Wizi huu wa Benki sio mzuri kwa Taifa

Kamundu

JF-Expert Member
Nov 22, 2006
4,210
2,000
Rafiki yangu mmoja mwenye asili ya India anapata shida kupata pesa zake. Kaka yake diaspora Canada kamtumia $100,000 wanunue mabasi ya biashara ya familia.

Pesa ikaingia mwezi wa kumi alipoenda akaambiwa kwasababu ya uchaguzi wana wasiwasi hivyo pesa haitakuwepo mpaka baada ya uchaguzi. Mwezi wa kumi na moja akaniomba ushauri nikamwambia watakuwa wameweka kwenye fixed deposit kwa muda ili wapate faida binafsi maana sababu zao hazipo kisheria.

Akatafuta wakili kabisa wakili kuandika barua anaambiwa pesa hamna hazipo kabisa ! Lakini wataanza kupewa nusu Tarehe 10 mwezi wa kumi na mbili na nyingine kwa awamu mbili!

Yaani ni kama nilivyosema wameweka pesa kwenye fixed na inaelekea kwenye fixed deposit ya zaidi ya miezi 3 ili wale faida ya pesa. Fixed deposit mfano kama inalipa 3% tu kwa miezi hiyo ni $3,000 ambayo hawajafanyia kazi yoyote.

Na kwasababu ni Wahindi wanatishiwa bila kuwa na sababu zozote kisheria. Kibaya zaidi hii inatisha watu kuleta Tanzania pesa za miradi na inatakiwa kuchunguzwa mara moja.

Tusaidieni kulisema hili linauwa sana uwekezaji wa ndani.

Pascal Mayalla
 
Bill

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
6,531
2,000
Rafiki yangu mmoja mwenye asili ya India anapata shida kupata pesa zake. Kaka yake diaspora Canada kamtumia $100,000 wanunue mabasi ya biashara ya familia. Pesa ikaingia mwezi wa kumi alipoenda akaambiwa kwasababu ya uchaguzi wana wasiwasi hivyo pesa haitakuwepo mpaka baada ya uchaguzi...
Mkuu ikiwa pesa ni clean money haikutakiwa wawazungushe namna hiyo. Msiwalazie damu, mwanasheria wenu anaweza kuripoti hili suala BOT kwani wanachofanya ni uhuni.

BTW hao ni benki gani?

Tatizo la benki nyingi zina shida ya pesa za kigeni wakipata hako ka mwanya wanachangamkia kweli kweli. Benki nyingi zinajiendesha kimagumashi kuonesha zina pesa nyingi kumbe hakuna. Kuna sheria inayowabana kuwa na kiasi fulani cha pesa sasa inawezekana kwa kufanya hivyo wana balance vitabu vyao ili kukidhi matakwa ya BOT.

HILI SUALA LAKO HALIINGILIANI NA WALA HALINA UHUSIANO NA UCHAGUZI. KWANI WAO NI HAZINA?

CHUKUA HATUA KABLA HAUJACHELEWA, WANA TATIZO LA PESA HAO KWANI $100,000 NI SAWA NA TZS 230,000,000
 
Kamundu

JF-Expert Member
Nov 22, 2006
4,210
2,000
Huu ni mfano mmoja tu wa wazi ni bank karibu zote kwa ushirikiano na jamaa wa bank kuu. Lakini target zao kubwa ni wahindi na diaspora. Bank zote zina hili tatizo. Nasubiri apate pesa zake kwanza nitasema hii bank nayo lakini ni ma bank yote kuna watu wachafu ndani
 
Kamundu

JF-Expert Member
Nov 22, 2006
4,210
2,000
Mkuu ikiwa pesa ni clean money haikutakiwa wawazungushe namna hiyo. Msiwalazie damu, mwanasheria wenu anaweza kuripoti hili suala BOT kwani wanachofanya ni uhuni...

Hakutaka hata kutoa kwa Dollar! Lakini kuna fees za 1% kama account yako ya dollar ambayo ni standard maana ni gharama ya kuleta $ Tanzania
 
Mshuza2

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
8,304
2,000
Bank nyingi zina liquidity issue (Ukata), haukawii kusikia kesho yake BOT wametia timu na makufuli yao. Ukitaka kuweka pesa nyingi benki kwa sasa inabidi ufanye due deligence ya kutosha kujua uimara wa benki katika kulipa madeni yake (liabilities).
Wana maswali mengi sana siku hizi,pesa zako lakini mpaka ujute.
 
Bill

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
6,531
2,000
Huu ni mfano mmoja tu wa wazi ni bank karibu zote kwa ushirikiano na jamaa wa bank kuu. Lakini target zao kubwa ni wahindi na diaspora. Bank zote zina hili tatizo. Nasubiri apate pesa zake kwanza nitasema hii bank nayo lakini ni ma bank yote kuna watu wachafu ndani
Mkuu hebu funguka katika hili ili wahusika wajue kwani inawezekana michezo inafanyika under carpet na wachukua maamuzi hawajui. Tulisemee hili na pengine hata wabunge wapewe maelezo wakalisemee bungeni kwa mpango kuhusu watu wanaohujumu uchumi wa nchi kwa kuvuruga (frustrate) diaspora na wengine wenye nia njema
 
Bill

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
6,531
2,000
Hakutaka hata kutoa kwa Dollar! Lakini kuna fees za 1% kama account yako ya dollar ambayo ni standard maana ni gharama ya kuleta $ Tanzania
Awaripoti BOT ikiwa wanaendelea kumkwamisha. Haiwezekani pesa zake watumie kubalance vitabu vyao wapuuzi hao. Awape notice ya siku hata 3 kisha awapeleke BOT.
 
Kamundu

JF-Expert Member
Nov 22, 2006
4,210
2,000
Mkuu hebu funguka katika hili ili wahusika wajue kwani inawezekana michezo inafanyika under carpet na wachukua maamuzi hawajui. Tulisemee hili na pengine hata wabunge wapewe maelezo wakalisemee bungeni kwa mpango kuhusu watu wanaohujumu uchumi wa nchi kwa kuvuruga (frustrate) diaspora na wengine wenye nia njema

Hapa kuna maswala mawili . Kwanza wizi lakini nimegundua hatuna utaratibu wa kuwalinda minority wetu kama wahindi au Watanzania wenye asili nyingine kwa manyanyaso. Jamaa anaogopa sana ingawa hajafanya kitu chochote kibaya. Mimi pia ni minority hapa US najua kuna uwoga tu wa kuwa minority. Hivyo siwezi kutoa specific mpaka aniruhusu lakini limeniuma tu.
 
Nokia83

JF-Expert Member
Jan 16, 2014
24,649
2,000
Hapa kuna maswala mawili . Kwanza wizi lakini nimegundua hatuna utaratibu wa kuwalinda minority wetu kama wahindi au Watanzania wenye asili nyingine kwa manyanyaso. Jamaa anaogopa sana ingawa hajafanya kitu chochote kibaya. Mimi pia ni minority hapa US najua kuna uwoga tu wa kuwa minority. Hivyo siwezi kutoa specific mpaka aniruhusu lakini limeniuma tu.
Bank gani hiyo?..unaogopa kuitaja?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom