Wizara ya Afya toeni majina ya Ufadhili, mnatupatia mzigo

Kamkunji

Member
Sep 14, 2023
92
272
Habari za wakati huu ndugu zangu,

Huku nilipo sasa imekua shida, kuna vijana hawa(kama watano ama sita hivi), wengi wa fani ya udakitari na famasi hawaishi kwenye korido, walikua admitted kwenye kozi mbalimbali za afya huku, nafikiri hazitolewi bongo,

Wako huku toka August na September, wanasema wameshatumia budget zao walizokuja nazo zimeisha, sasa wanateseka maana unajikuta umegeuka ndugu wa mtu, (breakfast na lunch) inabidi uwashtue waje ofisini kula, dinner sijui wanafanyaje, lakini kusema ukweli wengi wanapumulia mashine, japo wengi naona ni watumishi wa umma, lakin kama mjuavyo pesa ya bongo huku ni kiduchu sana

Kama ikiwapendeza wizara ya Afya, toeni majina ya ufadhili ili hawa ambao hawatafanikiwa kupata bas wajue wanafanyaje (japo mngewapa kipaumbele tu), kama wanarudi bongo ama la, kuliko wakae huku wakisubiri majina yatoke na bado hawawezi kumudu gharama za maisha, japo nilikua nawaza what if mtu akakosa na ameshakaaa huku almost four months, amelipia na registration fee, kaanza na masomo n.k, hebu pitieni kanzidata vizuri muone walioomba hivi vyuo vya nje na kozi zao ambazo nimeona nyingi zina soko muwape pia kipaumbele,

Lakini pia ushauri, kama waliyoyasema ni kweli bhas nina ombi kwenu,
Semester za vyuo vikuu duniani zinatofautiana lakin main nyingi zinaanza August,September na kuendelea, mnaonaje kama haya majina ya ufadhili mngekua mnatoa labda tuseme October mwanzoni kuliko sasa mnavyotoa November katikati au mwishoni, itakuaje kama kozi aliyochaguliwa mtu haitakua na intake ya katikati,

Tanzania inahitaji vijana wenye upeo na exposure, tusilale tu nyumbani, dunia inaenda kasi, tukimbizane nayo

kwenu Ummy Mwalimu na Mollel
 
Kuna shida kubwa sana namna serikali inavyoendesha elimu ya juu hapa nchini, kama kwa mujibu wa mpina watu wanaweza kufisadi trilioni 30 inauma sana kusikia vijana wanahangaishwa kupata ufadhili wa masomo yao ya juu.......mnaua morale wa hao vijana na kuwaathiri kisaikolojia.

Hivi serikali inashindwa hata kuweka tozo ku-raise pesa za kutosha kusomesha vijana elimu ya chuo kikuu......seriously!!! au ndo wana mpango wa kuua elimu ya watoto wa wanyonge ili vizazi vyao pekee ndo waendelee kutawala.​
 
Kwahiyo hizi tozo tulizonazo bado unaona hazitoshi? Una matatizo ya akili ama?
 
Hivi kumbe huwa inawezekana watumishi wa umma wanaamua kutangulia nje ya nchi kusoma halafu hela ya ufadhili itawafuata?

Tulikuwa tunaambiwa mara akaunti yako inatakiwa ioneshe balance ya salio na mambo mengi kibao. Au ipoje?

Sasa kama mpaka mtu amekuwa admitted na kakaa miezi minne, maana yake mamlaka za huko si zinajua huyo mfadhili wake yupo sirias atalipa ada, wasiwasi wa nini kuhisi kama jina halitakuwemo? Je, angeweza kufika huko bila dhamana ya hiyo wizara kweli? Au siku hizi ni rahisi kwenda huko hata kimasomo?

Nauliza tu ili kujifunza, mimi sijui mambo yalivyo kusoma nje ya nchi, zaidi ya kuyasoma mitandoni.
 
Pole sana kwa kubaki nyuma kiasi hiki, lakini ni vyema nikakupa ABC za duniani

suala la kuomba chuo na kupata si suala la serikali ni suala lako binafsi, baada ya kupata chuo either ndani ama nje ya nchi, unaandika barua ya kuomba ruhusa ya masomo, inayoonesha unaenda kusoma wapi na kozi gani,
ikishakubaliwa unakua huru kuendelea na mambo yako, kama ni kuomba ufadhili ama kujisomesha hayo ni mambo yako,
sasa kwa watu wengi wanaoomba huku ughaibuni semester ziko tofauti na nyumbani unaweza kukuta huku semester inaanza August wakati home inaanza october, kwa hiyo option iliyopo kwa mtu aliyepata chuo cha namna hiyo wengi huamua kujilipia registration fee ili nafasi yake isipotee, na wengine kuanza masomo pia,
huku sehemu ya mdhamini wako ukiandika ni serikali, kwakua wewe ni mtumishi wa umma vyuo vingi vinakua na imani kubwa nawewe na unaruhusiwa kuendelea na masomo wakati ukisubiria serikali yako ifanye jambo
 
issue ya account yako kua na pesa sijui kiasi gani ina apply sana kwa watu ambao hawafungamani na serikali, yaani wanaokuja kujisomesha
 
Hivi kumbe huwa inawezekana watumishi wa umma wanaamua kutangulia nje ya nchi kusoma halafu hela ya ufadhili itawafuata?

Tulikuwa tunaambiwa mara akaunti yako inatakiwa ioneshe balance ya salio na mambo mengi kibao. Au ipoje?

Sasa kama mpaka mtu amekuwa admitted na kakaa miezi minne, maana yake mamlaka za huko si zinajua huyo mfadhili wake yupo sirias atalipa ada, wasiwasi wa nini kuhisi kama jina halitakuwemo? Je, angeweza kufika huko bila dhamana ya hiyo wizara kweli? Au siku hizi ni rahisi kwenda huko hata kimasomo?

Nauliza tu ili kujifunza, mimi sijui mambo yalivyo kusoma nje ya nchi, zaidi ya kuyasoma mitandoni.
hiyo aya ya tatu sitakujibu kwa kua sijaona cha kukujibu, samahani
 
Hivi kumbe huwa inawezekana watumishi wa umma wanaamua kutangulia nje ya nchi kusoma halafu hela ya ufadhili itawafuata?

Tulikuwa tunaambiwa mara akaunti yako inatakiwa ioneshe balance ya salio na mambo mengi kibao. Au ipoje?

Sasa kama mpaka mtu amekuwa admitted na kakaa miezi minne, maana yake mamlaka za huko si zinajua huyo mfadhili wake yupo sirias atalipa ada, wasiwasi wa nini kuhisi kama jina halitakuwemo? Je, angeweza kufika huko bila dhamana ya hiyo wizara kweli? Au siku hizi ni rahisi kwenda huko hata kimasomo?

Nauliza tu ili kujifunza, mimi sijui mambo yalivyo kusoma nje ya nchi, zaidi ya kuyasoma mitandoni.
Balozi nyingi ukishakua na kibali cha serikali kwenda masomoni, hakuna maswali mengi, wanajua hata ukikwama huko utarudi tu, maana umefunga ndoa na serikali,
 
emoji38.png

Pole sana kwa kubaki nyuma kiasi hiki, lakini ni vyema nikakupa ABC za duniani

suala la kuomba chuo na kupata si suala la serikali ni suala lako binafsi, baada ya kupata chuo either ndani ama nje ya nchi, unaandika barua ya kuomba ruhusa ya masomo, inayoonesha unaenda kusoma wapi na kozi gani,
ikishakubaliwa unakua huru kuendelea na mambo yako, kama ni kuomba ufadhili ama kujisomesha hayo ni mambo yako,
sasa kwa watu wengi wanaoomba huku ughaibuni semester ziko tofauti na nyumbani unaweza kukuta huku semester inaanza August wakati home inaanza october, kwa hiyo option iliyopo kwa mtu aliyepata chuo cha namna hiyo wengi huamua kujilipia registration fee ili nafasi yake isipotee, na wengine kuanza masomo pia,
huku sehemu ya mdhamini wako ukiandika ni serikali, kwakua wewe ni mtumishi wa umma vyuo vingi vinakua na imani kubwa nawewe na unaruhusiwa kuendelea na masomo wakati ukisubiria serikali yako ifanye jambo
Thanks, nimejifunza mambo kadhaa
 
Habari za wakati huu ndugu zangu,

Huku nilipo sasa imekua shida, kuna vijana hawa(kama watano ama sita hivi), wengi wa fani ya udakitari na famasi hawaishi kwenye korido, walikua admitted kwenye kozi mbalimbali za afya huku, nafikiri hazitolewi bongo,

Wako huku toka August na September, wanasema wameshatumia budget zao walizokuja nazo zimeisha, sasa wanateseka maana unajikuta umegeuka ndugu wa mtu, (breakfast na lunch) inabidi uwashtue waje ofisini kula, dinner sijui wanafanyaje, lakini kusema ukweli wengi wanapumulia mashine, japo wengi naona ni watumishi wa umma, lakin kama mjuavyo pesa ya bongo huku ni kiduchu sana

Kama ikiwapendeza wizara ya Afya, toeni majina ya ufadhili ili hawa ambao hawatafanikiwa kupata bas wajue wanafanyaje (japo mngewapa kipaumbele tu), kama wanarudi bongo ama la, kuliko wakae huku wakisubiri majina yatoke na bado hawawezi kumudu gharama za maisha, japo nilikua nawaza what if mtu akakosa na ameshakaaa huku almost four months, amelipia na registration fee, kaanza na masomo n.k, hebu pitieni kanzidata vizuri muone walioomba hivi vyuo vya nje na kozi zao ambazo nimeona nyingi zina soko muwape pia kipaumbele,

Lakini pia ushauri, kama waliyoyasema ni kweli bhas nina ombi kwenu,
Semester za vyuo vikuu duniani zinatofautiana lakin main nyingi zinaanza August,September na kuendelea, mnaonaje kama haya majina ya ufadhili mngekua mnatoa labda tuseme October mwanzoni kuliko sasa mnavyotoa November katikati au mwishoni, itakuaje kama kozi aliyochaguliwa mtu haitakua na intake ya katikati,

Tanzania inahitaji vijana wenye upeo na exposure, tusilale tu nyumbani, dunia inaenda kasi, tukimbizane nayo

kwenu Ummy Mwalimu na Mollel
Kwa uungwana kabisa naomba kutoa updates ya suala hili.
Kwanza niwashukuru Wizara ya Afya na Serikali yangu kwa ujumla, majina yalitoka na vijana wote sita wamesema wamepata ufadhili,
wanasema wamewasilisha documents Dodoma kupitia kwa ndugu zao, hivyo rai yangu kwa serikali yangu, wafanyieni upesi ili waweze kuendelea na masomo yao vyema bila vikwazo, maana kwa uzoefu wangu najua ilivyo ngumu kukaa ugenini
mchakato ufanyike mapema na waingiziwe pesa zao(wanasema wenzao wanawaambia mwaka jana majina yametoka November sijui na pesa imekuja kutoka May mwaka huu, hii siyo sawa), ili tuendelee kuongeza wataalamu hasa hawa waliothubutu kuongeza elimu nje ya nchi, kwa kua si kila mtu anaweza kukubali kuondoka nchini mwake kwenda mbali kisa kutafuta elimu wakati angeweza kusoma kufuata mkumbo maana kozi ziko kibao hapo bongo, hakika taifa letu limebarikiwa
 
Back
Top Bottom