Wivu kwa mchepuko

Wivu kwa mchepuko

Ha ha haaah....mpendwa wakati mwingine labda heavy traffic au mashimo mashimo yaliyoko njia kuu ndio yanaweza ku-dictate mtu uchepuke. Just thinking though!! Ha ha haah
Tatizo ukienda mchepukoni na ukakutana na jam kutoka inakuwa ishu.....bora njia kuu ....foleni ikiisha mnatembea fasta......ni kuvumilia tu na kuyafukia mashimo ya njia kuu ili muende sawa........
 
R mbuna,ni nini ulicho kosa kwa mkeo mpaka una fanya mambo kama hayo!!je hiyo papuchi mkeo hana?maisha yenyewe ya kulenga kwa manati,jaman mbona mkeo ni mzuri hivyo! Ngoja wajanja wampitie mana kama una mchepuko na yeye anatakiwa kuwa nao ili iwe ngoma droo!!! Kati ya wanaume wapuuzi we ni number moja.
 
ulimheshimu zaidi ya mke wako mpaka kumtoa dodoma na kumpangisha mjini sasa anakuona fala, huyo ni kama mke wako mdogo maana naye umembeba mgongoni kwako sasa dawa yake ndogo mkwapue kila kitu, chukua duka lako,kitanda,king'amuzi flat tv yako mpaka bakuli mpelekee mke wako kipenzi ambaye anakusaliti kwa heshima siyo huyo msaliti wa wazi wazi.
 
pole kaka huenda mke wako nae kaenda kwa mchepuko wake....tulia na familia yako...tatizo wew ni kivulana na sio mwanamme ....mwanamme aliyekamilika hachepuki huwa anawaza aifanyie nin familia yake ili wajivunie kuwa nae na sio kuhangaika na micheppuko....badilika kaka...
 
eeeeh, mchepuko sio mali yako wivu wa nini? ukishamfanya mwenzio mchepuko ujue na ww kwake ni mchepuko vile vile
 
Hujafanywa mjinga bali ndio nyumbani kwao na ujinga
 
Habari za wakati huu wana MMU,

Juma mosi ya juzi nilivyotoka kazini nikawa sina mahali pakwenda kupumzika kama mnavyojua hiyo siku huwa tunafanya kazi nusu siku .

Mke wangu kipenzi alikuwa amesafiri so nikaona niende kwa mchepuko wangu bila kutoa taarifa kwake. Nilivyofika mlangoni nikaona kuna sandals za kiume sikuwa na shaka ila radio ilifunguliwa kwa sauti ya juu sana.

Niligonga mlango wala sikupata majibu yoyote ikabidi nimpigie simu lakini haikupokelewa.Ikabidi nisepe ila roho ilikuwa inaniuma sana.

Baada ya dakika tano wala sikuwa nimefika mbali akanibip nikampigia.Akasema nipo kwenye gari simu ilivyoita sikuisikia, Nikamuuliza nyumbani kuna mtu akasema nyumba ameifunga so hakuna mtu. Nikasikia hasira sana yaani amenifanya mimi boya.

Ikabidi nigeuze nirudi mpaka pale kwake ili nihakikishe kama kweli hakuna mtu au niliangalia vibaya.Bahati nzuri pale nilimfungulia biashara ya kuuza duka na duka lilikuwa wazi nikaenda dukani nikajifanya nahitaji kununua bidhaa pale mara akatoka yeye alivyoniona alipata mshtuko mpaka akawa ameganda tu pale hata hajanisemesha mbaya zaidi alikuwa amevaa upande tu wa kanga.

Nikamuuliza umerudi saa ngapi hakujibu nikamwaambia endelea na maisha yako mama siwezi kupigana mimi.

Jana jumapili ilipita kimya hakunisumbua wala nini ila leo nashangaa ghafla nakuta msg ya kuomba msamaha na maelezo kibao wala sijamjibu mpaka sasa na nilishatia nia ya kumuacha moja kwa moja kwa sababu sina nguvu za kupigania papuchi.

Kwa wale wazoefu hivi roho inapouma kwa mchepuko wako kuchepuka katika nyumba unayolipia kodi ni dalili ya wivu au ni kujihisi umefanywa mjinga?

Mbona ni kawaida sana, yule ni mchepuko na anajitambua, hivyo anajuwa fika wewe hutamuoa kwa hiyo anatupia kete kwingineko kujaribu bahati yake. Asikudanganye mtu, wanawake hawapendi kufanywa mchepuko ila hawana jinsi tu.
 
Habari za wakati huu wana MMU,

Juma mosi ya juzi nilivyotoka kazini nikawa sina mahali pakwenda kupumzika kama mnavyojua hiyo siku huwa tunafanya kazi nusu siku .

Mke wangu kipenzi alikuwa amesafiri so nikaona niende kwa mchepuko wangu bila kutoa taarifa kwake. Nilivyofika mlangoni nikaona kuna sandals za kiume sikuwa na shaka ila radio ilifunguliwa kwa sauti ya juu sana.

Niligonga mlango wala sikupata majibu yoyote ikabidi nimpigie simu lakini haikupokelewa.Ikabidi nisepe ila roho ilikuwa inaniuma sana.

Baada ya dakika tano wala sikuwa nimefika mbali akanibip nikampigia.Akasema nipo kwenye gari simu ilivyoita sikuisikia, Nikamuuliza nyumbani kuna mtu akasema nyumba ameifunga so hakuna mtu. Nikasikia hasira sana yaani amenifanya mimi boya.

Ikabidi nigeuze nirudi mpaka pale kwake ili nihakikishe kama kweli hakuna mtu au niliangalia vibaya.Bahati nzuri pale nilimfungulia biashara ya kuuza duka na duka lilikuwa wazi nikaenda dukani nikajifanya nahitaji kununua bidhaa pale mara akatoka yeye alivyoniona alipata mshtuko mpaka akawa ameganda tu pale hata hajanisemesha mbaya zaidi alikuwa amevaa upande tu wa kanga.

Nikamuuliza umerudi saa ngapi hakujibu nikamwaambia endelea na maisha yako mama siwezi kupigana mimi.

Jana jumapili ilipita kimya hakunisumbua wala nini ila leo nashangaa ghafla nakuta msg ya kuomba msamaha na maelezo kibao wala sijamjibu mpaka sasa na nilishatia nia ya kumuacha moja kwa moja kwa sababu sina nguvu za kupigania papuchi.

Kwa wale wazoefu hivi roho inapouma kwa mchepuko wako kuchepuka katika nyumba unayolipia kodi ni dalili ya wivu au ni kujihisi umefanywa mjinga?
Mi naona kafanya vzur tu,we una mmke bado ukuni unakuendesha mbio na ukongwe wote huo mmkuu.mpotezeee
 
Back
Top Bottom