Barua ya wazi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola

MANKA MUSA

JF-Expert Member
Jul 9, 2014
922
1,093
KWA MHE. RAIS NA MHE. WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI
Napenda kumpongeza Mhe. Kangi Lugola kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi nafasi aliyoichukua kutoka kwa mtangulizi wake Mhe. Dr. Mwigulu Lameck Nchemba bila kumsahau Maj. Gen. Kingu Katibu Mkuu mpya wa wizara hii. Lakini pia nimpe pole Mh. Kangi Lugola kwa sababu amekutana na wizara yenye changamoto nyingi sana pengine kuliko wizara nyingine yoyote. Pia nimpe pole kwa sababu amekutana na kipindi ambacho wizara hii yenye dhamana na usalama wa wananchi na mali zao ikiwa imechoka vibaya sana na huku ikikabiliwa na mambo lukuki ya kuyashughulikiwa.

Mhe. Kangi Lugola ameanza kwa mbwembwe sana kazi ya uwaziri katika wizara hii, tunakuomba usizime moto huo, uendelee nao kwa lengo la kuhakikisha wizara hii inakaa katika mstari wake sahihi zaidi kuliko ilivyo sasa, tuko pamoja na tunakuahidi kukupa ushirikiano na wewe tunakuomba utupe ushirikiano hasa kwa kuyasoma na kuyashughulikia yaliyomo na mengine ambayo hatujayaandika humu kutokana na unyeti wake kiusalama.

SUALA LA MASLAHI: Hili tumtupie Mhe. Rais, kama kuna jambo linavunja morali wa maafisa na askari wa vyombo vya ulinzi na usalama vya Wizara ya Mambo ya Ndani ni suala zima la maslahi. Hapa tunamaanisha; mishahara, ration allowances, professional allowances, house allowances, package allowance, electricity allowance, water bill allowance, Hardship allowance n.k. Bwana mkubwa mara kadha umesikika hadharani ukijinadi kuwa wewe ni Amiri jeshi wa majeshi yote ya ulinzi na usalama ambayo ni: JWTZ, TISS, PT, MT, UT, ZMU. Lakini uhalisia ni tofauti, wenzetu wa vyommbo vingine vya ulinzi na usalama wanapata posho zote na mishahara yao iko juu kulinganisha na vyombo vya ulinzi na usalama vya Wizara ya Mambo ya Ndani. Kwa mfano Private wa JWTZ mshahara wake ni mkubwa kulinganisha na Constable wa Wizara ya Mambo ya Ndani. Kibaya zaidi Afisa wa JWTZ kama Luteni Usu, mshahara wake ni mara mbili zaidi ya Assistant Inspector wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vya Wizara ya Mambo ya Ndani. Kapteni wa JWTZ anamuacha mbali kwa mshahara Mrakibu Mwandamizi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani. Tumeamua kufikisha kilio chetu kwa njia hii kwa sababu inavunja mioyo ya maafisa na askari yaani ni kama vile tunafanya kazi katika serikali mbili tofauti na huku sote tunafanya kazi za aina moja, utofauti wa kikazi ni mgawanyo wa kimajukumu tu ambao hata JWTZ wanao. Askari wa mambo ya ndani si kwamba hawezi kufanya kazi kama askari wa Navy, Airforce au Land Force, sote tunaweza kazi za kijeshi na ndiyo maana tunashiriki baadhi ya mafunzo kama JKT na hadi katika kozi za ajira na pia kumbuka sote tunafanya paredi ya pamoja katika sherehe za kitaifa, hiyo ni kuonyesha kwamba sote kwa pamoja ni walinzi wa taifa tuliogawanyika katika majeshi tofauti ili tu kazi za ulinzi ziende kwa ufanisi zaidi.

HAKUNA AFISA/ASKARI ALIYE MUHIMU/BORA ZAIDI KULIKO MWINGINE.

SUALA LA NIDHAMU NA KUACHISHWA KAZI: Hapa tumgeukie Mhe.Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Katibu Mkuu wa Wizara. Kuna tatizo kubwa sana katika Vyombo vya Ulinzi na Usalama vya Mambo ya Ndani kuhusu mfumo wa kuwashughulikia askari na maafisa wanaokwenda kinyume katika kufuata sheria, kanuni na taratibu za kijeshi. Ni kweli kuwa hakuna mwajiri ambaye yuko tayari kuvumilia mwajiriwa ambaye hana nidhamu, lakini basi taratibu za kimajeshi zifuatwe ili kuweka sawa mizania katika majeshi yetu. Hakuna haki katika kusikilizwa mashitaka na hukumu huwa ni za hovyo na zisizolenga maslahi ya askari/afisa na bila kujali usalama wa nchi. Unapofukuza hovyo askari na bado unalalamika ongezeko la uhalifu huko mitaani, unapaswa kujitafakari upya. Hao mnaowafukuza hovyo hatimaye ndiyo huwa majambazi kwa sababu wana elimu kubwa ya kijeshi na bado wana nguvu na hatimaye ni kutumia elimu hiyo ya kijeshi kwa njia hasi. USHAURI: Mhe. Waziri tunakuomba uunde kamati teule ya wizara ikiwa na wakuu wote kama IGP, CGP, CGI, CGF wakiongozana na wataalamu wa sheria na wataalamu wa utumishi kutoka katika vyombo vyote hivi kwa pamoja muende wizara ya ulinzi, mkajifunze namna ya mfumo wa kisheria wa kijeshi kutoka kwa JWTZ, natumai Afande CDF kwa kushirikiana na Mhe. Waziri wa Ulinzi watawapatia msaada wa kutosha ili hatimaye suala la kuendesha kesi za kinidhamu za kijeshi liwe zuri na makamanda wa mikoa wakose nafasi ya kufukuza kazi watu hovyo jambo linalochochea ongezeko la wahalifu mitaani.

MAFUNZO: Bado tupo nawe Mhe. Waziri, Kuna tatizo la ulegevu wa mafunzo katika vyombo vyetu vya mambo ya ndani kwa mfano POLICE, UHAMIAJI na ZIMAMOTO. Kwa mfano kozi ya awali ya Police ni ndefu sana na haina tija. Muda mwingi unapotea kwa askari mwanafunzi kufundishwa kubrashi viatu, kufua na kunyoosha nguo jambo ambalo linaweza kufundishwa kwa mwezi mmoja lakini linakua ni somo endelevu la miezi 9 ukiondoa wiki sita za mafunzo ya kijeshi porini. Hakuna sababu ya kua na kozi kama hizi zisizo na tija na kutumia teknolojia ya kizamani ya pasi ya mkaa na huku tupo katika karne ya sayansi na teknolojia ambapo nishati ya umeme, gesi zipo na zinapaswa kutumika ili kuokoa muda wa mafunzo na kumuandaa askari mpya kuwa ni askari wa kisasa anayeweza kukabiliana na changamoto za kiuhalifu za kisasa hasa za kiteknolojia. Unapokomalia askari mwanafunzi wa kozi ya awali atumie pasi ya mkaa ni sawa unadunisha uwezo wake wa kufikiria na hana tofauti na mtu wa kijijini ambaye hana utaalamu wowote wa kiteknolojia. Pia unakua unawaibia Watanzania fedha kwa sababu unalazimisha askari wanafunzi wakae sana mafunzoni bila sababu za msingi huku wakitumia kodi za Watanzania. Mfumo wa mafunzo uwe wa muda mfupi, masomo ya darasani yawepo ya kushibisha bongo za kuruti, mazoezi ya kimwili hasa mbio za jioni ziwepo ili kuimarisha afya za kuruti wa mwili. Kwa upande wa mafunzo ya kupandishwa vyeo [promotion rank courses] pia hali si shwari sana. Nendeni JWTZ mkajifunze namna wenzenu walivyoweka sawa mifumo ya kozi kuanzia RECRUIT, LEVEL 3, LEVEL 2, LEVEL 1, JUNIOR NCO, SENIOR NCO, CADET, KUP, KUK n.k. Kingine pia, kila kitengo awekwe afisa au askari ambaye amefanyia kozi kitengo husika. Unapomuweka Afisa au askari amabye hana ujuzi wa litengp husika, usitarajie matokeo mazuri kiufanisi kazini.

KUDHARAULIWA NA MAJESHI MENGINE/KUDHARAULINA/ KUDHARAULIWA NA RAIA: Tunadharauliwa na wenzetu wa vyombo vingine vya ulinzi na usalama kutokana na kozi soft tunazofanya wizara ya mambo ya ndani, pia mfumo wetu wa GAZETTED OFFICERS unatufanya tudharaulike kulinganisha na wenzetu COMMISSIONED OFFICERS. Tunaomba kadiri itavyowezekana, tuwe na mfumo wa pamoja wa kozi ili kuondoa hali hii kwa sababu hata raia wanatudharau kutokana na ulaini wa mafunzo ya vyombo vya wizara ya mambo ya ndani. Tunaweza kufanya mafunzo yote kama wafanyayo wenzetu hasa wa wizara ya ulinzi na tunaweza kufanyia mafunzo popote pale katika shule na vyuo vya mafunzo vilivyo chini ya wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa. Hili jambo litaleta heshima na kua na mfumo mmoja wa kimafunzo ya kijeshi ili kuleta umoja na mshikamamo na kuweka sawa mila, desturi na tamaduni za kijeshi. Leo tuna maafisa na askari wa majeshi tofauti ambao wanatofautiana sana katika suala la mila, tamaduni na desturi za kijeshi. Itakapoanza mfumo wa kozi za pamoja itasaidia sana kuwa na mfumo mmoja wa mila, tamaduni na desturi za kijeshi. Usishangae Mhe. Waziri, hii haitokua jambo jipya kwa Tanzania, nenda Kenya ukatazame namna KDF na POLICE wanavyofanya mafunzo ya kijeshi kwa pamoja na hali hii imeleta heshima sana kwa maafisa na askari wa vyombo hivyo, lakini kwa hapa kwetu tunapendekeza utaratibu huo kama utawezekana uhusishe: JWTZ, PT, UT, MT, JZMU, TAWA.

UKOSOAJI WA VIONGOZI WA MAJESHI: Mhe. Waziri ulikua ni Afisa wa PT kabla ya kuamua kuacha kazi hiyo ya awali. Natumai wewe ni shahidi kua katika muda wote wa utumishi wako sidhani kama uliwahi kumuona kiongozi wa kisiasa wa ngazi yoyote kuanzia Rais, PM, VP, Mawaziri, RCs, DCs ambaye aliwahi kumuadhiri kiongozi wa kijeshi wa ngazi yoyote ile hadharani. Ni ombi letu kua ufike muda sasa majeshi yarudi katika heshima yake. Mkiona kiongozi wa kijeshi amekosea, tafuteni njia za faragha za kuweza kumuita na kumuonya. Unapomuaibisha kiongozi wa kijeshi tena mwenye uteuzi wa Mhe. Rais, ina maana umemuabisha Mhe. Rais na kumuona Rais hafai kwa sababu ameteua Kiongozi asiyefaa jambo ambalo kwa sisi Wapiganaji na Makamanda linatuuma sana kwa sababu tunawaheshimu sana viongozi wetu na tunamtii, kumheshimu na kumtukuza Amiri Jeshi Mkuu wa taifa letu Mhe. Dr, John Magufuli, hatupendi kuona wanasiasa wanaotaka tuchafukwe nyongo kwa sababu ya kiki za kisiasa.

VITENDEA KAZI: Mhe. Waziri pindi tu ulipoanza kazi ulianza kwa kumshusha cheo RFO wa Kagera kwa kosa la kutokwenda katika tukio la moto. Kuzima moto na kuokoa mali ni taaluma inayojitegemea na ndiyo maana likawekwa jeshi la zimaoto na uokoaji. Huwezi kwenda katika tukio tu kwa sababu ni tukio, unakwenda katika tukio kwa sababu unamudu kukabiliana na tukio husika. Hivi ni mara ngapi tumesikia watu wamekufa makumi kwa mamia katika matukio ya moto? Hivi tunadhani ni suala la urahisi tu wa kuweza kufika katika tukio ndiyo watu waende? Masuala ya kitaalamu waachiwe wataalamu wenyewe. Hadi sasa katika wilaya na vituo vingi hakuna magari, pikipiki, vifaa vya ofisini, radio calls, n.k. hali inayofanya kazi kuwa ngumu. Wakati huo huo maafisa na askari hawa hawana mishahara na posho za kueleweka na bado hata vitendea kazi pia ni tatizo, hivi mnadhani tutafanyaje kazi kwa mtindo huu? Halafu bila hata aibu Mhe. Rais anazungumza kua JZMU hawana magari tangu mwaka 1987, na mzigo wa lawama anatwishwa Waziri aliyeondolewa !! Msipende kucheza na akili za Watanzania, hivi suala la miaka 31 iliyopita inakuwaje atwishwe zigo la lawama waziri ambaye amedumu katika nafasi husika kwa muda usiozidi miaka miwili???

TEUZI: Mhe. Rais mara zote tumeona teuzi zako zilizotukuka zikiwasahau makamanda na maafisa wa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyo chini ya wizara ya mambo ya ndani. Tunapenda kukutaarifu kuwa wapo makamanda na maafisa wenye elimu kubwa na sifa zilizotukuka wenye uwezo wa kuongoza katika nafasi mbalimbali kwa mujibu wa teuzi zilivyo. Tungependa kuona mseto wa kiuongozi huko uraiani kwa kuwaona makamanda na maafisa wa vyombo vya ulinzi na usalama vya wizara ya mambo ya ndani wakishika nyadhafi mbalimbali za kiuongozi kama wanavyoteuliwa wengine kutoka katika vyombo vingine vya ulinzi na usalama.
MWISHO: Maafisa na askari wa vyombo vya ulinzi na usalama wizara ya mambo ya ndani ya nchi tupo pamoja na Mhe. Amiri Jeshi wetu kipenzi Dr. John Magufuli katika mikakati ya kuipeleka nchi yetu katika uchumi wa kati na uchumi wa viwanda. Tupo tayari kuilinda nchi yetu adhimu kwa gharama yoyote ile, Polisi wapo tayari kulinda raia na mali zao, Zimamoto na Uokoaji wako tayari kukinga madhara yanayoweza kuletwa na moto na maafa mengine, Uhamiaji wako tayari kulinda na kuhakikisha raia wa kigeni wanaingia na kutoka kwa kufuata sheria na kuingizia fedha za kigeni nchi yetu bila kusahau wazawa wanaotoka nje nao wanalipia tozo stahiki kwa faida ya nchi yetu, Magereza wako tayari kulinda magereza yetu na kuzalisha mazao mbalimbali yatakayoiingizia faida nchi yetu.

Tunaomba yote yaliyoandikwa humu yafanyiwe kazi mapema kwa sababu sote ni walinzi wa taifa hili la Tanzania kwa namna moja au nyingine, hatupendi mgawanyiko wa kimajeshi uliopo, tunakuomba Mpendwa wetu Amiri Jeshi Mhe. Dr. John Magufuli kwa kushirikiana na Mhe. Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Katibu mkuu wake, Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyo chini ya wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, uyashughulikie matatizo haya kwa uweledi wa hali ya juu sana bila kusahau kauli ya Mhe. Kipenzi chetu Amiri Jeshi Dr. John Magufuli kuwa HAKUNA AFISA/ASKARI AMBAYE NI BORA KULIKO MWINGINE, MAJESHI YOTE NI YANGU NA YAKO SAWA.

NI SISI MAAFISA NA ASKARI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
 
Hakika JF ni jukwaa huru, makamanda wetu wasikilizwe. Naomba mpiganie na kutetea democrasia pia.Bila hiyo hata jukwaa hili lipo hatari ni. Salute kwenu makamanda wetu.
 
Kwa akili ya kawaida kabisa mm nafananisha (mfano usio rasmi).
JWTZ = Madaktari
TISS = Mainjinia
POLISI(na ndugu zake) = Walimu
Haingii akilini kwa hizo kada
1. Kufanya mafunzo yalio sawa
2. Kupata maslahi sawa
3. Kuwa na hadhi sawa kwa watendaji wake, na
4. Kupata heshima iliyo sawa katika jamii.

Hata hivyo hoja ya kufanyiwa maboresho ya kimuundo, kimaslahi na sifa za kiujuzi kwa Idara za usalama za Wizara ya mambo ya ndani ni ya lazima kama tunajali mustakabali mzuri wa taifa letu.

Ni mtizamo tu...
 
Kwa akili ya kawaida kabisa mm nafananisha (mfano usio rasmi).
JWTZ = Madaktari
TISS = Mainjinia
POLISI(na ndugu zake) = Walimu
Haingii akilini kwa hizo kada
1. Kufanya mafunzo yalio sawa
2. Kupata maslahi sawa
3. Kuwa na hadhi sawa kwa watendaji wake, na
4. Kupata heshima iliyo sawa katika jamii.

Hata hivyo hoja ya kufanyiwa maboresho ya kimuundo, kimaslahi na sifa za kiujuzi kwa Idara za usalama za Wizara ya mambo ya ndani ni ya lazima kama tunajali mustakabali mzuri wa taifa letu.

Ni mtizamo tu...
Wewe jamaa unazingua kweli hivi kazi ya TISS unataka kuifananisha na kazi ya kiume ya polisi!! Nenda Ngara huko uone polisi wanavyo fanya kazi au mipakani huko uone polisi wanavyo fanya kazi ya doria ya ndani.TISS ni kazi ya kimama umbea mwiingi.

Ushauri; C in C naomba uondoe haraka hii 'double standard' ambayo iliwekwa na Rais Hb wa awamu ilio pita ambapo aliijali sana Tipidenga na kuyapuuzia majeshi ya Mambo ya ndani.
 
Police Na magereza wanafanya kazi ngumu sana.(Tatizo upendeleo Wa Wana siasa Wa Tanzania)
 
lakin saw unajua nashindwa kuelewa tatizo liko wap yaan wahusika nikama hawaoni huu mgawanyiko wa kimaslai ukiendelea kudumishwa ndani ya majeshi yetu hivi nikweli mh rais haoni hili yaani nikweli haoni humuimu wa hili .bas saw viongoz wote wa ngazi za juu waendelee kuto ona humuimu wa hili swala Go ahead my country
 
lakin saw unajua nashindwa kuelewa tatizo liko wap yaan wahusika nikama hawaoni huu mgawanyiko wa kimaslai ukiendelea kudumishwa ndani ya majeshi yetu hivi nikweli mh rais haoni hili yaani nikweli haoni humuimu wa hili .bas saw viongoz wote wa ngazi za juu waendelee kuto ona humuimu wa hili swala Go ahead my country
Ya ngoswe
 
Ya ngoswe
kiongozi hili linanihusu mm. Baada yakusoma huu uzi mpaka nimeumia yaan hivi ninavyo andika huu uzi nipo kwenye opp moja hivi polin ingawa barabara inapita na mtandao unapatikana Kwa halotel tu. tupo uku kwaajili ya kuzui ualifu uliokuwa unafanywa na majambazi yakilundi yaliyokuwa yakiteka magari na kupola watu pesa na Simu tangu kipindi cha uko nyuma na kwa hii opp imefanikiwa kwa asilimia 95 now magari yanapita kwa raha mpaka mda huu na kuendelea magari yanapita na bila tatizo lolote lakin ukiangalia maslai ni hafifu inauma San.
 
kiongozi hili linanihusu mm. Baada yakusoma huu uzi mpaka nimeumia yaan hivi ninavyo andika huu uzi nipo kwenye opp moja hivi polin ingawa barabara inapita na mtandao unapatikana Kwa halotel tu. tupo uku kwaajili ya kuzui ualifu uliokuwa unafanywa na majambazi yakilundi yaliyokuwa yakiteka magari na kupola watu pesa na Simu tangu kipindi cha uko nyuma na kwa hii opp imefanikiwa kwa asilimia 95 now magari yanapita kwa raha mpaka mda huu na kuendelea magari yanapita na bila tatizo lolote lakin ukiangalia maslai ni hafifu inauma San.
Pole sana Kiongozi!!!! Tatizo mheshimiwa anafikiri nguo ndo zinafanya kazi.
 
Simu ya Lugola huijui ?
You must be a coward, why do you hide behind your mother's skirt. Face the man and tell him.
Usituchoshe hapa.
You are very unprofessional. mxccukjhgeesd
 
kiongozi hili linanihusu mm. Baada yakusoma huu uzi mpaka nimeumia yaan hivi ninavyo andika huu uzi nipo kwenye opp moja hivi polin ingawa barabara inapita na mtandao unapatikana Kwa halotel tu. tupo uku kwaajili ya kuzui ualifu uliokuwa unafanywa na majambazi yakilundi yaliyokuwa yakiteka magari na kupola watu pesa na Simu tangu kipindi cha uko nyuma na kwa hii opp imefanikiwa kwa asilimia 95 now magari yanapita kwa raha mpaka mda huu na kuendelea magari yanapita na bila tatizo lolote lakin ukiangalia maslai ni hafifu inauma San.
Punguzeni siasa jeshinla polisi
 
Tatizo lenu mmewapa uhuru wanasia wawaendeshe wanavyotaka na ninyi bila kutumia akili mkiambiwa piga yule mnapiga haswaa na hata mkiamiwa uweni mnaua mnahitaji kubadilika muwe na mismamo yenu la sivyo mtaendelea kudharaulika maisha yote................
 
Na watumishi wa umma wengine wakalile wapi? Acheni kufuru nyie askari, hayo maalawance mbona mengi sana? Huku hata extra duty ya elfu 30 mpaka kikao cha madiwani kiazimie. Acheni kumkufuru Mungu nyie askari
 
kiongozi hili linanihusu mm. Baada yakusoma huu uzi mpaka nimeumia yaan hivi ninavyo andika huu uzi nipo kwenye opp moja hivi polin ingawa barabara inapita na mtandao unapatikana Kwa halotel tu. tupo uku kwaajili ya kuzui ualifu uliokuwa unafanywa na majambazi yakilundi yaliyokuwa yakiteka magari na kupola watu pesa na Simu tangu kipindi cha uko nyuma na kwa hii opp imefanikiwa kwa asilimia 95 now magari yanapita kwa raha mpaka mda huu na kuendelea magari yanapita na bila tatizo lolote lakin ukiangalia maslai ni hafifu inauma San.
Mnapewa posho zote hizo na bado unasema umeumia? Mnapewa hela mnaenda kuhonga baa mademu zenu
 
Moderator naomba ondoeni huu uzi, ni makosa makubwa saana kwa mambo ya taasisi za ulinzi na usalama kuanikwa mitandaoni, hii hupelekea vyombo hivi kuwa uchi na adui kufahamu mapungufu yenu!!

Zipo njia za kuwasilisha madai au malalamiko sehemu husika ila si kwa kuandika mitandaoni, plz mode ondoeni hii kitu
 
Moderator naomba ondoeni huu uzi, ni makosa makubwa saana kwa mambo ya taasisi za ulinzi na usalama kuanikwa mitandaoni, hii hupelekea vyombo hivi kuwa uchi na adui kufahamu mapungufu yenu!!

Zipo njia za kuwasilisha madai au malalamiko sehemu husika ila si kwa kuandika mitandaoni, plz mode ondoeni hii kitu
Kama utaangalia motto wa JF unasema "Jamii Forums, where we dare to talk openly" and that is the main reason why we are ghosts here with exception to few angels in this forum.

Sitaki kusema mengi ila kama moderators watauondoa huu Uzi ntawashangaa sana
 
Back
Top Bottom