NguchiroTheElde
Member
- Jun 13, 2010
- 22
- 1
Wizi wa kura unaanza na Tume ya Uchaguzi inapotangaza idadi ya wapiga kura waliosajiliwa. Katika idadi hii kunakuwa na pasenti kubwa ya WAPIGA KURA HEWA. Hawa wapiga kura hewa watatumika kujaza mapengo pale mgombea wa CCM atakapoonekana kuelemewa.
Ili kutumia hizi kura feki wanakuwa pia na VITUO VYA KUPIGA KURA FEKI ambavyo vinakuwa na masanduku ya kupiga kura kama yaliyoko kwenye vituo vya kweli.
Hizi kura zinapigwa kisirisiri largely na usalama wa taifa na kuwekwa kwenye haya masanduku ya vituo hewa siku kadhaa kabla ya uchaguzi.
Mawakala wa uchaguzi wanasimamia kura katika vituo halali tu na hivyo vingine vilivyo feki of course hawana habari navyo. Kwa hiyo matokeo ya kura wanayoyafahamu mawakala ni yale ya vituo waliko tu na hata haya yanaweza kukumbwa na matatizo ya
(i) orodha ya wapiga kura kuwa na majina kibao ya wapiga kura hewa na watu kuandaliwa kuja kupiga kura kwa niaba ya hayo majina bandia,
(ii) kura zao kuweko kwenye masanduku kabla ya kupiga kura au
(iii) watu walioandaliwa kutumbukiza bulunguti la kura kwenye sanduku.
Kura kadhaa zimeshapatikana kwenye masanduku zikiwa zimeshikamana kwa njia ambayo ni wazi kuwa zimetumbukizwa na mtu mmoja. Tatizo hili laweza kupunguzwa, ijapokuwa siyo kumalizwa, kwa kutumia masanduku yalio transparent lakini nasikia masanduku hayatakuwa hivyo.
Tume ya uchaguzi ndiyo inayoruhusu haya yote yatokee na ndiyo inayojumlisha kura na kutangaza matokeo na jinsi sheria ya uchaguzi ilivyoandikwa ni wazi kuwa waliyoitayarisha hiyo sheria walikuwa na dhamira ya kuwezesha wizi wa kura na kutumia Tume kuhalalisha wizi huo.
Kutumia wakurugenzi wa Halmashauri kama wasimamizi wa uchaguzi majimboni ni nyenzo kubwa ya kufanikisha haya kwani wakurugenzi wote wanateuliwa na Rais directly au indirectly na Waziri wa TAMISEMI na you can be sure that they are all loyal members of CCM. Mambo mengine kama kuwarubuni mawakala wa vyama vingine au kuwahonga wagombea wajitoe dakika za mwisho ni mwendelezo tu wa msingi huu wa kuwaibia wananchi haki yao ya kuchagua viongozi wao.
Kwa jinsi sheria ya uchaguzi ilivyoandikwa, Tume ya Uchaguzi inaweza kumtangaza mgombea ambaye actually amepata kura chache kuwa mshindi na kutoa namba tu zanazodai kuwa huyu kashinda kwa kura nyingi ijapokuwa si hivyo.
Wizi wa kura uliofanyika Iran na Afganistan kwenye chaguzi zao za mwisho ni mifano mizuri ya kuwafumbua macho Watanzania kuhusu tatizo hili.

Huwezi kuiba hela uache kuiba kura, and vice versa!