SoNotorious
JF-Expert Member
- Sep 11, 2011
- 2,422
- 859
Ndugu wana JF!
Je mnajua jinsi Bank inayosikiliza "CRDB" inavyoibia wateja wake? Fikiria kila ukitoa pesa kwenye ATM wanakata shs. 700.00. Wanasema kwa siku unaweza kutoa shs. 1,000,000.00. Lakini huwezi kutoa hiyo million moja mara moja utatoa mara tatu na kila ukitoa unakatwa shs. 700/=, kwa ujumla utakatwa shs. 2,100/=, hizo ni hela nyingi sana.
Na ujue kila mwezi unakatwa shs 1,500/= kama reja fee. Sasa huu ni wizi kama ule wa ESCROW.
Watanzania tuamke na tukatae wizi wa mchana mchana.
Naomba kuwasilisha!
Kama unaona kuweka hela benki ni gharama weka ndani kwako tuje tuzichukue mchana kweupe.