Wizi wa Kura Kawe wasababisha maandamno | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizi wa Kura Kawe wasababisha maandamno

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Gold Digger, Aug 3, 2010.

 1. Gold Digger

  Gold Digger Member

  #1
  Aug 3, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kura zimejitokeza 1,000 eneo la msitu wa Mabwepande.

  Wanachama wa CCM wakiwepo baadhi wa wagombea wamepanga kuandamana leo baada ys kura karivia 1,000 kujitokezaeneo la msituni wa Mabwepande. Uwezekano wa idadi hiyo ya kura kutoka eneo la msituni, ambalo ni eneo dogo ndicho chanzo cha ugomvi. Msitu wa Mabwepande unakuwa na washiriki na wanachama wengi kuliko eneo la mjini na makazi ya wengi kama vile tegeta?:drama:

  Kura hizo zilikuwa hazipo katika matokeo ya uchaguzi mpaka ghafla, j3 saa 7 Mchana.

  Mawakala Wa wagombea wote kumi na tano wamekataa na kushangazwa na matokeo hayo. Kura hizo za Angela Kizigah zimewastaajabisha wagombea wenza hasa kwa kuwa alishakubali kushindwa na walikuwa wote wameshampongeza mshindi halali Kippi Warioba.

  kura hizo 1,000 zimejitokeza nyumbani kwa katibu kata Wa chama, nd Mohammed Mbetu ambae ni campaign manager Wa Angela Kizigha. Uchaguzi na matokea ya Jimbo la Kawe yako chini Agatone Mwingira, na huyo huyo Mohammed Mbetu, ambao wote wawili walijiweka wazi katika kuendesha campaign ya Angela.
   
 2. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  tupe chanzo habari hii haijakaa sawa
   
 3. Gold Digger

  Gold Digger Member

  #3
  Aug 3, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanachama wa CCM,
  Jimbo la Kawe,
  Dar Es Salaam.
  2 Agosti, 2010


  MKURUGENZI WA UCHAGUZI,
  WILAYA YA KINONDONI,
  MKOA WA DAR ES SALAAM


  YAH: MABADILIKO YA KURA NAFASI YA UBUNGE, JIMBO LA KAWE.

  Tafadhali husika na kichwa cha habari.

  Sisi wanachama wa CCM Jimbo la Kawe, kwanza tungependa kukipongeza Chama kwa maamuzi ya kurejesha upigaji kura za maoni kwa wanachama.

  Lakini tumesikitishwa kwa mambo yaliyotokea yafuatayo:

  Hadi kufika tarehe 1 Agosti, 2010 Usiku, na Hata tarehe 2 Agosti Asubuhi wakati tunamsindikiza Rais wetu kuchukua fomu, tulishapata matokeo ya vituo vya Matawi vyote. Wengine wagombea wetu walianguka, na wengine walipeta sehemu mbali mbali lakini tuliridhishwa na hali ya demokrasia.

  Kufika leo mchana saa 7, matokeo yote yalishawasilishwa wilayani kasoro tu, yale ya Mabwepande ambayo yalikuwa bado kuwasilishwa wilayani. Cha kushangaza ni hili
  1. Matokeo ya kata hii moja kuchelewa sana kufika.
  2. Kujitokeza na mahudhurio makubwa sana ya wanachama (kwa asilimia 47%), tofauti na
  utaratibu wa matawi ya Dar Es salaam,ukilinganisha na idadi ya wanachama. Kwa Mfano:
  KATA IDADI YA WANACHAMA ASILIMIA YA MAHUDHURIO
  Mabwepande 2,080 47%
  Bunju 3,510 33%
  Makongo, Kawe, Mbezi Juu 9,526 14%
  Mbweni 2,320 27%
  Msasani 2,822 21%
  Mikocheni 4,056 22%

  Jionee jinsi Mabwepande pamoja na kwamba kwenye mikutano ya Kampeni hakuna Tawi ambalo mahudhurio yalizidi wanachama 60, lakini si tu kura zilipigwa nyingi, bali mahudhurio yametia for a.
  3. Matokeo ya Udiwani.

  Je Matokeo ya MabwePande waliyacheleweshwa wakijua wazi ni eneo la shamba/msitu kwamba wanachama hatutajua ukweli?

  Tunaomba haki itendeke na kura zetu zituchagulie kiongozi. Aidha kura zirudiwe za Mabwepande, Kura za Mabwepande zifutwe, au zigawiwe kwa ailimia ya mahudhurio ama kwa asilimia walizozipata wagombea kwenye jumla ya kata zote tisa.

  Tuteendeeni Haki!

  WANACHAMA HAI WA CCM
  JIMBO LA KAWE'
  DAR ES SALAAM


  Nakala Kwa:-
  Mwenyekiti CCM Taifa - Mh. Jakaya Mrisho Kikwete
  Katibu CCM Mkoa
  Katibu Mkuu CCM
   
 4. Gold Digger

  Gold Digger Member

  #4
  Aug 3, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari hii imeripotiwa na ITV, Radio One na Clids FM leo asubuhi
   
 5. M

  MathewMssw Member

  #5
  Aug 3, 2010
  Joined: Mar 27, 2009
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kazi kwenu!
   
 6. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #6
  Aug 3, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hiyo ndiyo TRUE IMAGE ya kinachofanywa na CCM kwenye chaguzi nyingi hapa nchini 100 + 100 = 1000.
   
 7. Kamaka

  Kamaka JF-Expert Member

  #7
  Aug 3, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 565
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tokeni huko ..........NJOONI HUKU.
   
 8. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #8
  Aug 3, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  Kippi kishalizwa kwenye hizi kura... Sad indeed
   
 9. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #9
  Aug 3, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Wow! Lichama dume hilo..!!
  Kumbe ni u-dume wa wizi wa kura..
   
 10. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #10
  Aug 3, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,582
  Likes Received: 4,692
  Trophy Points: 280
  CCM ni chama cha kishetani, cha kijambazi , cha kifisadi, cha kimafia hakuna lolote jema linaloweza kupatikana toka huko. Nashukuru Mungu kwa matokeo ya kura za maoni kwani yamewaonyesha watz kuwa CCM ni genge la majambazi tu, ubaya ubaya tu. Hivi wabongo wanataka Mungu awaonyesheje ubaya wa mijitu hii? Tuwapige chini ili Taifa letu lipone.
   
 11. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #11
  Aug 3, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Go Kippi go...aleyaleyale!
   
 12. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #12
  Aug 3, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kimchezo kama hiki kimemliza Mwakalinga huko Kyela. Wiki moja kabla ya UCHAGUZI wapambe walishafahamu kuwa WATASHINDWA vibaya sana. Rafu zilipangwa na zikawa zinachezwa waziwazi. Nilimuonya Mtani wangu aingie CHADEMA walau huko ataweza kutetewa mana CCM ina wenyewe. Na wenyewe hao kama KEIL na PASCO walivyosema, "....CCM itahakikisha WAPIGANAJI wanarudi mjengoni kwa hali na mali ili wasipige makelele na kumwaga siri nzito za RIchmonduli na mengineyo."

  Ila kwa kutumia mbinu chafu kuingilia MJENGONI, mbunge wenu huyo ndiyo kashajiondolea MENO yake bungeni. Atakuwa Mpole kama kondoo kwani CCM wana machafu yake yoote na wanaweza hata kumshtaki kwa kutumia TAKURURU huku wakijifanya kuwa wamepata hizo data hivi karibuni. Ni kama yule mwenyekiti wa Umoja wa vijana-CCM ambaye walimuondoa kwa sababu ALIDANGANYA MIAKA.

  Kweli hiki chama cha Mafia. Wanakupa kazi huku wamekushika PABAYA. Ukiropoka tu...........................
   
 13. Gold Digger

  Gold Digger Member

  #13
  Aug 3, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katibu kata wa chama (CCM), Ndugu Mohammed Mbetu, ametoweka hapatikani nyumbani wala ofisini
   
 14. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #14
  Aug 3, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  thieves
   
 15. K

  KIKO New Member

  #15
  Aug 3, 2010
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  dhaaa sasa haya mambo mbona yanatisha?
   
 16. whizkid

  whizkid JF-Expert Member

  #16
  Aug 3, 2010
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 299
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 60
  Duh, ulisikiliza radio na kuangalia TV ukaweza kuiandika barua yote hii? Au wewe ni muhusika/mwanachama wa Kawe? Ingependeza zaidi kama ukituandikia link yoyote kama ipo ya source ya barua hii.
   
 17. Gold Digger

  Gold Digger Member

  #17
  Aug 3, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Barua nimepatiwa kama mwaandishi wa habari, lakini habari ya kwanza nimekariri na taarifa iliyosomwa na Paul James kwenye kipindi cha power breakfast. Taarifa ya ITV ilikuwa fupi ni hivi punde tumetoka kwenye ofisi ya CCM wilaya ya kinondoni, mkwajuni ambapo wanachama wa CCM (takriban 170) wamekusanyika kulalamikia hizo kura za kawe. Hamna gazeti lilochapisha habari hizi kwani zimetokea jana usiku...lakini hakikisha unaangalia taarifa za habari za leo mchana
   
 18. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #18
  Aug 3, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Watakuja huku tu..... maana Dr Slaa kesha anza kuwachota wengi tu. Hujasikia jana JK na Makamba wanaweweseka ovyo -- wanajihami kabla kwa makombora mazito. Wameanza kumjibu Dr Slaa hata kabla tuhuma zao hajaanza kuzisema majukwaani. Jee pale akianza kuzisema? Na analo rundo la makabrasha ushahidi. Twajua tu watakimbilia kusema "matusi hayo!"
   
 19. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #19
  Aug 3, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,865
  Trophy Points: 280
  Kama wenyewe kwa wenyewe mnaibiana ndani ya nyumba yenu, jirani yako atasalimika na huyo mwizi mzoefu? Nashukuru sana mbinu zao za wizi zimekuwa wazi sana kipindi hiki, hii ni habari nzuri kwa sasa jirani hata lala ili kupambana na wezi hao.
   
 20. mamsindo

  mamsindo Member

  #20
  Aug 3, 2010
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 28
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 5
  CCM inadhihirisha jinsi ilivyo na mafisadi.Kama mgombea ana uwezo wa kuongoza kwanini atumie rushwa katika kutafuta ushindi?Na sisi wananchi kwanini tukubali "kuuza haki zetu"?Nadhani kwa kujiosha CCM inabidi ifute matokeo ya wale wote ambao watathibitika kujihusisha na rushwa.Wagombea wote waliahidi kuikubali na kuifuata sheria ya uchaguzi ya mwaka 2010 hivyo wale wote waliokiuka wachukuliwe hatua za kisheria.
   
Loading...