Wizara ya Mambo ya Ndani ndiyo inayoongoza kwa Mawaziri wake kufukuzwa

ebaeban

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
2,196
2,000
Wizara ya mambo ya ndani ndiyo inayoongoza kwa mawaziri wake kufukuzwa.

Katika kuuaga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya tujikumbushe mawaziri wa mambo ya ndani waliomaliza salama, waliojihudhuru na waliofukuzwa, Sasa tuanze:-

1. Said Maswanya............alifukuzwa na Nyeyere
2. Ali Hassani Mwinyi ............alijihuzulu katika kashifa ya Teddy Kasela Bantu ya kuuwa wachawi
3. Alhaji Omary Muhaji............alifukuzwa katika ile kashifa ya gari aina ya VOLVO miezi sita tu Volvo zote 60 juu yamawe inasemekana alichukua mlungula
4. Salmin Amour....................alihamishwa kwa usalama
5. Abdala Natepe ............... alifukuzwa ile kashifa ya wahaini kukimbia magereza ukonga akina Banyikwa
6. Brigadia Mhidin Kimariyo..................alifukuzwa katika kashifa ya gorafa la wizara kuunguwa moto
7. Agustino Lyatonga Mrema..................alifukuzwa baada ya kulewa madaraka, alilewa akawa chakari
8. Mgunya mmoja kwa jina AMIR.......... ALIKIMBLIA Zanzibar kugombea urais akakosa
9. Omary Mapuri ...............alifukuzwa kashifa ya kupiga waandishi wa habari katika barracks za magereza
10. Laurence Masha ....................... alifukuzwa na wanainchi wa Mwanza
11. Emmanuel Mnchimbi ..................... huyu alifukuzwa na vumbi likatimka

Hebu nisaidieni niliowasahau.
 
allydou

JF-Expert Member
Apr 16, 2009
1,598
2,000
Hiyo ya mrema, maisha na nchimbi nimecheka Mpaka mbavu zinauma. Dahh mrema alilewa chakari, masha wana mwanza wakamgeuza kibanga na mkoloni, jeuri nchimbi ndio Mpaka vumbi likatimka. Kweli jf raha mustarehe.
 
Uledi

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
588
1,000
Mrema alikuwa mtu wa ajabu sana kuna siku alilewa kwenye party aliyoalika Wahindi ambao kipindi kifupi nyuma walikuwa maadui zake( kumbuka mambo ya kina Chavda) akaanza kucheza kama mwehu huku anasema wahindi ni shemeji zake mara sijui nn jamaa bure kabisa
 
fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,449
2,000
Kweli wizara hiyo ni ngumu, ila kwa hawa wanne wa juzi juzi, nadhani JK alikuwa amewachoka ile hali ni marafiki zake wa karibu akaunda mbinu ya kiusalama salama wa taifa hivi ili wafukuzwe. Si unajua Mathayo Mtoto wa Msuya, Nchimbi rafiki wa karibu Enzi za UVCCM, Nahodha heshima ya Waziri Kiongozi na Kagasheki rafiki wa karibu, angewafukuza vipi???
 
Chris Lukosi

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
4,581
2,000
Kwa sababu ni wizara kioo kwa serikali

Pale akiingia Deo Filikunjombe na kangi lugora lazima moto uwake
 
Bukile

Member
Sep 12, 2013
88
125
Kwa sababu ni wizara kioo kwa serikali

Pale akiingia Deo Filikunjombe na kangi lugora lazima moto uwake

Mkuu umenena, nitakuwa confortable kinoma maana wanaijua ndani nje. Tofauti na wengine wakifika hapo wanalewa saluti kama mmoja wa waliotajwa hapo juu, hadi disco anataka kuitwa afande mbele ya vimwana kibao!!!!
 
Bukyanagandi

JF-Expert Member
Jun 24, 2009
9,160
2,000
Wakuondoka pale ni Watendaji wakuu specifically makatibu wakuu save yule mama naibu katibu mkuu - yule kichwa sana na ajiamini sana, actually mimi ningekuwa na uwezo wa kutehua Waziri ningempa huyo Uwaziri kamili huyo naibu katibu mkuuu wa Wizara ya mambo ya ndani. Kinacho takiwa kufanywa pale ni mabadiriko makubwa kwa wajiliwa wa kudumu hao ndio tatizo - bila ya kutekeleza zoezi hilo hakuna kitakacho badirika, narudia watendaji wakuu ndio matatizo wanapashwa kupigwa transfer kwenda Wizara nyingine au wengine kustaafishwa kabisa.
 
Nikupateje

JF-Expert Member
Dec 22, 2009
1,326
2,000
Wizara ya mambo ya ndani ndiyo inayoongoza kwa mawaziri wake kufukuzwa.

Katika kuuaga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya tujikumbushe mawaziri wa mambo ya ndani waliomaliza salama, waliojihudhuru na waliofukuzwa, Sasa tuanze:-

1. Said Maswanya............alifukuzwa na Nyeyere
2. Ali Hassani Mwinyi ............alijihuzuru katika kashifa ya Teddy Kasela Bantu ya kuuwa wachawi
3. Alhaji Omary Muhaji............alifukuzwa katika ile kashifa ya gari aina ya VOLVO miezi sita tu Volvo zote 60 juu yamawe inasemekana alichukua mlungula
4. Salmin Amour....................alihamishwa kwa usalama
5. Abdala Natepe ............... alifukuzwa ile kashifa ya wahaini kukimbia magereza ukonga akina Banyikwa
6. Brigadia Mhidin Kimariyo..................alifukuzwa katika kashifa ya gorafa la wizara kuunguwa moto
7. Agustino Lyatonga Mrema..................alifukuzwa baada ya kulewa madaraka, alilewa akawa chakari
8. Mgunya mmoja kwa jina AMIR.......... ALIKIMBLIA Zanzibar kugombea urais akakosa
9. Omary Mapuri ...............alifukuzwa kashifa ya kupiga waandishi wa habari katika barracks za magereza
10. Laurence Masha ....................... alifukuzwa na wanainchi wa Mwanza
11. Emmanuel Mnchimbi ..................... huyu alifukuzwa na vumbi likatimka

Hebu nisaidieni niliowasahau.

Mrema hakufukuzwa kama unavyodai. Rais Mwinyi baada ya kukemewa na Nyerere alimfukuza Waziri Mkuu na ikabidi avunje Baraza lake la Mawaziri na akaitumia nafasi hiyo kumhamisha Mrema kutoka Mambo ya Ndani kumpeleka Wizara ya Vijana na Kazi, vilevile akakiondoa cheo cha Naibu Waziri Mkuu.
 
ebaeban

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
2,196
2,000
Mrema hakufukuzwa kama unavyodai. Rais Mwinyi baada ya kukemewa na Nyerere alimfukuza Waziri Mkuu na ikabidi avunje Baraza lake la Mawaziri na akaitumia nafasi hiyo kumhamisha Mrema kutoka Mambo ya Ndani kumpeleka Wizara ya Vijana na Kazi, vilevile akakiondoa cheo cha Naibu Waziri Mkuu.

All in all mtoa mada, nakukubaliana nae kabisa Agustino Lyatonga Mrema alifukuzwa kwenye hiyo wizara kwa sababu alivyohamishiwa kwenye wizara ya kazi aliona kama wizara imekuwa ndogo ndipo alipoasi na kujifuza mwenyewe kwa hiyo mtoa mada yuko sahihi alifukuzwa.

My in put ni kwa Mzee Mwinyi aliyemponza siyo Teddy Kasela Bantu bali ni baba yake Teddy aliyeitwa Joseph Kasela Bantu, Tedy alikuwa mbunge wa Bukene kabla hajafukuzwa na wanainchi

Pia Laurence Masha hakufukuzwa na wanainchi wa Mwanza bali alifukuzwa na tume ya uchaguzi kwa sababu aliisha chonga deal kwa kutumia madaraka yake kuwa Wenje siyo raia ni tume ndiyo ilibumbuluwa deal akaja kufukuzwa.

Pia mtoa mada aliyemwachia wizara Mrema siyo huyo mgunya Ali Ameir Mohamedy bali ni msukuma mmoja akiitwa Arnest Nyanda huyu ndiye aliyetoa siri kwamaba baada ya Mrema kumkabidhi wizara alichukua condom zake akaondoka, pia huyu maziri alianza ugomnvi na waandishi wa habari ati wanawachora viongozi kwa ujumbe wa katuni, huyu nae bahati alifariki naye angefukuzwa tu kwa mwenendo alioingia nao.

Mchango wangu ni huo bwana ebaeban.
 
Basi malizia vizuri useme kabisa kwamba hata Jakaya Mrisho Kikwete naye alifukuzwa toka Wizara ya Maji na Nishati kwenda Wizara ya Fedha, siku ileile Augustine Mrema alipofukuzwa toka Wizara ya mambo ya Ndani kwenda Wizara ya Vijana na Kazi!!!!!

Ben Mugashe, Pasco
 
pazzy

Senior Member
Feb 5, 2012
194
195
Kwa sababu ni wizara kioo kwa serikali

Pale akiingia Deo Filikunjombe na kangi lugora lazima moto uwake

hayo ni mawazo yako lkn wenye mamlaka ya Uteuzi wao wanaangalia nani atawatumia POLISI kuwadhibiti chadema..!Amini uteuzi wakulindana umesababisha askari wadogo waichukie serikali ya ccm kwakuwa Imeshindwa kuwajali...Mf;malipo yao ya safali na likizo yamezuiliwa makao makuu,Nyongeza ya posho ya chakula kutoka 150,000/= kwenda 225,000/= Imeendelea kuwa ndoto..!
 
Afande Kirusi

Senior Member
Mar 15, 2018
110
250
Hii nawakumbusha nyinyi wapiga kelele kua

Mwigulu si wakwanza,mtaleta siasa lakini ukweli ni kua hakuna wizara ngumu inayodumu na waziri kwa muda mrefu kama wizara ya mambo ya ndani

Walikuepo akina nchimbi,nahodha nk lakini haijawai kudumu na kichwa Mda mrefu

Ni wizara inayobeba maisha na uhai wa watanzania,unapopewa hii wizara kua makini

Hata mzee wangu kangi(mzee wa mizura) piga kazi haswa.Hii wizara hua haidumu na mtu

Mwigulu si wakwanza wala wa mwisho,nashangaa mnaotaka kukuza mjadala wakati ukweli mnaujua

Mungu ibariki tanzania,Rais na watu wake

ameen
 
DR. MWAKABANJE

JF-Expert Member
Nov 7, 2012
1,973
2,000
Ukweli ni kwamba wengi wa mawaziri wanatumbuliwa awamu hii si kwa sababu waneshindwa kutekeleza wajibu wao kwa wananchi bali ni kwa sababu wameshindwa kutekeleza matakwa ya boss ambayo wakati mwingi hayako sahihi
 
Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
10,489
2,000
Hii nawakumbusha nyinyi wapiga kelele kua

Mwigulu si wakwanza,mtaleta siasa lakini ukweli ni kua hakuna wizara ngumu inayodumu na waziri kwa muda mrefu kama wizara ya mambo ya ndani

Walikuepo akina nchimbi,nahodha nk lakini haijawai kudumu na kichwa Mda mrefu

Ni wizara inayobeba maisha na uhai wa watanzania,unapopewa hii wizara kua makini

Hata mzee wangu kangi(mzee wa mizura) piga kazi haswa.Hii wizara hua haidumu na mtu

Mwigulu si wakwanza wala wa mwisho,nashangaa mnaotaka kukuza mjadala wakati ukweli mnaujua

Mungu ibariki tanzania,Rais na watu wake

ameen
Hata Mzee Mwinyi yalishamkuta enzi za Mwalimu
 
ELI-91

JF-Expert Member
Aug 24, 2014
3,589
2,000
kungekua na nafasi za ubunge wa kuteuliwa na raisi, basi hapo alifaa IGP mstaafu mwenye busara kama Mangu ateuliwe kuiongoza wizara. angeelewana vizuri na maafande wenzake, huyu "clown" wa sasa japo alikua polisi lakini hana busara
 
gunz

JF-Expert Member
Jun 30, 2018
312
500
=Tz bado tupo ktk zama za ujima/primitive. Ndo maana kazi ni ngumu
=Wajinga wasiojua kusoma na kuandika bado ni wengi/ illiterates
=teknolojia bado sana /poor
=katiba. Sheria bado hazipo vizuri. Sheria zingine za mwaka 47
=rushwa n.k

Mwisho
Weka mambo vizuri kama miundombinu,elimu kwa raia,sheria zinazoenda na wakati n.k uone kama kuna wizara ngumu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom