Wizi wa Airtel

Maengo

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
280
29
Jana usiku majira ya saa nne niliweka muda wa maongezi wa sh.4,000/= kisha nikanunua kifurushi cha intanet cha MB400 kwa sh2500. Nikaperuziperuzi kwenye intanet kwa muda wa nusu saa pasipo ku-download kitu chochote. Leo asubuhi nikaperuz tena kwa muda wa kama wa kama lisaa limoja na baada ya hapo connection ya intanet ikawa inazingua. Cha kushangaza nilipoangalia salio langu kifurushi nikaambiwa nimeshatumia MB400 zote! Na nilipojaribu kuangalia salio la kawida ambapo jana nilkuwa nimebakiwa na sh 1500 sikukuta kitu! Nilipojaribu kuwapigia huduma kwa wateja walinipa majibu ambayo sikuridhishwa nayo kabisa.
Naona hawa jamaa nao wameanza wizi kama wa TIGO.
 
tungekuwa na active tcra haya yote yasingekuwa yanatupata
10% zinatutafuna watz. mi ndo leo nimehamia airtel
kutoka kwa wase.nge tigo halafu ndo hivo tena. but sirudi
nyuma.
 
Hapana matatizo Kama haya huwa yanatokea Mara chache sana hii inaitwa use overchaged hapo cha msingi piga Tena customer care wakuangalizie matumizi ya siku ya jana au nitumie number yako ya simu unayotumia kwenye modem nitawapelekea kitengo kinachohusika wakuangalizie Mimi nipo kitengo kingine mkubwa!!
 
Nashawishika kupingana na ww. Mimi hununua kifurushi cha Airtel internet cha 400 MB kwa tsh 2500. Natumia mobile internet karibu kila wakati ingawa ku download ni mara chache tumie. Inafika siku 30 najikuta bado nina balance ya mb100 au zaidi ambazo sijazitumia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom