Wizi wa Buguruni kwa Wajenzi

Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
5,149
4,674
Ni vizuri kupeana uzoefu hata kama ni mdogo hasa kwa mambo mabaya yanayoendelea ktk jamii yetu. Mpendwa kama unakwenda kununua mbao a.k.a treated timber hasa Buguruni na kwingineko weka akili sawa. Kuna wizi kiasi cha kukatisha tamaa. Ukiweza nenda na futi kamba yako,na ikibidi hata calculator,futi zinapopimwa na kusomwa na wewe andika,maeneo wanayopenda kuwaliza watu ni haya yafuatayo.

Moja, watakwambia mita moja(kwa sasa) ni Tsh 1600/ kwa hiyo kwa hesabu za haraka utasema futi ni 1600/3 badala ya Tsh 1600/3.3 kwa hiyo kama ni mbao nyingi hiyo 0.3 ni hela nyingi sana umeibiwa.

pili, zile futi zao wamekata pale ktkt kipande cha kati ya futi moja mpaka mbili na kukiondoa, kama hujashituka kila ubao (one pc) utakuwa umeibiwa hizo futi. Ukifika wanakupa futi kagua, kisha watazunguka zunguka mpaka wakubadirishie futi.

Tatu, wanapotaja futi na point zake,wanaongeza ktk kuandika zile point,kama huandiki wewe,basi utaibiwa hadi basi.

Nne, eneo la kujumlisha ni hatari pia, watakupeleka speed kwa lengo maalum.

Kwa upande wa mabati, kuna wahuni wanachanganya gauges, juu wanaweka 30 na ndani wanaweka 32.

Kama unataka kununua vifaa hivyo, basi usiwe na haraka kabisa.
 
Ukitaka mbao za dawa kabisa nenda pale sao hill wana mbao nzuri za dawa au mtafute agent wao mbezi beach Enea hardware simu 0784207307
 
duh, najihisi kutafuta mume wa kunisaidia mambo haya, maana hadi nyumba yangu inaisha ntakuwa nimenyonywa mpaka basi.
 
Asante mkuu kwa taarifa.nilishajiuliza sana kwa nini mibongo inapenda utapelitapeli tu sipati jibu
 
Na kama unanunua mabati yanayoitwa ya kiwandani, label wanaweka 30G lakini utakuta ni 32G
Wabongo uchakachuaji kila mahala!
 
Kwa Dar es Salaam ukiona mtu amejenga nyumba amemaliza, fahamu kuwa 40% ya expenditure aliibiwa na Hardware Suppliers & Mafundi Ujenzi! Wao wanasema wakale wapi!!!!
 
Mimi nilikwishalizwa kwa kununua bundle 3 za bati, tena zilizofungwa kabisa kwa core, lakini bati chache tu za juu na chini zilikuwa za geji sahihi. Na hiyo ilikuwa Mabatini Mbeya - bila shaka Dar ndio zaidi.
 
Je umewahi kununua saruji yenye uzito pungufu? Hata kilo moja ya misumari wanaiba. Kuna jamaa kila nondo inayofika kwao wanakula ft nne, kwa hiyo ukinunua kwa pcs bila kupima,unapoteza ft 4 au 3 hivi kwa kila nondo.

Nilikwenda soko la dunia pale, jamaa kaniambia kuna nondo za Tsh 14,000/ mm 12 na Tsh 16500/ za mm 12. Nikamuuliza inakuwaje, jamaa kaniambia wao wakale wapi? Kwa hiyo zile ft 4 wanazokula ndio wanawauzia jamaa wa madirisha. Hiyo ni bongo zaidi ya uijuavyo. Kwa hiyo wakiona wewe mshamba fulani hivi, wanakuuzia nondo zenye urefu pungufu.
 
Ni vizuri kupeana uzoefu hata kama ni mdogo hasa kwa mambo mabaya yanayoendelea ktk jamii yetu. Mpendwa kama unakwenda kununua mbao a.k.a treated timber hasa Buguruni na kwingineko weka akili sawa. Kuna wizi kiasi cha kukatisha tamaa. Ukiweza nenda na futi kamba yako,na ikibidi hata calculator,futi zinapopimwa na kusomwa na wewe andika,maeneo wanayopenda kuwaliza watu ni haya yafuatayo.

Moja, watakwambia mita moja(kwa sasa) ni Tsh 1600/ kwa hiyo kwa hesabu za haraka utasema futi ni 1600/3 badala ya Tsh 1600/3.3 kwa hiyo kama ni mbao nyingi hiyo 0.3 ni hela nyingi sana umeibiwa.

pili, zile futi zao wamekata pale ktkt kipande cha kati ya futi moja mpaka mbili na kukiondoa, kama hujashituka kila ubao (one pc) utakuwa umeibiwa hizo futi. Ukifika wanakupa futi kagua, kisha watazunguka zunguka mpaka wakubadirishie futi.

Tatu, wanapotaja futi na point zake,wanaongeza ktk kuandika zile point,kama huandiki wewe,basi utaibiwa hadi basi.

Nne, eneo la kujumlisha ni hatari pia, watakupeleka speed kwa lengo maalum.

Kwa upande wa mabati, kuna wahuni wanachanganya gauges, juu wanaweka 30 na ndani wanaweka 32.

Kama unataka kununua vifaa hivyo, basi usiwe na haraka kabisa.

Mkulu.. wamekuchekecha na uzoefu wako wote...?:evil:
 
Nimekoswa koswa kwa ncha ya sindano, ile nafika tu,nakuta kisanga cha kufa mtu, mjeshi mmoja karudi na mbao zote na wajuba na fundi wake. Palikuwa padogo mkuu. Kingine ninachofanya mara nyingi, ni kufanya survey kwanza, ndio nikayaona haya ya soko la dunia.

Vifaa vyangu nanunulia Yemen enter/Wahenga, ni warasimu lakini walau unapata genuin.
 
Mara ya mwisho wakikuingiza chaka nijuze.. nina kikosi kazi Tandale kwa mtogole.. mabaka cha mtoto(jk)...!!!:evil:
 
Mkuu hiyo kwenye red wako wapi hao mkuu maana nami najiandaa kuanza ujenzi.
 
Asante mkuu kwa taarifa.nilishajiuliza sana kwa nini mibongo inapenda utapelitapeli tu sipati jibu

Yaani pia huwa najiuliza sipati jibu na kwa kweli inauma sana. Vyombo vyetu vya dola vinajua sana haya lakini watu hawa hawachukuliwi hatua ndo maana wanafanya yote haya. Kama kungekuwa na adhabu kali kwa wahusika nafikiri wageacha huu uhuni wanaotufanyia.
 
Mara ya mwisho wakikuingiza chaka nijuze.. nina kikosi kazi Tandale kwa mtogole.. mabaka cha mtoto(jk)...!!!:evil:

Poa, nilitaka niwachomee nguru,huruma kwa mwenye mali ikaniingia,hasa wale wa nondo pale soko la dunia.
 
Mkuu hiyo kwenye red wako wapi hao mkuu maana nami najiandaa kuanza ujenzi.

Yemen enter, wapo Buguruni karibu kabisa na KCB yaani ukifika Kobil petrol station,fanya kama unakwenda Ubungo mkono wa kulia kwako, duka la kwanza acha ni vimeo,duka la pili ni Yemen na jengo linalofuata ni KCB ( kenya commercial Bank) pia wana tawi pale Mwembechai. Ni wadada damu za kiarabu,hawana haraka lakini haibiwi mtu pale. Hawana mbao, ila mazagazaga mengine yapo.

Wahenga wako upande huo huo wa kulia, wao ni bati,nondo zaidi, wewe uliza Wahenga wapi, slow lakini uhakika, pia uliza one one, wao wanafuata kwa chini baada ya Wahenga, hawa ni bati zaidi. Kwa Buguruni central pale hayo ni maduka ya kuaminika. Na moja liko karibu na Sekulu,nimesahau jina lake, wao ni saruji kwa vipimo vya kiwandani.
 
Ukitaka mbao za dawa kabisa nenda pale sao hill wana mbao nzuri za dawa au mtafute agent wao mbezi beach Enea hardware simu 0784207307

Mkuu naona umeamua kujipigia debe kabisa hapa........Enny=Enea (?)
 
Back
Top Bottom