Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari yawakabidhi wakandarasi mikataba ya shilingi bilioni 7.5

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
295
679
1612422162727.png

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amewaagiza wakandarasi wanaokwenda kutekeleza miradi minne ya miundombinu ya mawasiliano yenye thamani ya shilingi bilioni 7.5, kuhakikisha wanafanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha kazi hiyo ndani ya muda wa mkataba bila kuongeza hata siku moja ya ziada.

Dkt. Ndugulile alizungumza hayo alipokuwa katika hafla ya makabidhiano ya mikataba ya kazi hiyo baina ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula na wakandarasi hao wazalendo ambao ni Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) na Raddy Fibre Solution Ltd katika viwanja vya Bunge, jijini Dodoma.

Miradi hiyo ni pamoja na kujenga, kupanua na kuunganisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ili kuunganisha na kuimarisha mawasiliano kutoka Mkoa wa Singida hadi Mkoa wa Mbeya, maeneo ya Mkoa wa Mtwara ili kuunganisha mawasiliano kati ya Tanzania na Msumbiji na kutoka eneo la Mji wa Serikali Mtumba hadi Msalato jijini Dodoma.

Aliongeza kuwa jumla ya kilomita 409 zitaunganishwa na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika maeneo hayo na Halmashauri 12 nchini zitawekewa vibao vya majina ya mitaa/barabara na namba za nyumba katika kutekeleza Mradi wa anwani za makazi na postikodi.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa lengo ni kuhakikisha mpaka kufikia mwaka 2025 asilimia 80 ya wananchi wanapata mawasiliano ya uhakika na kushiriki katika kuinua uchumi wa kidijitali kupitia biashara mtandao, ambapo mnunuzi na muuzaji lazima wawe na mawasiliano ya mtandao na mnunuzi kuwa na anwani ya makazi ili afikishiwe bidhaa aliyonunua mpaka nyumbani kwake.

“Sina shaka na wakandarasi wazalendo, mtajiengua ninyi wenyewe iwapo mtakuja na visingizio vya kutokamilisha kazi kwa wakati, mkafanye kazi mchana na usiku kuhakikisha miradi inakamilika ndani ya muda wa mkataba na ubora unaokubalika”, Dkt. Ndugulile

Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa Wizara inaendelea na mchakato wa kushughulikia suala la vifurushi na bando na kuomba wananchi kuwa na subira mpaka mwisho wa mwezi huu ili Wizara kuja na tamko rasmi ambalo halitaathiri mapato ya watoa huduma, mapato ya Serikali na vilevile kutomuathiri mwananchi.

Katika hatua nyingine, Dkt. Ndugulile ametoa rai kwa wananchi wasipokee maelekezo yeyote kuhusu miamala binafsi kwa njia ya simu bali njia sahihi ni kwenda kwenye vituo vya mawakala vinavyotambulika na vilivyosajiliwa na makampuni ya simu.

“Tunataka kuimarisha mifumo ya mawakala wa makampuni ya simu ili kuweza kuwabaini na kuwachukulia hatua mawakala ambao sio waaminifu”, Dkt. Ndugulile

Amesema kuwa, Serikali imeanza mkakati wa kushughulika na watu wanaotoa lugha za matusi, kashfa na utapeli mitandaoni ambapo mpaka sasa genge la watu 17 wanaoongoza genge la uhalifu mitandaoni waliokuwa wamejificha mkoani Morogoro wameshakamatwa na muda wowote watapandishwa mahakamani.

Ameongeza kuwa Serikali ina nia njema ya kujenga mazingira wezeshi ya kuweza kutumia mitandao ya mawasiliano na katiba ya nchi inaruhusu wananchi kukosoa kwa lugha ya staha, huku akisisitiza kuwa lugha za matusi, kashfa na kejeli hazitovumilika.
 
Dkt. Ndugulile amesema kuwa lengo ni kuhakikisha mpaka kufikia mwaka 2025 asilimia 80 ya wananchi wanapata mawasiliano ya uhakika na kushiriki katika kuinua uchumi wa kidijitali kupitia biashara mtandao, ambapo mnunuzi na muuzaji lazima wawe na mawasiliano ya mtandao na mnunuzi kuwa na anwani ya makazi ili afikishiwe bidhaa aliyonunua mpaka nyumbani kwake.
Ili kufanikisha hili la kushiriki uchumi wa kidigitali serikali iruhusu matumizi ya kupokea pesa kwa Paypal

Tanzania kumekuwa na tatizo kubwa la ajira. Njia moja ya kuondoa hilo tatizo ni kwa watu kutafuta kazi za kufanya online, yaani mitandaoni. Kazi zipo nyingi. Mfano, waweza pata kazi ya kutafsiri website ya kampuni au mtu kwa Kiswahili au kutafsiri kitabu. Unafanya online malipo yanakuwa kwa njia ya PayPal hata kwenye simu yako ya mkononi, hata mwajiri au mnunuzi awe Ulaya au Marekani.

Pia, mtu waweza chora hata katuni, ramani za nyumba n.k ukauza online. Au, ukajitungia wimbo wako wa kienyeji binafsi nyumbani kwako bila hata kwenda studio, ukauweka kwa mfumo wa video au audio ukauuza online kwenye maduka kibao ya online.

Tatizo kwa Tanzania haijaruhusu matumizi ya kupokea pesa kwa njia ya PayPal ambapo mtu aki-click tu kununua bidhaa yako, pesa yako inaingia chapchap kwenye PayPal account yako.

Kenya walisharuhusu; vijana wengi hushinda mitandaoni wakitengeneza pesa wakiuza bidhaa zao, viwe vichekesho, michezo ya kuigiza n.k ambavyo huviuza online. Wanaweka clip zao kwenye maduka ya online mtu ananunua anamlipa online kupitia Paypal.

Kuna shughuli nyingi za ujasiliamali online. Kikwazo kwa nchi yetu ni upataji wa pesa wa kazi yako au mauzo yako online. Bado tuko enzi za mawe tukiamini minjia ya kizamani ya kupokea hela. Na hivyo kuifanya nchi yetu kuwa ni ya kulipa zaidi pesa za kigeni na si ya kupokea pesa za kigeni.

Serikali ikiruhusu upokeaji pesa kupitia PayPal itafanya vijana wengi waingie mitandaoni kutafuta pesa.

Biashara za online zaweza kufungua Watanzania wengi kupata pesa toka nje, sababu ni juhudi ya mtu binafs na ubunifu wake tu auze nini. Waweza kujirekodi unarukaruka kama ngedere ukiimba hovyohovyo tu bila hata vyombo halafu ukaita wimbo Crazy Monkey Song ukauweka online na ukauza. Wapo watu wana pesa wanapenda vituko wananunua.

Taasisi za elimu nazo ziweke kwenye mitaala ujasiliamali wa online wasibakie tu kufundisha ujasiriamali wa kuzurura tu juani wa kimachinga.
 
Back
Top Bottom