Wizara ya Afya: 94% ya Watanzania wapo katika hatari ya kupata maambukizi ya Malaria katika kipindi cha mwaka mzima

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Kwa mujibu wa Takwimu za Wizara ya Afya, 94% ya Watanzania wapo katika hatari ya kupata maambukizi ya Ugonjwa wa #Malaria katika kipindi cha mwaka mzima. Hayo yameelezwa na Waziri Ummy Mwalimu katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani

Amesema kwa Mujibu wa takwimu za Mwaka 2021, kati ya kila Wagonjwa 100 waliohudhuria Hospitali/Zahanati/Vituo vya Afya, 10.6 kati yao walihudhuria kwasababu ya Malaria

Ameeleza, "Bado Ugonjwa huu unaweka mzigo mkubwa katika utoaji Huduma za Afya, bado ni chanzo cha vifo vya Watanzania. Mikoa inayoongoza kuwa na kiwango kikubwa cha maambukizi ni Kigoma, Kagera, Geita, Mtwara, Lindi na Ruvuma"
 
Kwahiyo 6% tu ndo hawata ugua maleria, na bajeti yao kila mwaka kuna kutoa vyandalua, elimu kuhusu malaria kwa ufupi hiyo wizara ni failure kabisa.
 
Huu ugonjwa munaulea wenyewe,
Hivi zile centre zinazofanya uchunguzi wa mbu pale jangwani, kule amani muheza tanga na kwingineko kuna umuhimu kweli hao wazungu waje wafanyie hizo tafiti huku?
Kwanini wasifanyie kwao? Mimi nadhani wanatuzalishia mbu kwa matoleo vile wanaona inafaa
Hawafai kabisa hawa wazungu,
Algeria walifukuza hawa na matokeo yake ndani ya mwaka mbili tu ni malaria free country
 
Back
Top Bottom