Wizi huu wa Benki sio mzuri kwa Taifa

Mkuu kuwakomoa mwambie kaka yao akadai pesa yake kwa kuwa haijawafikia walengwa ili Bank yake aliyoitumia kutuma pesa iwapeleke puta hayo majizi ya Bank na pia adai riba yake yote.
Rafiki yangu mmoja mwenye asili ya India anapata shida kupata pesa zake. Kaka yake diaspora Canada kamtumia $100,000 wanunue mabasi ya biashara ya familia. Pesa ikaingia mwezi wa kumi alipoenda akaambiwa kwasababu ya uchaguzi wana wasiwasi hivyo pesa haitakuwepo mpaka baada ya uchaguzi...
 
Rafiki yangu mmoja mwenye asili ya India anapata shida kupata pesa zake. Kaka yake diaspora Canada kamtumia $100,000 wanunue mabasi ya biashara ya familia. Pesa ikaingia mwezi wa kumi alipoenda akaambiwa kwasababu ya uchaguzi wana wasiwasi hivyo pesa haitakuwepo mpaka baada ya uchaguzi...
Kama ni kweli nenda BoT mnara wa kaskazini ghorofa ya 6 utapata msaada hapohapo. Nenda na nyaraka ikiwepo SWIFT message aliyopewa mtumaji na benki yake ya Canada.
 
Nilitumiwa 135$ kutoka kwa kutoka Standard Chartered Kenya kuja Tz , muvi linaanza alienitumia alilipia gharama ya 20$ huko kwao,

Naenda cheki mzigo benki yangu wameruka na 34$ imebaki 101$.

Nikasema hizo mambo za bank tranfer siztaki tena. Bora nirudi western au mpesa tu.

Movie la pili kuna rafki yangu alitakiwa atumiwe kama 1000$ msoto aliopitia na benki daaah.. mara anaekutumia aandike barua mara tushughulike maombi. Stori kibwenaaa
 
Rafiki yangu mmoja mwenye asili ya India anapata shida kupata pesa zake. Kaka yake diaspora Canada kamtumia $100,000 wanunue mabasi ya biashara ya familia...

Mkuu hizo sababu alizokueleza huyo jamaa yako sidhani kama zina ukweli, na hicho ulichomwaminisha kuhusu fixed pia sio kweli.

Iko hivi, ktk suala zima ka anti- money laundering policy, benki zinaelekezwa na BOT kufanya KYCs za kutosha kabla ya kuruhusu fedha kutumwa iwe ni nje au ndani ya nchi vilevile wakati wa kulipwa/kupokelewa.

Hapa lazima mtumaji atoe maalezo yaliyojitosheleza yakiambatana na vielelezo juu ya uhalali wa fedha hizo. Hata hivyo hayo hayachukui muda mrefu kufanyika na pengine ikawa ni dk 5, 10, 30 nk kutegemea na situation.

Kuhusu fixed. Kwa mujib wa mwongozo wa BOT ambaye ndiye msimamizi wa benki zote nchini TZ, fixed ni akaunti kama zilivyo akaunti nyingine zifunguliwazo na benki km vile normal saving accounts ambapo lazima awepo mteja (mfunguaji wa hiyo account) ambapo anapaswa kuleta barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa anaoishi au kwa mwajiri wake kama ni mtumishi.

Anatakiwa ajaze fomu ya kufungua akaunti, alete kitambukisho chake hasa cha utaifa au mpiga kura au passport ya kusafiria au work permit.
Asaini hiyo fomu vizuri na kuweka dole gumba na mambo mengine mengi ikiwa ni pamoja na picha zake.

Fixed account zote zilizofunguliwa ndani ya mwaka lazima zikaguliwe na auditors ili kuona kama kulikuwa na compliance.

Kwa hali hiyo rafiki hakuna mfanyakazi anayeweza kujiunguza vidole vyake mwenyewe eti kisa anatete benki kwa kukeuka miongozo ya BOT na sheria nyingine za kifedha za kimataifa. Kumbuka penalty kutokana na in compliance ni kubwa sn na hata wakati mwingine benki kusimamishiwa huduma kwa muda
 
Hii habari inawezekana ni yakupika. Ni nini kinamfanya ashindwe kuweka jina la benki hapa kama ni kweli?!
 
Awaripoti BOT ikiwa wanaendelea kumkwamisha. Haiwezekani pesa zake watumie kubalance vitabu vyao wapuuzi hao. Awape notice ya siku hata 3 kisha awapeleke BOT.

Kwani zile pesa za watu walioporwa kwenye Bureau de change zilienda wapi!
 
Kwani zile pesa za watu walioporwa kwenye Bureau de change zilienda wapi!
Mkuu huo hauwezi kuita uporaji, tambua kuna sheria inayosimamia uendeshaji wa maduka hayo. Sasa ikiwa walikiuka lazima wakumbane na adhabu. Mfano tu nikupe, mtaji uliosajili wewe ni dola 300,000 wakaja kukagua na kufanya hesabu za usuluhishi ( accounts reconciliation) ukakutwa una ziada inafikisha mzunguko wako hadi dola 500,000. Moja kwa moja wewe ni mtakatisha fedha haramu ( money launder) na adhabu yake unaijua, hizo pess sio zako zinabebwa zote pamoja na kila kitu kilichokutwa humo.

Sasa hapo mtu asiyejua anaita uporaji wakati ni uhalifu wa kiuchumi umedhibitiwa.
 
Rafiki yangu mmoja mwenye asili ya India anapata shida kupata pesa zake. Kaka yake diaspora Canada kamtumia $100,000 wanunue mabasi ya biashara ya familia.

Pesa ikaingia mwezi wa kumi alipoenda akaambiwa kwasababu ya uchaguzi wana wasiwasi hivyo pesa haitakuwepo mpaka baada ya uchaguzi. Mwezi wa kumi na moja akaniomba ushauri nikamwambia watakuwa wameweka kwenye fixed deposit kwa muda ili wapate faida binafsi maana sababu zao hazipo kisheria.

Akatafuta wakili kabisa wakili kuandika barua anaambiwa pesa hamna hazipo kabisa ! Lakini wataanza kupewa nusu Tarehe 10 mwezi wa kumi na mbili na nyingine kwa awamu mbili!

Yaani ni kama nilivyosema wameweka pesa kwenye fixed na inaelekea kwenye fixed deposit ya zaidi ya miezi 3 ili wale faida ya pesa!. Fixed deposit mfano kama inalipa 3% tu kwa miezi hiyo ni $3000 ambayo hawajafanyia kazi yoyote.

Na kwasababu ni wahindi wanatishiwa bila kuwa na sababu zozote kisheria. Kibaya zaidi hii inatisha watu kuleta Tanzania pesa za miradi na inatakiwa kuchunguzwa mara moja.

Tusaidieni kulisema hili linauwa sana uwekezaji wa ndani
Pascal Mayalla
Huu ni wizi sasa. Dah very bad better to invest in Kenya than Tanzania
 
Back
Top Bottom