Wizi wa aina mpya ukiwa Kariakoo

Wizi wa aina mpya ukiwa Kariakoo

Habari zenu wanajamvi!

Dhumuni la uzi huu ni kutoa taarifa ya tahadhari muwapo maeneo ya Kariakoo mitaa ya Agrey na msimbazi au Agrey yote! Jana baada ya yakutoka katika mizunguko yangu mida ya saa kumi za jioni! Nilipitia maeneo hayo na wadada fulani wawili niliowapa lift wakaniomba niwashushe kuna kitu walikua wanahitaji maeneo hayo!

Sasa baada ya kuwashusha kusogea mbele kidogo nikasikia jamaa akiniita kunieleza kua naitwa ile kugeuka kutizama tu kushoto kwangu jamaa mwengine akaingiza kichwa na kuchomoa simu yangu aina ya s8 galaxy iliokuepo kwenye charge! Kumbe kufunga vioo pia inasaidia sana kupunguza wahalifu kufanya yao!kwahiyo hapa nilipo maumivu yangu ni makali mnoo!hata kazini sijakwenda kwa maumivu ya jana!!

so nawapa angalizo muwapo maeneo hayo!!
Mimi pia mitaa ya Livingstone walinifanyia kitu kama hicho ila hawakufanikiwa,jamaa mmoja aliniita upande wangu akidai ananifahamu kwahiyo nisimamishe gari ile nageuka upande wa pkushoto nakutana na jamaa mwingine ameshaingiza kichwa anataka kuchukua simu nikampiga ngumi ya akili akachomoka na kukimbia,toka siku hiyo nikiwa mitaa yaenye mikusanyiko ya watu wengi nafunga kioo au kupandisha juu kabisa na kuacha nafasi kidogo..
 
Huuu wizi sio mpya dogo...uko long tym ago...hakunaga mjanja wa dar anapita eneo hatarishi akaacha kioo wazi...unayajua maeneo hatarishi?
Km sio mwenyeji dar waulize jiran zako watakueleza
 
Tatizo nililoona ni kuwa ulikuwa haujafunga vioo tu na wala si lift.
 
Habari zenu wanajamvi!

Dhumuni la uzi huu ni kutoa taarifa ya tahadhari muwapo maeneo ya Kariakoo mitaa ya Agrey na msimbazi au Agrey yote! Jana baada ya yakutoka katika mizunguko yangu mida ya saa kumi za jioni! Nilipitia maeneo hayo na wadada fulani wawili niliowapa lift wakaniomba niwashushe kuna kitu walikua wanahitaji maeneo hayo!

Sasa baada ya kuwashusha kusogea mbele kidogo nikasikia jamaa akiniita kunieleza kua naitwa ile kugeuka kutizama tu kushoto kwangu jamaa mwengine akaingiza kichwa na kuchomoa simu yangu aina ya s8 galaxy iliokuepo kwenye charge! Kumbe kufunga vioo pia inasaidia sana kupunguza wahalifu kufanya yao!kwahiyo hapa nilipo maumivu yangu ni makali mnoo!hata kazini sijakwenda kwa maumivu ya jana!!

so nawapa angalizo muwapo maeneo hayo!!
pole sana hy ni style ya zamani sana,ulikuwa hujalizwa tu,ndio maana mliambiwa muweke tinted
 
Back
Top Bottom