kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 16,247
- 16,169
Baada ya sekeseke la Oct29 kuunda wizara ya vijana kulionekana kama sehemu ya majibu na tiba ya kilichotokea na kilichosababisha vijana wakubali kutumika.
Hata hivyo, vijana ni nani na wako wapi?. Vijana ni wale wenye umri chini ya miaka 40 hivi. Vijana hawa wengi wao wako kwenye familia, mitaani, shuleni, vyuoni, majeshini, kwenye ajira za umma na watu binafsi binafsi, na wengine wengi wamejiajili wenyewe kwenye kazi mbalimbali; lakini lipo kundi ambalo hawana ajira kabisa.
Hii maana yake vijana tayari wako kwenye wizara ambazo tayari zipo, ilikuwa ni maswala tu ya kila wizara na kila sekta itimize wajibu wake katika kuwahudumia wadau ambao wengi wao ni vijana. Mfano, TAMISEMI, wizara ya ulinzi, ujenzi, usafirshaji, maendeleo ya vijana, wazee na wenye ulemavu, habari, michezo, utamaduni wanafanya nini kwa vijana wao walioko kwenye secta zao?
Kuunda wizara ya vijana itasababisha mkanganyiko wa kimajukumu na wizara nyingine kwasabu vijana ni haohao wanaohudumiwa kwenye wizara zote kama kilimo, ufugaji, elimu, usafirishaji, tamisemi, nk. Labda jina la wizara lingekuwa Wizara ya vijana wasiokuwa na ajira.