na mawakala wawe wametoa taarifa kwa vyama vyao juu ya namba zilizotumika kwenye vituo vyao.
5) Kwa kuwa mawakala ndio wameaminiwa na vyama vyao, wayasindikize masanduku ya kura hadi jimboni pale uhakiki na utangazaji unapofanyikia. Kuyasindikiza hadi kwenye kata na kuishia hapo hutoa mwanya kwa watendaji wa kata kushirikiana na CCM kuyabadili. Sanduku lolote litakalowasilishwa bila mawakala litengwe na lihasabiwe tofauti na kama litakuwa na kura tofauti na fomu za mawakala, likataliwe - Nakumbuka hii ilifanyika Temeke wakati Mrema akigombea. Ni marufuku mawakala kusafiri tofauti na masanduku yao - magari yabebe masanduku kidogo na mawakala.

Huo ni mchango wangu - ongezeeni kabla ya uchaguzi

Nilikuwa sina mawasiliano kwani satcom ambao ndio nawatumia walikuwa wanafanya marekebisho, sasa niko hewani
 
Nimesubiri sana kusikia k utoka kwenu mnipe ushauri kama nilivyoomba lakini sijasikia chochote kutoka kwenu zaidi ya kuombwa tu nakala. Sasa nisaidieni niweze kuattach hii video hapa.
 
Mimi sijui cha kufanya ningeshakusaidia. Lakini polepole watatokea wanaoelewa wakusaidie mkuu. Ubarikiwe na Mungu wangu.
 
Nitaifanyia kazi, mimi ni mtaalamu na nina software kadhaa za kuicompress, muhimu tutaiweka katika sehemu mbili (2 parts) kisha tunaiweka kwenye utube na link kuwa hapa kila mmoja aione. Tutawasiliana zaidi
 
Tuma e-mail kwa Invisible, may he could help!! Ubarikiwe kaka. Yaonyesha dhamira ya kweli.
 
Nimesubiri sana kusikia k utoka kwenu mnipe ushauri kama nilivyoomba lakini sijasikia chochote kutoka kwenu zaidi ya kuombwa tu nakala. Sasa nisaidieni niweze kuattach hii video hapa.

Nitaifanyia kazi, mimi ni mtaalamu na nina software kadhaa za kuicompress, muhimu tutaiweka katika sehemu mbili (2 parts) kisha tunaiweka kwenye utube na link kuwa hapa kila mmoja aione. Tutawasiliana zaidi

Mkuu nadhani Invisible amesikia hilo na Wa Ndima anahangaika nalo.
 
Nimeongea na Kamende nimuone Mnyika kwa ajili ya kuiupload kwenye utube, mimi niko Kunduchi, mwenye hiyo DVD kwa sasa anitaarifu kwa PM tafadhali kesho mchana link iwe hapa pls!
 
Nimeisoma na kuikiubali hii thread ya Kamembe, ila mara nyingi wizi mkubwa hufanyika wakati wa kusafirisha masanduku:
Kinachofanyika huwa ni kubadilisha kura ndani ya masanduku na kuyajaza za ccm, halafu fomu alizotaja Kamembe zinabadilishwa. Ni wazi kuwa fomu zilizobadilishwa hazitakuwa na saini za mawakala wengine isipokuwa wa ccm ambaye anahusika moja kwa moja na ubadilishaji huo. Mnapofika kwenye jimbo wakati wa majumisho na kuhakiki, utaona matokeo katika fomu ya wakala wa chama cha upinzani (CHADEMA) ni tofauti na yanayotajwa na msimamizi! Hapo patatokea malalamiko, fomu ya wakala wa ccm itasema sawa na msimamizi alivyosoma, lakini ya CHADEMA tofauti - ubishi huo utapelekea kuhakiki physically kilichomo ndani ya sanduku; hapo ndipo utakuta viroja -kura zimeshabadilishwa ndani ya sanduku, utakuwa huna ujanja tena maana sanduku ndiye msemakweli!
Ndiyo maana mimi nikapendekeza wakala kunukuu namba za karatasi za kupigia kura ili wakati wowote namba hizo hizo ndizo ziwemo ndani ya sanduku- period
Hii itafanya wizi uwe mgumu kwani itabidi wawe na karatasi zenye kufanana namba, na wawe wamepredict vituo watakavyoshindwa.
Pili nikasema wakala aandamane na sanduku lake hadi mwisho wa safari kwa msimamizi wa jimbo na si kwa mtendaji wa kata.
Mkakati narudia tena hapa:(unganisha na elimu nzuri ya Kamembe)
Kwa kuwa kila karatasi ya kupigia kura huwa ina namba, na kwa kuwa kila msimamizi wa kituo hukabidhiwa vitabu hivyo kwa namba; yafuatayo yafanyike

1)Kila chama kipate nakala ya namba za vitabu vya kupigia kura vilivyopelekwa kila kituo
2)Mawakala waelekezwe kunukuu namba za vitabu kwenye kituo kabla upigaji kura haujaanza na msimamizi awadhibitishie kuwa hivyo ndivyo vitabu alivyopokea toka msimamzi wa jimbo
3) Iwe ni lazima kwa kila wakala kusaini fomu ya matokeo kituoni na kama ana malalamiko yoyote yale ajaze kwenye fomu ya malalamiko (unajua mkiachia wa CCM pekee akasaini, hata ikijabadilishwa anatafutwa huyo mmoja anasaini na mchezo unakuwa umeisha)
4) Wakati wa kuhesabu kura, iwe vituoni au wakati wa kuhakiki katika ngazi ya jimbo (ambako huwa ndipo matokeo huwa yameshachakachuliwa), kila sanduku la kura lihesabiwe peke yake na ihakikishwe kuwa namba za karatasi zilizozomo zinaoana na namba alizokuwa amekabidhiwa msimamizi wa kituo na mawakala wawe wametoa taarifa kwa vyama vyao juu ya namba zilizotumika kwenye vituo vyao.
5) Kwa kuwa mawakala ndio wameaminiwa na vyama vyao, wayasindikize masanduku ya kura hadi jimboni pale uhakiki na utangazaji unapofanyikia. Kuyasindikiza hadi kwenye kata na kuishia hapo hutoa mwanya kwa watendaji wa kata kushirikiana na CCM kuyabadili. Sanduku lolote litakalowasilishwa bila mawakala litengwe na lihasabiwe tofauti na kama litakuwa na kura tofauti na fomu za mawakala, likataliwe - Nakumbuka hii ilifanyika Temeke wakati Mrema akigombea. Ni marufuku mawakala kusafiri tofauti na masanduku yao - magari yabebe masanduku kidogo na mawakala.
 
Je vipi utaratibu wa TUME, inarushusiwa wakala kusafiri na sanduku? Isije ikawa wana maelekezo kuwa mawakala HWARUHUSIWI kusafiri na masanduku!!!

Hioyo itakuwa shida kaka!!!
 
Mimi DVD hii nimeshapata na kuwatumia Chadema kata nilikozaliwa,

Nasikia mbinu za CCM kuiba kura ni pamoja na
1. Kusababisha vurugu na wanawaita police ilikuwahoji mawakala , watawaitapeleka mawakala pembeni kwa mahojiano hapo ndipo CCM hupenyeza masanduku ya kura za CCM

2. Mbinu nyingine nikuwapandisha wana CCM kwenye silinbodi kama chumba ina silingbodi. Hii hufanyika mapema kabla mawakala hawajafika kituoni. Wakati wa chakula wasimamizi watawaamuru mawakala kula chakula nje ya chumba na funguo atapewa wakala mojawapo wa vyama vya upinzani ilikuwaaminisha kuwa hakuna kinachoharibika. Walioko kwenye silingbodi watashuka nakubadilisha masanduku.
 
Mkuu Invisible je hujapata namna ya kushughulikia hii video hadi leo?
Ninajiridhisha kuwa utatu wa Mnyika Wa Ndima na Invisible unaweza kutusaidia tupate hii video humu jamvini.

Hata hivyo na mimi mwenyewe nimeamua kutafuta namna ya kuiconvert into VCD ya kama MB 300 hivi. Nikifanikiwa nitakuja tena kwenu kwa maelekezo.

Mungu awabariki sana!!!
 
WanaJF naomba mnifowardie iyo Documentary ili nifikishe bukoba kwa wahusika. Plz tuwasiliane kwa kutumia ada32010@gmail.com ntashukuru sana wakuu. Kamende, long Life brother!!
 
Kama una hiyo DVD jiunge na skype kisha mtafute mwanacha mwingine ambaye naye yuko kwenye skype. Mnapokuwa wote mko kwenye skype unaweza ukamtumia mwenzako dvd ya ukubwa wowote itachukua muda lakini bado itafika kama ilivyo. Hivyo utakapokuwa umeingia skype unaweza kutoa address yako ya skype tutakutafuta na utatuma kwa njia hiyo.
Tutakuelekeza namna ya kutuma hapo kwenye skype.
 
Nimefurahi sana imebidi nikusaidie hata kwa kutumia Computer ya mpendwa yenye kuweza kugeuza file la Microsoft kuwa PDF. Kama unaweza tumia sasa file hili kwani mtu hawezi kurekebisha lolote katika file hili la pdf.
 
Attachments

  • MAJUKUMU YA WAKALA.pdf
    84.4 KB · Views: 95
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom