Ngonalugali
JF-Expert Member
- Jan 12, 2008
- 659
- 102
Habari zenu wana JF,
Ni kwamba kuna utaratibu kwenye viwanja vya ndege kuzuia abiria kubeba vichupa vyenye vimiminika zaidi ya ml100. Kwa hiyo inalazimu abiria kulazimisha kupima mzigo hata kama una 6kg ili mradi kusalimisha mafuta na vi-manukato kwa namna moja ama nyingine.
Kitu kilichojitokeza pale ni kwamba kampuni ya kupakia na kupakua mizigo ya Swiss port imeshindwa kudhibiti wafanyakazi wake na hivyo kupoteza hadhi ya kuchukua dhamana ya mizigo ya abiria. Nilichokiona mimi ni kwamba wale jamaa wanaobeba mizigo hufungua zipu na kukagua kilichomo ndani. Wakiona kitu cha thamani wanaweka mifukoni mwao. Na kinachoumiza ni kwamba kama kuna vitu vilikuwa kwenye mifuko midogo ndani ya begi ambavyo labda ulitaka visigusane na vingine basi utavikuta tofauti, maana wanachana vimifuko ili kutafuta wanachokitafuta wao (WIZI MTUPU), ustaarabu hakuna hata kidogo.
Sasa nataka kuuliza kuna usalama gani kama mtuu amepima mzigo ili kufuata sheria za usalama wa usafiri wa anga na hatimae wajinga wachache wapitie vitu vya thamani kwenye mizigo yake?
Na je, hii itatoa picha gani kwa abiria wapendao kutumia viwanja vyetu kusafiri kwa kuchukulia kuwa ni salama kwa kwa mali na mizigo yao?