CRDB ukiangalia salio tu simbanking, wanakata, lakini NMB-mobile sijaona haya mambo. Kweli watanzania tunanyonywa.
Mkuu je unafahamu kuwa banking ni biashara kama biashara zingine? Unapofanya biashara unategemea kutengeneza faida na si hasara. Sasa unapowaita ni wezi wakati umesaini mkataba nao, na umekubaliana na masharti yao bila shuruti yoyote, huoni kama huwatendei haki? Halafu tambua kuwa tundu la kutolea pesa kwenye ATM lina uwezo wa kutoa noti 40 tu kwa wakati mmoja. Kwa maana hiyo kiasi unachoweza kutoa kwa wakati mmoja kinategemea na thamani ya noti iliyowekwa kwenye ATM.
Mfano
- Kama ni noti ya shilingi 500 basi itakuwa 500 x 40 =20,000/=
- Kama ni noti ya shilingi 1,000 basi itakuwa 1,000 x 40 =40,000/=
- Kama ni noti ya shilingi 2,000 basi itakuwa 2,000 x 40 =80,000/=
- Kama ni noti ya shilingi 5,000 basi itakuwa 5,000 x 40 =200,000/=
- Kama ni noti ya shilingi 10,000 basi itakuwa 10,000 x 40 =400,000/=
Faida kubwa ya bank inategemea kukopesha hela, ambazo kwa sasa zina insurance hivyo wanajihakishia faida for over 90%. Hayo mabilioni wanayopata ya mikopo kwa hela za wateja more than 20% interest kwa mkopo; mteja aliyewapa hela zake wafanyie biashara anafaidikaje??
kwa ujumla naona CRDB wameingiza michango mingi sana kwa pamoja;
Kutoa hela juu
- kuangalia salio wanacharge
- statement wanacharge
- Kubadilisha kard ambayo ni lazima kila 2yrs shs 7300???? huu sio wizi??
- kutoa hela mara moja 700shs
- Michango hiyo yote na mingine imeingizwa bila taarifa rasmi ya makato yanayo ongezeka kwa wateja
binafsi naona wamejisahau???
Ndugu wana JF!
Je mnajua jinsi Bank inayosikiliza "CRDB" inavyoibia wateja wake? Fikiria kila ukitoa pesa kwenye ATM wanakata shs. 700.00. Wanasema kwa siku unaweza kutoa shs. 1,000,000.00. Lakini huwezi kutoa hiyo million moja mara moja utatoa mara tatu na kila ukitoa unakatwa shs. 700/=, kwa ujumla utakatwa shs. 2,100/=, hizo ni hela nyingi sana.
Na ujue kila mwezi unakatwa shs 1,500/= kama reja fee. Sasa huu ni wizi kama ule wa ESCROW.
Watanzania tuamke na tukatae wizi wa mchana mchana.
Naomba kuwasilisha!
yaan hawa jamaa ni noma mi nilifungua business ac nakatwa 12500 kwa mwezi na kila nikitoa hela kwenye atm nakatwa hela tena unaweza kutoa mil 2 yaan lak nne mara 5 hivyo unakatwa 4000. Halafu wizi mwingine mkubwa kila mteja hukatwa 4400 kwa ajili ya kumiliki atm card. majanga!!!
Kwani hela yetu hawaizungushi kupata faida? Ningekuwa na akaunti huko ningebeba hela zangu zoteJamani hizo ndo bank charges au hamjui? Hakuna free lunch. Kutoa au kutuma milion moja m pesa kiasi gani?
Faida kubwa ya bank inategemea kukopesha hela, ambazo kwa sasa zina insurance hivyo wanajihakishia faida for over 90%. Hayo mabilioni wanayopata ya mikopo kwa hela za wateja more than 20% interest kwa mkopo; mteja aliyewapa hela zake wafanyie biashara anafaidikaje??
kwa ujumla naona CRDB wameingiza michango mingi sana kwa pamoja;
Kutoa hela juu
- kuangalia salio wanacharge
- statement wanacharge
- Kubadilisha kard ambayo ni lazima kila 2yrs shs 7300???? huu sio wizi??
- kutoa hela mara moja 700shs
- Michango hiyo yote na mingine imeingizwa bila taarifa rasmi ya makato yanayo ongezeka kwa wateja
binafsi naona wamejisahau???
Kahamishie hela zako kwenye M-pesa!
Kule nchi jirani wana mbinu za kuteka mtu kisha wanakuambia uhamishe salio lako lote!